Serikali imesema wahamiaji haramu walioolewa na Watanzania wanaruhusiwa kubaki nchini, hawalazimiki kuvunja ndoa zao ingawa wanatakiwa kupata kibali maalumu kutoka Idara ya Uhamiaji.
Akizungumza mjini hapa jana, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, alisema wahamiaji haramu walioolewa wanatakiwa kwenda Idara ya Uhamiaji kupata hati hizo.
Pia, alisema kwa mujibu wa sheria,
mhusika atapewa kibali alichokiita 'Independence Pass' kitakachomwezesha
kuendelea kuishi nchini na kwamba, kinyume chake itakuwa ni kuvunja
haki za binadamu.
Hata hivyo, Massawe alibainisha kuwa
lazima zoezi la kuondoa wahamiaji haramu lifanyike, kwani walioondoka
kwa hiari ni 11,601 na waliokadiriwa kuondoka ni kati ya 52,000 na
53,000, hivyo idadi kubwa bado wanaishi nchini.
Akizungumzia zoezi la kurudisha
wahamiaji haramu lililoanza rasmi Septemba 6, mikoa ya Kagera, Geita na
Kigoma, Mkuu Msaidizi wa Operesheni hiyo, Simon Sirro, alisema tayari
wamewakamata 1,851.
Pia, Sirro alisema ng'ombe 1,765, sare
za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na bunduki saba vimekamatwa na
kwamba, wahamiaji wanaokamatwa wanarudishwa kwa mujibu wa sheria kwa
kuzingatia haki za binadamu.
No comments:
Post a Comment