Moshi mweusi ulifuka jana jioni kutoka
kwenye dohani huko Vatican ikiwa ni ishara kwamba
Baraza la siri la Makadinali bado halijampata Kiongozi mpya wa Kanisa
Katoliki baada ya kupiga kura ya kwanza.
Mchakato wa kupiga kura ulianza mapema jana ambapo Makadinali 115 kutoka nchi 48 walikutana kwa
faragha ili kumchagua atakaechukua nafasi ya aliyekuwa papa Benedikt wa
16 aliejiuzulu mwishoni mwa mwezi uliopita.
Zoezi la kupiga kura litaendelea hadi hapo
mmoja wa Makadinali atakapopigiwa theluthi mbili ya kura yaani kura 77.
Atakaefikia kiwango hicho atakuwa Baba
Mtakatifu wa 266.
Ikiwa Makadinali, wanaopiga kura
watakubaliana juu ya Kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki, moshi mweupe utatoka dohani na kengele zitapigwa kwenye
makao makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican.
No comments:
Post a Comment