Polisi
wawili nchini Tunisia walioshitakiwa kwa kumbaka mwanamke ndani ya gari
la polisi, wameongezewa adhabu katika kesi iliyowashtua wengi.
Maafisa hao walifungwa jela mwezi Machi huku kukiwa na malalamiko kwamba adhabu hiyo haitoshi.Hukumu hiyo, iliongezwa hadi miaka 15 Alhamisi baada ya rufaa kuwasilishwa mahakamani na mwathiriwa wa kitendo hicho cha unyama Meriem Ben Mohamed.
Wakili wake alitaja hatua ya mahakama kuwoangeza adhabu watuhumiwa kama jambo zuri, na pia kusifu ambavyo kesi za ubakaji zinashughulikiwa nchini Tunisia.
Aliambia shirika la habari la AFP, kwamba ameridhishwa na adhabu hiyo.
"lakini bado haitoshi, kwa maoni yangu kwa tendo la kukera kama hilo,'' aliongeza kusema wakili huyo.
Meriem Ben Mohamed alishambuliwa mwaka 2012 na maafisa wa polisi waliosimamisha gari lake alimokuwa na mpenzi wake mjini Tunis. Alikuwa na umri wa miaka 27.
Watuhumiwa walikanusha mashitaka wakisema kuwa waliwapata wawili hao wakiwa wanashirki tendo la ndoa ndani ya gari lao.
Maafisa wa polisi walijaribu kuwashitaki Meriam na mpenzi wake kwa kosa la kukosa maadili lakini maandamano yalifanywa kupinga hatua kama hiyo huku wengi wakiwatetea wawili hao.
Ilisababisha Rais wa Tunisia kumsamehe Meriam na mpenzi wake.
Afisaa mwingine wa tatu aliyejaribu kuwatoza hongo wawili hao, atatumikia kifungo cha miaka miwili alichokuwa amepewa.
Ripoti iliyotolewa na mtaalamu wa kisaikolojia ilisema kuwa yote yaliyotokea yalimsababisha Meriam kusongwa na mawazo.
Kesi hii inatokea wakati ambapo kumekuwa na shinikizo kali kwa serikali kuzingatia haki za wanawake kufuatia kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa Rais Zine al-Abidine Ben Ali.
Na BBC
No comments:
Post a Comment