Serikali ya Jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo imeikashifu serikali ya Rwanda kwa kuwalinda
wapiganaji wanaotuhumiwa kwa kusababisha mauaji ya halaiki chini ya
nembo ya wapiganaji wa M23.
Afisa mmoja wa Serikali ya DRC ameiambia BBC
kuwa imekuwa vigumu kwa serikali yake kuwahoji zaidi ya wapiganaji 500
ambao wamekita kambi nchini Rwanda licha yao kutuma ombi la kufanya
hivyo yapata miezi saba iliyopita . Zaidi
ya watu 800,000 walitoroka makwao haswa mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemkrasia ya Congo wakati wa mapigano hayo ya wenyewe kwa wenyewe.Rwanda imekuwa ikipinga madai hayo na kusema kuwa imeshirikiana na serikali ya DRC. Kundi hilo la M23 lichukua silaha mashariki mwa DRC kuanzia Aprili 2012, liliaumu serikali ya Kinshasa kwa kuwabagua jamii ya watutsi na pia kupuuza makubaliano ya awali ya kusitisha mapigano. Kundi hilo hata hivyo lilishindwa katika mapigano yaliyoongozwa na jeshi la Umoja wa mataifa likisaidiwa na majeshi ya serikali ya Congo mnamo November 2013. Wapiganaji hao walitorokea Rwanda na Uganda.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Serikali ya Congo imetangaza kuwa itawapa msamaha wapiganaji hao. Tulipoingia ndani ya kambi hiyo ,hali na taswira ilikuwa tulivu na shwari. Kulikuwa na hema kubwa nyeupe, majengo kadha mbali na bustani iliyolindwa na nadhifu. Wapiganaji hao wanalala sita katika chumba kimoja .
Wanajipikia wenyewe hadharani na hawaruhusiwi kuondoka kambini ila wanapokwenda kupata matibabu. Japo taswira hiyo ni ya utulivu wapiganaji zaidi ya 100 wametoroka tangu kuzinduliwa miezi 15 iliyopita .
Afisa wa Serikali ya DR Congo Francois Muamba,amesema kuwa Rwanda kinyume na Uganda ,imekuwa ikijivuta sana katika swala kuu la kuwataka wale wanaotuhumiwa kwa mauaji ya halaiki na makosa mengine dhidi ya binadamu kufikishwa mahakamani .
Muamba ameilaumu serikali ya Kigali kwa kuwalinda makamanda wanne wa M23 wanaoshtumiwa kwa kuongoza mauaji ya halaiki nchini DR Congo. Anasema Rwanda imezuia mahojiano ya wapiganaji hao licha ya kutakiwa kuwawakilisha kwa vyombo vya usalama vya DRC. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC
No comments:
Post a Comment