Wananchi
wa Zimbabwe leo wanapiga kura ya maoni kuhusu katiba mpya ambayo
itaweka kikomo cha muhula wa urais na kuongeza uhuru wa vyombo vya
habari.
Hata hivyo, wasiwasi
umeongezeka baada ya wanachama kadhaa wa chama cha upinzani cha Waziri
Mkuu Morgan Tsvangirai kushambuliwa wakati wakifanya kampeni katika
kitongoji cha Mbare kwenye mji mkuu Harare, hapo jana.
Msemaji wa chama hicho
cha Movement for Democratic Change-MDC, Douglas Mwonzora, amewashutumu
wafuasi wa Rais Robert Mugabe kuhusika na tukio hilo.
Katiba hiyo mpya itadhibiti mamlaka ya Rais Mugabe na kuweka misingi ya kufanyika kwa uchaguzi mwezi Julai, mwaka huu.
Uchaguzi huo
utahitimisha makubaliano yaliyokumbwa na matatizo ya kugawana madaraka
kati ya Rais Mugabe na Waziri Mkuu Tsvangirai.-DW.
No comments:
Post a Comment