Wakati Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akisema ofisi yake
imewakutanisha na kumaliza mgogoro baina ya wabunge wawili wa Bunge la
Afrika Mashariki (Eala), mmoja wa wabunge hao, Dk Nderakindo Kessy
amesema hakuna kitu kama hicho.
Dk Kessy jana aliripotiwa na vyombo vya habari
akidai kupigwa na mbunge mwenzake, Shy-Rose Bhanji, akisema
alisababishiwa maumivu makali, lakini likapingwa na Sitta. Jana, sakata hilo lilitinga bungeni na Serikali ikitakiwa kutoa maelezo kwa nini wabunge wa Tanzania wanafanya mambo ya ajabu.
Akijibu swali hilo, Waziri Sitta alisema ilitokea
bahati mbaya Bhanji kupitia CCM akamgonga Dk Kessy (NCCR-Mageuzi) na kwa
kuwa mbunge huyo wa chama tawala alikuwa na haraka kwenda kuwahi gari,
hakusimama, hivyo baadhi ya wabunge wa Uganda wakamshauri Dk Kessy
kwenda kuripoti tukio hilo polisi. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Alifafanua kuwa wabunge hao wamekutanishwa pamoja, wamezungumza yameisha.
Akizungumza na gazeti hili jana, Dk Kessy alisema
tangu tukio hilo lilipotokea hajakutana, kukutanishwa wala kuzungumza na
Bhanji, bali mbunge mwenzake huyo amekuwa akimpita bila kumsemesha
lolote.
Dk Kessy alisema wabunge wa Tanzania katika Bunge hilo wamegawanyika na katika baadhi ya vikao wanavyofanya baadhi yao hawaitwi.
Bhanji, ambaye amekuwa katika mgogoro na wabunge
wenzake kwa kipindi cha miezi miwili sasa na hadi jana alikuwa
hapatikani kwa simu kujibu madai hayo ya kumvamia Dk Kessy na kumpiga
mgongoni. Akizungumza kwa simu kutoka Nairobi, Dk Kessy alisema tukio hilo lilitokea bungeni juzi jioni baada ya kikao kuahirishwa.
Kauli ya Sitta
Jana Mbunge wa Konde (CUF), Khatibu Said Haji
aliomba mwongozo wa Spika akitaka kujua kwa nini baadhi ya wawakilishi
wa nchi katika Bunge la Afrika Mashariki wanafanya mambo ya ajabu hivyo
akataka kujua hatua gani zimechukuliwa dhidi ya Bhanji.
Naibu Spika, Job Ndugai ilimpa nafasi Sitta ambaye
alisema kilichotokea kinahusiana na mgogoro ulioko kati ya wabunge na
Spika wa Eala, Dk Magreth Zziwa.
Na Mwananchi
“Wabunge wamegawanyika pande mbili, kuna wanaotaka Spika abaki
na wengine wanataka aondoke na Tanzania ndiyo kikwazo kwa kuwa wanataka
abaki,” alisema Sitta.
Alisema kilichotokea juzi siyo kama kinavyoelezwa,
kwani Shy-Rose ni mfuasi mkubwa wa Spika hivyo alikuwa anawahi gari
akapita katikati ya wabunge na kumgonga Kessy ambaye alihamaki na kwenda
polisi kufungua madai ya kushambuliwa.
Sitta alisema askari wa Bunge jijini Nairobi
walijaribu kumaliza jambo hilo na kwamba walifanikiwa baada ya kuwaweka
Shy-Rose na Kessy pamoja kisha kuzungumza na kuyamaliza wakati huohuo.
Alisema kuhusu madai ya mambo aliyofanya Shy-Rose
miezi mitatu iliyopita, Serikali inasubiri Tume ya Eala ieleze nini
kilichotokea ili Bunge kama jimbo ichukue uamuzi.
“Kwa sasa hatuwezi kufanya lolote, kuna mambo tunasubiri kwanza ndipo tufanye uamuzi,” alisema Sitta.
Bunge la Eala, tangu mwanzoni mwa mwaka huu,
limekuwa likitawaliwa na vioja na mivutano ya hapa na pale na mikakati
ya kumng’oa Spika Zziwa kwa madai ya kutofanya kazi kwa weledi
ikishindwa kutimia.
Hivi karibuni, Bhanji aliliingiza Bunge hilo
katika mvutano baada ya kudaiwa kuliaibisha wakati wa ziara ya nchini
Ubelgiji iliyowashirikisha wajumbe wa tume na wenyeviti wa kamati za
Bunge akituhumiwa kufanya fujo ndani ya ndege kwa kutoa lugha chafu kwa
wabunge wenzake na wahudumu wa ndege.
Baada ya tukio hilo, baadhi ya wabunge walitaka
Bhanji achukuliwe hatua za kinidhamu, jambo ambalo halijatekelezwa hadi
sasa na kuchochea mgogoro zaidi. Mara zote Bhanji amekuwa akikana tuhuma
dhidi yake na kudai zinalenga kumchafulia jina. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment