Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, John Mnyika
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kuwa adui yake
namba moja ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha Alliance for Change and
Transparance (ACT-wazalendo), Zitto Kabwe.
Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, John Mnyika akihutubia mkutano wa
hadhara uliofanyika Uwanja wa Furahisha Mwanza juzi, alisema Chadema
haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo ndani ya Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) kutokana na kile alichosema ‘ni adui kwao’.
“Mtume Muhamad (S.A.W) alikuwa anazungumzia unafiki ambao una sura mbili
na sifa zake, leo (ACT) wanasema wapo upinzani, wanasema msiunge mkono
Ukawa halafu mnawakaribisha?
“Nendeni kila mahali waambieni wananchi adui yetu mkuu ni Zitto.
Sikilizeni niwaambie Taifa hili kama ni ufisadi tumeshazungumzia sana
kuanzia EPA mpaka Richmond. Dk. Slaa (Willbrod) alipoingia bungeni
aliyasema haya kwa sasa si mapya. Adui yetu ni Zitto na hatumtaki
Ukawa,” alisema Mnyika.
Alisema Chadema haiko tayari kuikaribisha ACT-Wazalendo Ukawa kwa sababu adui kwao. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Zitto ajibu
Akihutubia mamia ya wananchi wa Mwanza jana, Zitto alisema kadri siku zinavyosonga wabaya wake wamekuwa wakijionyesha.
Zitto alisema pamoja na hali hiyo, ACT-Wazalendo haiko tayari
kuzungumzia siasa za wakati uliopita kwa vile kufanya hivyo si afya
njema kwa siasa za upinzani.
Alisema ni vema viongozi wa vyama vya upinzani waachane na ugomvi binafsi na watangulize masilahi ya taifa mbele.
“Mwanzo walipotufukuza walituambia tukatafute vyama vingine hilo
likafanyika, tulipopata vyama vya kufanyia siasa wakasema vipo kwa ajili
ya kugawa upinzani tukasema tupo tayari kuunganisha nguvu ya pamoja kwa
ajili ya kuiondoa CCM…wenzetu pia hili hawalitaki sasa ni wajibu wenu
kutambua watu gani hawataki kuiondoa CCM,” alisema Zitto.
Alisema wao (ACT) wana nia ya dhati lakini wenzao wanaweka ugomvi binafsi mbele ya masilahi ya taifa.
“Sisi ACT Wazalendo bado tupo tayari kushirikiana kwa mujibu wa misingi.
Shabaha yetu ni moja tu, kubomoa mfumo wa uchumi wa kinyonyaji na
ufisadi ili kujenga uchumi shirikishi wa wananchi,” alisema na kuongeza:
“Sikufundishwa kugombana na watu barabarani au kusema ovyo mitaani,
kufanya hivi hakuna tofauti na kumsema mke au mume mlioachana…mmoja kwa
kukosa busara na kwa kuwa aliachana na yule mke anaamua kwenda vijiweni
na kutoa siri za mzazi mwenzie, hili kwetu hapana.
“Tunakuja na jahazi jipya ambalo ndugu zangu wa Mwanza nimekuja
kuwakabidhi, kubwa tunataka kulirudisha taifa katika misingi yake ya
ujamaa na kujitegemea, tunahitaji ujamaa wa demokrasia,” alisema Zitto.
Alisema tafsiri ya ujamaa haina maana kuwa chama hicho kitataifisha mali
za watu, bali kitarekebisha makosa ya ubinafsishaji kwa kurejesha mali
zote za taifa zilizouzwa na wanunuzi hawajatekeleza mikataba yao.
Mapokezi
Zitto ambaye amefuatana na Mwenyekiti wa chama hicho, Anna Mghwira,
waliwasili Mwanza saa 8.00 mchana na kupata mapokezi makubwa yaliyoanzia
wilayani Misungwi.
Mapokezi hayo yaliongozwa na vijana waendesha pikipiki (bodaboda) na
kikundi cha wanawake ambao muda wote walikuwa katika shamrashara hadi
alipoingia kwenye uwanja wa Furahisha. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na Mtanzania
No comments:
Post a Comment