Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga
SIKU sita tangu ajali ya basi dogo aina ya Toyota Hiace kuua watu 19
mkoani Mbeya, nchi imeendelea kukumbwa na ajali za barabarani. Safari
hii watu kumi wamekatishwa uhai, kutokana na ajali ya basi na lori,
iliyotokea mkoani Shinyanga jana.
Katika ajali hiyo, watu tisa walikufa papo hapo na mmoja aliaga dunia
akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga. Abiria 51
walijeruhiwa na wanatibiwa hospitali hapo, wakati tisa, akiwemo dereva
wa basi, wako katika hali mbaya.
Ajali hiyo ilitokea katika kijiji cha Ibingo Kata ya Samuye wilayani
Shinyanga Vijijini na ilithibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Shinyanga, Justus Kamugisha.
Alisema ajali ilitokea majira ya saa 9:30 alasiri baada ya basi la
kampuni ya Unique, lililokuwa linatoka Mwanza kwenda Tabora kugongana na
lori la kampuni ya Coca Cola, lililokuwa linatoka Kahama. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.