Naibu
Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini, Mhe.
Stephen Masele, akimuonesha Balozi wa Finland nchini,Sinikka Antila
ramani ya maeneo ambapo kuna madini na uchimbaji unaendelea.
Serikali
imesema inahitaji kujifunza zaidi kutoka Finland hususan katika
uchimbaji wa madini ili kuwa na uchimbaji wenye tija kwa taifa.Hayo
yalisemwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Stephen Masele
alipokutana na Balozi wa Finland nchini, Sinikka Antila.Masele alisema
Tanzania inahitaji kujifunza masuala ya uchimbaji madini kutoka Finland
kwa kuwa mazingira ya uwekezaji ya nchini humo yanashabihiana na
mazingira ya uwekezaji nchini Tanzania.“Unajua kampuni kubwa
zinazojishughulisha na uchimbaji madini nchini Finland siyo za hapo
Finland bali ni kampuni kutoka nchi nyingine yani multi-nationals na
hili pia ndilo linalofanyika hapa kwetu Tanzania” alisema.
No comments:
Post a Comment