Papa wa zamani Benedict ameibuka kutoka kwenye ukimya binafsi ndani ya Vatican na kukanusha hadharani kwamba alificha vitendo vya manyanyaso ya kingono kwa watoto na mapadri wa kanisa katoliki.
Katika barua ndefu kwa mtunzi wa
vitabu wa Italia asiye na dini na mwanamahesabu (Piergiorgio Odifredi)
na kuchapishwa jana Jumanne na gazeti la La Republica , Benedict alikana
kutokuwajibika kwa kashfa ya ngono kwa watoto.Lakini amesema kanisa
lazima lifanye kila iwezalo kuzuia vitendo kama hivyo kutokea tena.
Makundi ya waathirika wamemshutumu
Papa huyo kwa kutokufanya vya kutosha kuzuia manyanyaso hayo, kabla ya
kuwa Papa na baada , wakati alipoongoza ofisi ya kanuni ya Kanisa,
ambayo ilihusika na kesi za manyanyayaso.
No comments:
Post a Comment