Barcelona
walitawazwa mabingwa wa Ulaya kwa mara ya tano baada ya kuichapa
Juventus mabao matatu kwa moja katika mechi kali ya fainali iliochezwa
katika uwanja wa Olimpiki wa Berlin.
Barcelona walikuwa wa kwanza kufunga kupitia Ivan Rakitic kunako dakika ya nne ya mwanzo wa kipindi cha kwanza.
Hata hivyo Alvaro Morata
alisawazisha .Lakini Luis Suarez alifunga bao jingine baada ya kipa
Gianluigi Buffon kuutema mpira naye nyota Neymar akafunga udhia baada ya
gusa ni guse kati yake na Messy.
Katika mechi hiyo Andre Iniesta ndiye aliyetangazwa mchezaji bora.Hii inamaanisha kwamba Barcelona wameshinda mataji matatu ikiwemo lile la Copa Del Rey,La liga na la vilabu bingwa barani Ulaya.
Mechi
hiyo pia ilikuwa ya mwisho kwa kiungo wa wakati wa Barcelona Xavi
Hernandez ambaye anaondoka kilabu hiyo baada ya kuichezea kwa mda mrefu. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment