Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amekipongeza
kituo cha utamaduni cha Bujora kwa kutunza na kuhifadhi
utamaduni wa mtanzania unaolitambulisha kabila la wasukuma jambo
litakalosaidia kizazi kijacho kuweza kujifunza utamaduni huo.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) ametoa
pongezi hizo hivi karibuni alipokitembelea kituo hicho kilichopo
wilayani Magu katika mkoa wa Mwanza.
Amesema kuwa kituo hicho kimeonyesha mfano
wa kuigwa kwani amejionea na kujifunza mambo mbalimbali ambayo hakuwa
anayafahamu hapo awali kuhusiana na kabila hilo jambo la muhimu
wahakikishe kuwa wanaendelea kutunza utamaduni wao.
Akisoma taarifa ya kituo hicho Padre Fabian
Mhoja ambaye ni Mkurugezi amesema kuwa kituo kilianza mwaka 1954 kikiwa na lengo la kuhifadhi na kuendeleza tunu bora
ya maisha ya watu ili waweze kumfahamu Mungu na kuishi kadiri ya mpango
wake kwa kutumia utamaduni.
Amesema kuwa wanajihusisha na
shughuli za kutunza na kuendeleza urithi wa
utamaduni wa mtanzania kwani kupitia kituo hicho wameweza kutangaza
utalii na utamaduni ndani na nje ya nchi kupitia ngoma , nyimbo na
michezo mbalimbali.
Kituo hicho kimekuwa kikiandaa tamasha la
Bulabo ambapo Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
amekuwa akichangia ufanikishaji wa tamasha hilo ambalo hufanyika kila
mwaka na kukusanya watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment