Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), imewavua madaraka wakurugenzi wawili.
Mwenyekiti
wa Bodi hiyo, Profesa Cuthbert Mhilu alisema jana kuwa waliovuliwa
madaraka ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora, Dominic Mwakangale
na aliyekuwa Mkurugenzi wa Upimaji na Huduma za Vifungashio, Kezia
Mbwambo.
Profesa
Mhilu alisema hatua hiyo imekuja baada ya bodi hiyo kufanya usaili kwa
vigogo mbalimbali wa shirika hilo ulioanza juzi asubuhi hadi saa 3:00
usiku.
Katika
taarifa hiyo, Profesa Mhilu ambaye hakutaka kuingia kwa ndani juu ya
hatua hiyo, alisema viongozi hao watapangiwa kazi nyingine.
“Kwa
kipindi kirefu, TBS imekuwa ikikabiliwa na matatizo mbalimbali
yaliyochangia kudhoofisha utendaji wa watumishi na kulifanya shirika
kukosa tija na ufanisi. Bodi imeonelea ikae mara moja kuchambua,
kujadili na hatimaye kufikia uamuzi wenye lengo la kuweka mazingira bora
na kuwezesha kuanza utatuzi wa matatizo ili shirika lifikie malengo
yake.”
No comments:
Post a Comment