Mwandalizi mmoja wa mazishi
nchini Afrika Kusini, anayedaiwa kuwaagiza wafanyakazi wake kuikata miguu
ya maiti moja aliyodai kuwa ndefu sana alifikishwa mahakamani Ijumaa.
Ronel Mostert anayemiliki chumba cha kuhifadhi
maiti ambacho pia huendesha shughuli za mazishi, alitoa amri hiyo kwa
lengo la kuhakikisha kuwa maiti hiyo ingetosha katika jeneza. Anakabiliwa na kosa la kumkata miguu maiti.Mfanyakazi mmoja aliimbia mahakama kuwa Ronel alimuagiza kuchukua kifaa kimoja cha kukata ili kuikata miguu hiyo ya marehemu na kwamba jambo hilo limekuwa likimsumbua sana kimawazo.
Mwili marehemu ulifukuliwa ili kusaidia katika uchunguzi wa polisi.Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC