Mwendesha
mashtaka wa Serikali Basilius Namkambe aliaambia Mahakama hiyo Mbele
ya Jaji Samweli Karua kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Mei
15,2011 katika Kijiji cha Mpandapanda kata ya Kiwira Wilayani Rungwe
kinyume na kifungu cha 196(16) kilichofanyiwa marekebisho Mwaka 2002.
Aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni Hakimu Mwakalinga ambaye ndiye mtuhumiwa namba
moja katika kesi hiyo akiwa na Daudi Mwasipesya,Obote Mwanyimbili na
Kelvin Maurus Myovela ambao wanatuhumiwa kumuua John Mwankenja
aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiwira(CCM) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Rungwe.
Awali
baada ya kupandishwa kizimbani watuhumiwa kujibu kesi inayowakabili
yenye namba 31/2012 walimkataa Wakili aliyejulikana kwa jina moja
laMwakabubu aliyekuwa ameteuliwa kwa ajili ya kuwatetea kwa madai kuwa
hawana imani naye kutokana na mwenendo wa kesi alizosimamia.
“Mtukufu
Jaji kabla ya kesi yetu haijaanza kusikilizwa tunaomba kubadilishiwa
Wakili kwa sababu huyu Mwakabubu hana uwezo na tumeona kesi ndogo tu
anababaika na kesi yetu ni kubwa tunaona wazi kabisa kuwa hataweza
kututetea” alisema Mwakalinga Mshitakiwa namba moja.
Kufuatia
ombi hilo Jaji Karua alikubaliana nao ambapo alimteua Wakili mwingine
ambaye ni Sambwee Shitambala ambaye walimkubali kabla hajawaongezea
wakili mwingine ili asaidiane na Shitambala ambapo alimtaja Wakili
Zakia Selemani.
Akisoma
mashtaka yao Mwendesha mashtaka wa Serikali Basilius Namkambe
aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 19, Mei 2011 majira ya jioni
marehemu akiwa anatokea Mbeya mjini akirudinyumbani kwake Kiwira
Wilayani Rungwe alifika Nyumbani akiwa na gari lenye namba za usajili T
127ACZ Nissan (Double cabin).
Namkambe
aliongeza kuwa baada ya kufika nyumbani kwake alipiga honi ya gari kwa
ajili ya kuomba kufunguliwa geti la mlango ambapo baada ya kusikia
honi hiyo alitoka Mjomba wake ambaye baada ya kumfungulia aliambiwa
ashushe Kuku aliyokuwa amewabeba nyuma ya gari yake.
Alisema
kabla ya mjomba wa Marehemu hajaanza kushusha kuku kwenye gari
alitokea mshitakiwa namba moja akiwa na siraha ambapo alimwamuru
asifanye lolote ndipo akaanza kufyatua risasi akimwelekezea marehemu
kisha kumuuana kutoweka kusiko julikana.
Akijibu
tuhuma hizo Wakili wa Utetezi Shitambala na Zakia walikana washtakiwa
hao kuhusika na matukio hayo pamoja na baadhi ya vielelezo
vilivyotolewa na upande wa mashtaka kuthibitisha kuhusika kwa wateja
wao.
Walisema
mtuhumiwa wa kwanza hakuwepo Wilayani Rungwe siku ya tukio ambapo
walisema atakuwa na mashahidi ambao watathibitisha kwamba hakuhusika
ambao waliwataja kuwa ni pamoja na yeye mwenyewe, Askari Magereza
wawili wa gereza la Tukuyu Wilayani Rungwe waliotajwa kwa jina moja moja
la Hereda na Green.
Wengine
ni Padeso Mwakipesile, Aneth Siandene Kalinga na Jumanne Mwakisole
huku washtakiwa namba mbili, tatu na nne ambao hawatakuwa na mashahidi
ambapo watasimama wao wenyewe kujitetea.
Namkambe
aliiambai mahakama hiyo kuwa upande wa mashtaka utakuwa na mashahidi
zaidi ya 15 ambao aliwataja kuwa ni pamoja na Sofia Fungameza, Weston
Gilbert,Magdalena Mgawe, Musa Jackson, Issa Mwaipopo, Teresia Ludovick
na Williamu Mtanga.
Wengine
ni askari Polisi Mwenye namba D2385 Sajent Michael wa Tukuyu, Inspekta
Isaya Bwile wa Tukuyu, David Paul kutoka makao makuu ya Polisi Dar Es
Salaam, Twaha kutoka kitengo cha Upelelezi makao makuu ya Polisi Dar Es
Salaam, Haruna kutoka Polisi Tukuyu na WP3433 Agnes wa polisi Tukuyu.
Namkambe
aliwataja mashahidi wengine katika kesi hiyo kuwa ni pamoja na
aliyekuwa Mkuu wa upelezi (RCO) Mkoa wa Mbeya aliyehamishiwa makao
makuu SSP Anacletus Malindisa, John Mayunga na Dk. D Z Matata kutoka
ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali.
Jaji
Karua aliahirisha kesi hiyo hadi hapo itakapopangwa tena kwa ajili ya
kuendelea na kuwasilikiza mashahidi kutoka upande wa mashtaka baada ya
kuambia mahakama kuwa upelelezi umekamilika na mashahidi wote wako
tayari.
Na Venance Matinya, Mbeya.
No comments:
Post a Comment