Moshi
mweusi ulifuka jana jioni kutoka kwenye dohani huko Vatican ikiwa ni
ishara kwamba Baraza la siri la Makadinali bado halijampata Kiongozi
mpya wa Kanisa Katoliki baada ya kupiga kura ya kwanza.
Mchakato wa
kupiga kura ulianza mapema jana ambapo Makadinali 115 kutoka nchi 48
walikutana kwa faragha ili kumchagua atakaechukua nafasi ya aliyekuwa
papa Benedikt wa 16 aliejiuzulu mwishoni mwa mwezi uliopita.
Zoezi la
kupiga kura litaendelea hadi hapo mmoja wa Makadinali atakapopigiwa
theluthi mbili ya kura yaani kura 77.
Atakaefikia
kiwango hicho atakuwa Baba Mtakatifu wa 266.
Ikiwa
Makadinali, wanaopiga kura watakubaliana juu ya Kiongozi mpya wa Kanisa
Katoliki, moshi mweupe utatoka dohani na kengele zitapigwa kwenye makao
makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican.
No comments:
Post a Comment