MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wilayani
Mbogwe mkoani Geita Omari Atanas, amekamatwa na maofisa Uhamiaji
wilayani hapa kurudishwa kwao nchini Rwanda baada ya kubainika sio raia
wa Tanzania.
Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Mkuu wa wilaya hiyo, Aman Mwenegoha,
alisema Mwenyekiti huyo alikamatwa Desemba 22, mwaka huu na maofisa
Uhamiaji na kuhojiwa kwa muda na kugundulika sio raia wa Tanzania bali
ni raia wa Rwanda.
Mwenegoha alisema , awali tetesi za uraia wa Atanas, zilianza wakati
wa kampeni za Uchaguzi wa Serikali wa Mitaa uliofanyika hivi karibuni
nchini, baada ya Mwenyekiti huyo kufika kijiji cha Luganga. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Baada ya kufika kijijini hapo ambapo inadaiwa kuna Wanyarwanda wengi
aliwahamasisha kufanya vurugu kwa kuwa serikali haitaki kuwapa vibali
vya uraia.
Mwenegoha alisema baada ya mahojiano ya siku tatu, ndipo ilibainika
kuwa mwenyekiti huyo sio raia wa Tanzania bali wa Rwanda na
walimsafirisha hadi Rwanda, ambako alitambuliwa ni raia wa nchi hiyo na
ana mke na watoto wawili.
“Baada ya kumfikisha Rwanda wale maofisa walimhoji na baadaye
kumtambua kuwa ni raia wa nchi hiyo na wakati anakuja Tanzania walimpa
kitambulisho, zaidi ya miaka 15, iliyopita na wakamgundua kuwa anayo
familia ya mke na watoto wawili”, alisema Mwenegoha.
Kwa upande wake, Atanas alisema alifika nchini mwaka 2000 na kuishi
katika Kitongoji cha Manzese kata ya Busoka wilayani Kahama, ambapo
mwaka 2003 alihamia kijiji cha Luganga wilayani Mbogwe na kuishi hapo
hadi alipokamatwa mwanzoni mwa wiki hii.
Kuhusu wahamiaji waliopo katika wilaya hiyo, Mwenegoha alisema
wahamiaji 14, ndio walioomba uraia wa Tanzania na kupewa baada ya kukana
uraia wa nchi zao na kwamba katika orodha hiyo yeye hayumo.
Hata hivyo Atanas anadaiwa baada ya kukamatwa na kurudishwa kwao
ameacha deni la Sh milioni 1.5 alizokopa kutoka kwa Katibu Mwenezi wa
Chadema (hivi sasa kahamia CCM) kwa ajili ya kufanya kampeni katika
uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Mwenegoha alisema pamoja na yote
kunaonekana kuna uzembe mkubwa uliofanywa na uhamiaji wilayani humo kwa
kushindwa kumbaini mapema kiongozi huyo ambapo alisema atakaa na kamati
ya ulinzi na usalama wa wilaya hiyo ili kujadili suala hilo. Hata hivyo
Mwenegoha alisema kwa sasa wanajipanga kufanya operesheni kubwa ya
kuwasaka wahamiaji wote haramu ili sheria ichukue mkondo wake ikiwemo
kuwarudisha kwao watakaobainika. Kwa upande wao Chadema walipoulizwa
kuhusu tukio hilo walisema hawana taarifa na kwamba watafuatilia
kufahamu undani wake. Akizungumza na gazeti hili jana, Msemaji wa Chama
hicho, Tumaini Makene alisema, “Ndio kwanza unatupa taarifa hatufahamu
tukio hilo, ila tutafuatilia”, alisema Makene
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
No comments:
Post a Comment