Watu 11 wamefariki katika mkanyagano nchini Zimbabwe baada ya ibada ya kidini kufnayika katika uwanja wa soka.
Polisi wanasema kuwa watu wanne walifariki katika uwanja huo ulio mjini Kwekwe wakati wengine saba wakifariki hospitalini.
Mkanyagano
huo ulitokea wakati maelfu ya waumini wakikimbilia kuondoka uwanjani
humo baada ya ibada iliyoongozwa na mhubiri wa kipentekoste Walter
Magaya.
Mhubiri huyo anadai kuwaponya watu kwa kufanya miujiza.
Baadhi ya walioshuhudia mkanyagano huo wanatuhumu polisi kwa kufunga
baadhi ya milngo ya kuondokea uwanjani humo, huku watu wakiondoka
kupitia mlango mmoja tu.
Hata hivyo polisi wanakana kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya.
Bwana Mugaya ambaye ni mkuu wa kanisa la 'Prophetic Healing and
Deliverance' aliambia vyombo vya habari kuwa alipopata habari ya kutokea
vifo hivyo alihuzunika sana. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment