Lema aitisha maandamano
Mbunge
wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, ametangaza kuandaa maandamano
makubwa yatakayoshirikisha wanawake na watoto katika Jiji la Arusha ili
kushinikiza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA)
kuwasambazia maji.
Akizungumza
jana, Lema alisema ameamua kuandaa maandamano hayo ya kudai maji kwani
kwa zaidi ya miezi sita sasa asilimia 70 ya wakazi wa Jiji la Arusha
hawapati maji safi.
“Nimewaandikia
barua AUWSA wiki mbili sasa nikiwataka wanipe mipango yao ya muda
mfupi na mrefu ya kuondoa tatizo la maji Arusha, kwani mimi kama mbunge
ninaweza kushirikiana nao kupunguza tatizo hili, lakini hawajajibu
sasa tutawashinikiza kwa nguvu wa umma,” alisema Lema.
Hata
hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa AUWSA, Mhandisi Ruth Koya hakupatikana
kuelezea kama amepokea barua hiyo baada ya kutopatikana ofisini, pia
simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikani.
No comments:
Post a Comment