Rais wa China Xi Jinping ameanza ziara ya siku mbili nchini Pakistan hii leo.
Bwana
Xi atazindua mpango wa uwekezaji wa kichina wa gharama ya dola bilioni
50 ambao Pakistan ina matumaini kuwa utasuluhisha tatizo lake ya
nishati.
Mpango huo unaofahamika kama barabara ya uchumi ya China
na Pakistan ni pamoja na barabara , reli na mabomba ya jumla ya umbali
wa kilomita 3000 kutoka mji wa bandari wa Gwadar nchini Pakistan hadi
mji wa ulio mashariki mwa China wa Kashgar.
Waandishi wa habari
wanasema kuwa lengo la China ni kuongeza ushawishi wake wa kiuchumi kwa
Pakistan ili kulegeza ule wa Marekani na India. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment