Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge
Ngombale Mwiru akisisitiza jambo wakati uzinduzi wa kitabu historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri
Abedi katika hafla
iliyofanyika leo kwenye ukumbi
wa Karimjee jijini Dares Salaam.Kushoto ni Balozi Mstaafu Job Lusinde na
kulia ni Brigedia Hashimu Mbita.
Baadhi wa wadau wakifuatilia
kwa makini uzinduzi
wa kitabu historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi katika hafla
iliyofanyika leo kwenye
ukumbi wa Karimjee jijini Dares Salaam.
Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge
Ngombale Mwiru akizindua kitabu historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri
Abedi katika hafla
iliyofanyika leo kwenye ukumbi
wa Karimjee jijini Dares Salaam. Picha na Magreth Kinabo – Maelezo
*******************************************
NA: FRANK SHIJA & BENEDICT LIWENGA- MAELEZO
VIONGOZI
wahimizwa MWANASIASA mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kuwataka
viongozi nchini kukienzi na kuthamini lugha ya Kiswahili ili kuendelea
kujenga taifa lenye umoja na mshikamano.
Kauli hiyo ilitolewa leo (jana) na Mzee Kingunge ambaye
alikuwa mgeni
ramsi katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Hayati Sheikh
Kaluta Amri Abedi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es
Salaam .
“Hatima
ya Taifa inategemea lugha ya Kiswahili. Viongozi wanawajibu mkubwa
katika kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inakuwa kwani wao ndio
wanaweza kukipandisha au kuiua lugha ya Kiswahili kwakuwa jamii
inawategemea kwa kiasi kikubwa,” alisema Mzee Kingunge.
Aidha Mzee
Kingunge anawaasa kuwa wazalendo na kutumia lugha ya hiyo kwa ufasaha
tofauti na ilivyo sasa katika shughuli mbalimbali mfano Bungeni.
Hata hivyo, aliunga mkono lugha
hiyo kuwa rasmi kufundishia, lakini ametoa changamoto kuwa yatupasa
kuwa makini katika kuitumia hususani katika ngazi elimu ya msingi,
sekondari hadi vyuo vikuu.
Mzee Kingunge alitolea mfano wa wajukuu zake
kuwa masomo mengine kama vile hesabati wanapata alama 90 hadi 95,lakini lugha
hiyo wanapata alama ya 60 mpaka 70. Hivyo inaelekea ufundishaji wake ni
tatizo.
“Kama
kufundisha lugha ya Kiswahili katika elimu ya sekondari ni tatizo na
Kiingereza ni tatizo . Kiswahili kipi kifundishwe katika elimu ya Chuo
Kikuu,”alisema. Huku akitolea mfano kuwa kumekuwa na matumizi ya maneno
ambayo si sahihi kama vile neno masaa badala ya saa.
Kwa upande wake mwanazuoni na mdau wa lugha
hiyo Profesa
Mugyabuso Mulokozi na Profesa Joshua Madumula wameiomba serikali kuwa na
utaratibu wa kuenzi fasihi za Watanzania.
No comments:
Post a Comment