Dk. Ali Mzige
WANAWAKE wanaochelewa kubeba ujauzito, wameonywa kuwa kuchelewa huko
kunawaweka hatarini kuja kupata watoto wenye mtindio wa ubongo.
Mbali na hilo, pia wanaume wanaotafuta watoto wakiwa katika umri
mkubwa wa zaidi ya miaka 60, nao wametajwa kuwa hatarini kupata watoto
wa aina hiyo na wakiepuka hilo, watakosa uwezo mzuri wa akili darasani.
Taarifa ya daktari mkongwe nchini, Dk Ali Mzige aliyotoa wiki hii,
amebainisha kuwa hali ya umri mkubwa wa wazazi wa kike na kiume, ndio
chanzo kikubwa cha kuzaliwa kwa watoto wa aina hiyo, na siyo uchawi wala
mazingaombwe.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
“Naomba niweke wazi kwamba, mama mwenye umri zaidi ya miaka 35 kama
ndio anaanza kuzaa kwa mara ya kwanza, Mungu aepushie mbali, lakini ana
uwezekano mkubwa wa kupata mtoto mwenye mtindio wa ubongo. “Mbali na
hayo, pia kwa baba mwenye umri mkubwa miaka zaidi ya 60 na ushei,
akitaka kutafuta mtoto uwezekano upo wa kupata mtoto mwenye mtindio wa
ubongo. Kwa hiyo ushauri wangu kwa wazee wenzangu tunaostaafu sasa,
tulee wajukuu tusianze tena kutotoa vifaranga,” ameeleza Dk Mzige katika
taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Dk Mzige, kisayansi umri mzuri wa kuoa au kuolewa na
kuzaa kupata watoto wenye afya nzuri, ni kati ya miaka 18 na 35 kwa
pande zote mbili baba na mama.
Changamoto kijamii
Akizungumzia changamoto wanazokabiliana nazo watoto hao, Dk Mzige
alisema ni pamoja na unyanyapaa kutoka katika jamii kwa watoto hao
pamoja na wazazi wa waliowazaa.
Amesema kutokujua chimbuko la mtindio wa ubongo katika jamii,
kumekuwa kukihusishwa na imani za kishirikina, kwamba mzazi amefanya
kila awezalo, ili mwanawe awe na mtindio wa ubongo, ili apate mali na
kutajirika.
Mbali na wazazi kuonekana kusababisha mtoto wao kuwa na hali hiyo
kishirikina, Dk Mzige alisema watoto hao pia wamekuwa wakitengwa na
jamii na wakikua hasa wanawake, hudhalilishwa kijinsia ikiwemo kubakwa.
“Wengi hunajisiwa na kubakwa na watu wenye akili timamu, kwa imani
kuwa kufanya tendo hilo na mtu mwenye ulemavu, utapata utajiri na
mafanikio mazuri katika shughuli zako,” alisema.
Changamoto kiakili Alisema wanaozaliwa wakiwa na mtindio wa ubongo,
huchelewa kukua kiakili na kimaumbile, ni wapole sana hawana fujo kama
watoto wengine wanaozaliwa kikamilifu.
Pia huchelewa kutambaa, kunyanyuka, kuzungumza na wanakuwa na misuli
ambayo ni dhaifu haina nguvu ya kusukuma na kupiga mateke kama watoto
wengine.
“Uelewa wao kiakili uko katika asilimia 50 (IQ), ukilinganishwa na
watoto wa kawaida ambao wana uelewa na ufahamu wa asilima 100,” alisema
Dk Mzige.
Dk Mzige pia alifafanua kuwa kama baba atakuwa na umri wa zaidi ya
miaka 60, kama mtoto hatazaliwa na mtindio wa ubongo, mtoto huyo kiakili
atakuwa na kasoro endapo umri wa baba utakuwa umesogea na yeye bado
anaendelea kupata watoto.
Aidha wanaozaliwa na tatizo hilo, magonjwa makuu yanayosababisha vifo
kwao ni saratani ya damu (leukemia) na magonjwa ya moyo na wengi
hawafikishi umri wa kuishi wa miaka 40. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na Habari Leo
No comments:
Post a Comment