Tuesday, September 10, 2013

"NAJUTA KUMJUA LORD EYEZ MAISHANI MWANGU".... RAY C


INAWEZEKANA umekuwa ukisikia vitu vingi kuhusu lejendari wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ lakini hukupata chansi ya kumsikia mwenyewe akifunguka mwanzo mwisho juu ya kisanga kilichompata alipojikuta kwenye janga la matumizi ya dawa za kulevya.

Ijumaa Wikienda limefanya naye mahojiano (exclusive interview) ambapo amekidhi kiu yako ya kujua chochote kinachomhusu. UNGANA NAYE…
KWA MTU ASIYEKUJUA, UMETOKEA WAPI?
“Nimezaliwa Mei 15, 1982 mkoani Iringa. Kabla ya kuingia kwenye muziki nilifanya kazi ya utangazaji. Watu wengi walinijua wakati nikiwa Radio Clouds FM. Albamu yangu ya kwanza ni Mapenzi Yangu niliyoitoa mwaka 2003. Kilichofuata ni kujipatia mashabiki wengi sana ndani na nje ya nchi. Baadaye niliachia Albamu ya pili ya Na Wewe Milele ya mwaka 2004. 

Nilipata mialiko mingi nje ya nchi zote Afrika Mashariki, China, Uingereza na kwingineko. Kilichofuata ni singo kibao na tuzo hadi nilipopata matatizo mwaka jana. Unazikumbuka Mama Ntilie, Mahaba ya Dhati, Touch Me, Na Wewe Milele, Wanifuatia Nini na Nihurumie? Huyo ndiye Ray C mwenyewe.

JALADA LA SUGU LATUA KWA DPP


JALADA la Kesi inayomkabili Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA), limefikishwa katika Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali. Mbilinyi maarufu kwa jina la ‘Sugu’(pichani), anadaiwa kumjeruhi askari wa Bunge katika vurugu zilizotokea Bungeni mwishoni mwa wiki iliyopita. Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Susan Kaganda alisema polisi wameshapeleka jalada la mbunge huyo katika Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali na kwamba upelelezi unaendelea.

“Tayari jalada la kesi yake lipo katika Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali na upelelezi unaendelea,” alisema.

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka Jeshi hilo, Sugu alikwenda Polisi kujisalimisha siku ya kuahirishwa Bunge na kwamba aliambiwa arudi tena kuripoti Jumatano (kesho). “Kama akiripoti Jumatano, ndiyo itajulikana na kama jalada lake litakuwa limeshafikishwa mahakamani au bado,” kilieleza chanzo hicho.

Habari za uhakika kutoka katika Mahakama ya Mkoa wa Dodoma hadi jana mchana, hakukuwa na jalada lolote lililokuwa limefika mahakamani linalomuhusu Sugu. “Kwa leo (jana), majalada yaliyopokelewa hadi sasa ni mawili tu na yote yanahusu ‘Trafiki kesi’ kilieleza chanzo hicho.


Kusakwa kwa mbunge huyo kulitokana na vurugu zilizotokea katika ukumbi wa Bunge ambao uligeuka ulingo wa masumbwi, baada ya wabunge wa kambi ya upinzani kupigana hadharani na askari wa Bunge.

Wabunge hao walichapana ndani na nje ya ukumbi, hali iliyosababisha tafrani kubwa, huku maofisa usalama na askari polisi kutoka kituo kikuu mjini Dodoma, wakilazimika kuitwa kwenda kuongeza nguvu ili kukabiliana na hali hiyo.

WEMA SEPETU AWATOA MATE MANJEMBA KWA USTADI WA KUKATA KIUNO...!!!

MADAM, Wema Sepetu ameonesha upande wa pili wa maisha yake baada ya kunaswa akikata mauno mwanzo mwisho.  
Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa Kibongo, Madam alifi ka na kampani yake katika Ukumbi wa Thai Village, Masaki jijini Dar hivi karibuni na ndipo ‘mashetani’ yalipompanda baada ya kusikia sebene lililokuwa likiporomoshwa na Bendi ya Skylight.
Wema akiwa na kampani yake wakionekana kukolea kwa kilevi, waliinuka na kuanza kushindana kucheza huku Wema akijiweka ziro distance na mmoja wa wanamuziki wa bendi hiyo na kuanza kumkatikia.

NDUNGAI ATAJA SABABU ZAKE ZILIZOFANYWA AMTIMUE FREEMAN MBOWE BUNGENI


NAIBU Spika, Job Ndugai ametetea uamuzi wake wa kuagiza kutolewa ndani ya ukumbi wa Bunge, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akisema alikuwa sahihi.

Mabishano hayo ambayo yalisababisha kuibuka kwa vurugu bungeni yalitokea mwishoni mwa wiki, muda mfupi baada ya kipindi cha maswali na majibu, ambapo kiongozi huyo wa Bunge aliruhusu mjadala kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba uendelee.

Kutokana na hali hiyo, Mbowe alisimama kutaka kutoa ufafanuzi juu ya mjadala huo, lakini Ndugai alimzima na kumtaka kukaa chini, jambo ambalo halikumfurahisha Mbowe na kumfanya agomee agizo lake.

Akizungumza na MTANZANIA jana kwa njia ya simu, Ndugai alitumia muda mwingi kutetea uamuzi wake na kukosoa hoja za watu wanaompinga juu ya uamuzi wake huo.

SERIKALI YAKUSUDIA KUANZISHA MTIHANI WA TAIFA WA DARASA LA PILI...!!!



Mtihani mpya wa Taifa utaanzishwa kwa wanafunzi wa darasa la pili nchi nzima, ili kuchuja watakaoshindwa kusoma, kuandika na kuhesabu.

Akifafanua uamuzi wa kuanzishwa mtihani wa Taifa wa darasa la pili, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema mtihani huo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa matokeo makubwa sasa katika sekta ya elimu.

Malengo ya mtihani huo kwa mujibu wa Mulugo ni kuondoa uwezekano wa kuwa na wanafunzi katika madarasa ya juu, wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu na ili kufikia malengo hayo, watakaoshindwa 
mtihani huo, watarudia mpaka wajue kusoma na kuandika.

ANGALIA PICHA ZA MSANII RECHO AKIWA KWENYE TAMASHA LA FIESTA Duuuuh!!! NOMA SANA

VILIO VYATAWALA MSIBA WA MSANII WA FILAMU

 Mama mzazi wa Malisa akiwa na uso wa huzuni.
  Dada wa marehemu (wa tatu kushoto) akilia kwa uchungu baada ya msanii wa filamu, Chuchu Hansi (aliyeinamisha kichwa) kuingia na kuangua kilio.
   Wasanii wakongwe wa filamu, Devotha Mbaga na Vanitha wakilia kwa uchungu.
Waombolezaji wakiwa na nyuso za huzuni.
VILIO vimetanda msibani kwa msanii wa filamu za Kibongo, Zuhura Maftah ‘Malisa’ aliyefariki dunia jana akiwa hospitali ya Hindu  Manndal alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na maumivu makali ya kichwa.

Msiba wa msanii huyo upo nyumbani kwa dada yake Mikocheni na mazishi yatafanyika kesho makaburi ya Kinondoni.(Habari/Picha: Gladness Mallya na Hamida Hassan / GPL)

MAGAZETI YA LEO JUMANNE SEPTEMBA 10, 2013

DSC 0001 9c2fe
DSC 0002 bd55a

SERIKALI YAMPONGEZA MZEE GURUMO

11_fb546.jpg
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Bibi. Lilly Beleko kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akimkabidhi Mzee Muhidini Gurumo barua kama ishara ya Serikali kutambua mchango wake uliotukuka katika tasnia ya Muziki nchini pamoja na kumpongeza kwa kustaafu kazi kazi hiyo, hivi karibuni nyumbani kwake Makuburi, Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia nyuma ya Mkurugenzi ni Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania, Bw. Addo Mwasongwe na kulia pembeni ya Mzee Gurumo ni Mkewe, Bibi. Pili Said Kitwana.
22_c71f0.jpg
Nguli wa Muziki wa Dansi, Mzee Muhudini Gurumo (aliyevaa shati la drafti) akiwa na watumishi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, walipomtembelea nyumbani kwake Makuburi Jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Serikali kupitia Wizara hiyo ilimkabidhi barua rasmi Mzee huyo kutambua mchango wake katika tasnia ya Muziki na kumpongeza kwa kustaafu kazi hiyo. 
Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Bibi Lilly Beleko, wa pili ni mke wa Mzee Gurumo, Bibi. Pili Said Kitwana na wa Pili Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Wizara Upande wa Sanaa, Bibi. Joyce Hagu.
Picha zote na Concilia Niyibitanga


Monday, September 09, 2013

"WAHAMIAJI WALIOOLEWA RUKSA KUISHI NA WENZA WAO"

masawe_fa939.png
Serikali imesema wahamiaji haramu walioolewa na Watanzania wanaruhusiwa kubaki nchini, hawalazimiki kuvunja ndoa zao ingawa wanatakiwa kupata kibali maalumu kutoka Idara ya Uhamiaji.
Akizungumza mjini hapa jana, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, alisema wahamiaji haramu walioolewa wanatakiwa kwenda Idara ya Uhamiaji kupata hati hizo.
Pia, alisema kwa mujibu wa sheria, mhusika atapewa kibali alichokiita 'Independence Pass' kitakachomwezesha kuendelea kuishi nchini na kwamba, kinyume chake itakuwa ni kuvunja haki za binadamu.
Hata hivyo, Massawe alibainisha kuwa lazima zoezi la kuondoa wahamiaji haramu lifanyike, kwani walioondoka kwa hiari ni 11,601 na waliokadiriwa kuondoka ni kati ya 52,000 na 53,000, hivyo idadi kubwa bado wanaishi nchini.
Akizungumzia zoezi la kurudisha wahamiaji haramu lililoanza rasmi Septemba 6, mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma, Mkuu Msaidizi wa Operesheni hiyo, Simon Sirro, alisema tayari wamewakamata 1,851.
Pia, Sirro alisema ng'ombe 1,765, sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na bunduki saba vimekamatwa na kwamba, wahamiaji wanaokamatwa wanarudishwa kwa mujibu wa sheria kwa kuzingatia haki za binadamu.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 09, 2013

DSC 0017 9af83
DSC 0018 d7f1e

SERENA WILLIAMS AMCHAPA VICTORIA AZARENKA 7-5, 6-7 (6-8) 6-1 KATIKA FAINALI YA US OPEN

Serena Williams: Defended her US Open crown after beating Victoria AzarenkaSerena Williams amefanikiwa kulinda Heshima na Ubingwa wake Wa US OPEN mara baada ya Kumshinda mpinzani wake Victoria Azarenka Kwa Miaka Miwili MfululizoAzarenka is in tears after losing to Williams for the second year in succession

"WENGI MASIKINI KWA SABABU HAWATUMII FURSA ZILIZOPO" MENGI

Mwenyekiti Wa Makampuni ya IPP Reginald Mengi


MWENYEKITI wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi amesema Watanzania wengi wanazidi kuwa masikini kwa sababu hawazitumii fursa za utajiri uliopo nchini, hivyo kutaka vijana kuona kwa macho fursa hizo ili waweze kujikwamua kutoka kwenye dimbwi hilo la umasikini.

Akizungumza wakati wa kutoa zawadi kwa washindi watatu wa shindano la nini kifanyike kuzalisha ajira nyingi hapa nchini aliloanzisha Mwenyekiti huyo wa IPP, Mengi alisema baada ya Watanzania kupofushwa kuwa nchi yao ni masikini, wengi walibweteka na kushindwa kuchangamkia fursa zilizopo hali ambayo imeifikisha nchi hapa ilipo.

Alisema jambo la msingi kwa vijana wa Tanzania ni kuibua mawazo ya shughuli gani atafanya badala ya kukimbilia namna ya kupata mitaji, kwani wengi ambao wamekimbilia kutafuta mitaji wamejikuta wanaipata mitaji hiyo, lakini wakashindwa namna ya kuitumia.

Washindi katika shindano hilo ambalo limeanzishwa na Mengi lijulikanalo kama Tweet Bora ni Lilian Wilson wa Chuo Kikuu cha Ardhi aliyepata Sh milioni moja, Susan Senga ambaye ni mfanyabiashara ndogo alipata Sh 500,000 na Ombeni Kaaya ambaye ni mjasiriamali kutoka Nzega, Tabora aliyekabidhiwa Sh 300,000.

UNYAMA WA KUSIKITISHA....!!! MKE AZALIA CHOONI NA KUUA KICHANGA...!!!

KWELI dunia inakwenda ukingoni, mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu, amefanya kitendo cha kinyama baada ya kujifungua msalani na kukiua kichanga chake.


Tukio hilo limetokea hivi karibuni maeneo ya Mazizini, Ukonga Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam baada ya mwanamke huyo ambaye jina lake halikupatikana kukitumbukiza kichanga hicho chooni.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mwanamke huyo ni mkazi wa Ukonga Moshi Bar alidaiwa kunywa dawa kwa ajili ya kuutoa ujauzito aliokuwa nao wa miezi minane  na baada ya kuona hali imebadilika alitoka nyumbani kwake Moshi Bar na kukimbilia Ukonga Mazizini kwa ajili ya kutaka msaada kwa mama yake mdogo.

JK AONJA NGUVU YA CHADEMA MWANZA ISHARA YA VIDOLE VIWILI, PEOPLES POWER YATAWALA

RAIS Jakaya Kikwete jana alipata wakati mgumu, baada ya kukutana na nguvu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jijini Mwanza katika ziara yake, huku Waziri wake wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, naye akijikuta akizomewa mbele yake.

Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje, alivunja mwiko baada ya kujiunga katika msafara huo wa raia akiwa na gari lenye alama za Movement for Change (M4C) lililokuwa limefungwa bendera mbili za CHADEMA.

Hata hivyo maofisa usalama walipata wakati mgumu kulizuia gari hilo lisiwepo katika msafara huo, jambo lililozua tafrani kidogo katika uwanja wa Furahisha ambapo Kikwete alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara.

Awali wakati wa uzinduzi wa wodi ya wazazi iliyoko eneo la Butimba, Rais alilazimika kumpa Wenje nafasi ya kuwasalimia wananchi baada ya Mkuu wa Mkoa, Evarist Ndikilo, kutaka kufanya hila ya kumnyima haki hiyo kama mbunge wa jimbo husika.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...