Katibu wa CCM itikadi na Uenezi Nape Nnauye
--
Chama
Cha Mapinduzi kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kuvamiwa, kupigwa
na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) na Mhariri
Mtendaji wa New Habari 2006 Ndugu Absalom Kibanda usiku wa kuamkia
Jumatano Machi 6, 2013.
Chama
Cha Mapinduzi kinalaani kwa nguvu zote kilichotokea kwa Absalom
Kibanda, kwani ni unyama usiokubalika hata kidogo, unafaa kulaaniwa na
Watanzania wote.
CCM
tunaitaka Serikali kuhakikisha inawapata waliofanya unyama huo na
kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria ili sheria ifuate mkondo wake, na
kukomesha matukio ya namna hiyo.
Aidha,
Chama Cha Mapinduzi kinatoa pole kwa Uongozi wa Jukwaa la Wahariri,
Afisa Mtendaji Mkuu wa New Habari 2006, familia ya Ndugu Kibanda,
wanahabari na wadau wote wa habari nchini, na tunamwombea kwa Mwenyezi
Mungu apone haraka na kurejea katika kazi zake za Ujenzi wa Taifa.
Imetolewa na:
Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UEENEZI
08/03/2013
No comments:
Post a Comment