Mashabiki wake hupendelea kumuita "King of BongoCrunk"....jina halisi ni Ilunga Khalifa a.k.a CPwaa! Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania ambaye baada ya ukimya mrefu sasa kuachia kazi zake mpya.
C.P a.k.a CPwaa mwenye tuzo 3 za
Tanzania Kilimanjaro Music Awards na Multiple Channel O Africa Music
Video Awards nominations anakuja kivingine kabisa mwaka huu. Tarehe 1
mwezi wa October 2013, CPwaa ataachia single yake mpya na ya kwanza
kabisa kwa mwaka huu.Single hiyo iitwayo "Chereko Chereko" yenye mahadhi
ya AfroDance imefanywa chini ya studio za 'De Fatality Music" na
producer "Mesen Selekta" ambaye mwaka huu alichukua tuzo ya mtayarishaji
bora Tanzania anayechipukia.Nyimbo hii itapatikana kwenye mitandao yote
na media zote kuanzia tarehe moja October.
CPwaa
ambaye amesaini mkataba mnono na Universal Music group vile vile
anategemea kuachia single nyingine mwanzoni mwa mwaka 2014 ambapo
amewashirikisha mafahari wengine wawili kutoka Afrika. Single hiyo ya
kimataifa iitwayo "Cross-Borders Therapy" imekutanisha wakali kutoka
mashariki,magharibi na kusini mwa Afrika. CPwaa amemshirikisha "DBlack"
kutoka Ghana, DBlack ni moja ya wasanii wakubwa wa Hip Hop Afrika ambaye
ana tuzo nyingi ikiwemo zile za Channel O.
Kwa upande wa Afrika ya
kusini CPwaa amemshirikisha "Hip Hop Pantsula" a.k.a HHP kwenye nyimbo
hiyo hiyo ya Cross Borders Therapy.HHP ni mmoja ya MaMC wakali kutoka
bondeni mwenye tuzo nyingi ikiwemo ya MTV Base. Nyimbo hii itakuwa ya
kwanza Afrika ambayo imekutanisha wakali kutoka mashariki ,magharibi na
kusini ( The first East,West and South African Hip Hop Collaboration in
History).Nyimbo hii pia imefanyika chini ya producer Mesen Selekta pale
"De Fatality Music" Studio.
Kifuatacho baada ya nyimbo hizi kutoka
ni video zake ambapo Chereko Chereko itafanyiwa Tanzania na Cross
Border Therapy kufanyika nchini Afrika ya kusini. Kwa wale mashabiki
ambao watakuwa na kiu ya wimbo wa Cross Border Therapy ambao utatoka
mwakani wataweza kuupata wimbo huo kupitia iTunes,Amazon, Spotify na
digital store zingine bila kusahau mtandao wa "The Kleek" kwa wale
watumiaji wa smartphones za Samsung na Androids.
No comments:
Post a Comment