Waziri
mkuu wa Italia Matteo Renzi ametoa wito wa kufanyika kikao cha dharura
cha viongozi wa umoja wa ulaya kujadili swala la wahamiaji wanaoangamia
kwenye bahari ya Meditarenean wakijaribu kuingia ulaya. Inafuatia ajali
ya hivi punde ambao karibu watu 700 wanahofiwa kufa maji baada ya boti
kuzama baharini kaskazini mwa Libya, kilomita 200 kutoka kisiwa cha
Lampedusa, nchini Italia.
Manusura 28 wa janga la hivi punde
kwenye bahari ya Meditaranean walitarajiwa kufikishwa kisiwani Sicily
alfajiri ya Jumatatu. Hadi kufikia usiku, ni miili 24 iliyokuwa
imeopolewa, na maafisa wa usalama kwenye pwani ya Italia, wakaipeleka
kisiwani Malta.
Ni vigumu kuhakikisha idadi ya watu walioanza
safari kwenye boti hiyo kutoka pwani ya Libya. Lakini walionusurika
wanasema walikuwa kati ya watu 500 na 700 kabla ya kupinduka kilomita
mia mbili kutoka Lampedusa, kwenye maji ya Libya. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Ikiwa idadi hiyo
itathibitishwa basi hii itakuwa ndio ajali mbaya zaidi kati ya nyingi
ambazo zimekuwa zikitokea karibuni kwenye bahari ya mediteranean, huku
watu wakifanya safari za hatari kutafuta maisha bora ulaya.
Waziri
mkuu wa Italia Matteo Renzi amesema zaidi ya mawakala 900 wa
kusafirisha watu wamekamatwa. Alisema suluhu la tatizo la wahamiaji si
kutafuta manusura baharini, bali kuwakabili mawakala hao wa kusafirisha
watu, akiwaita wafanyabiashara wa watumwa wa leo. Ametaka kikao cha
umoja wa ulaya ndani ya wiki moja kujadili tatizo hili kubwa.
Papa
Francis kwenye misa ya Jumapili alitoa wito kwa jamii ya kimataifa
kuchukua hatua ya haraka kuepuka janga lingine kama hilo.
Meli
pamoja na helikopta za Italia na Malta ziliendelea na shughuli ya kusaka
miili usiku kucha. Mamlaka za Sicily zinasema wengi wa abiria kwenye
boti iliyozama walikuwa ni kutoka mataifa ya Algeria, Misri Somalia,
Senegal na hata Zambia. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Na BBC Swahili
No comments:
Post a Comment