Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nch, Isaac Nantanga.
WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakati wowote wiki hii itaanza
kutoa orodha ya vyama vya kijamii vitakavyofutwa kwa kuanzia na mkoa wa
Dar es Salaam.
Imesema vyama hivyo vitafutwa kutokana na kutotekeleza matakwa ya
kisheria ya kuwasilisha taarifa za mwaka za ukaguzi wa hesabu za vyama
na vile ambavyo havilipi ada ya mwaka kama sheria inavyoelekeza.
Msemaji wa wizara hiyo, Isaac Nantanga alisema hayo jana katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari kufafanua suala la uhakiki wa vyama
vya kijamii nchini.
Alisema vyama vitakavyobainika vitafutwa katika Daftari la msajili wa
vyama vya kijamii na wala siyo Taasisi zisizo za kiserikali (NGO,s)
kwani haihusiki nazo.
“Orodha ya vyama vitakavyofutwa itaanza kutolewa kwa awamu kuanzia
wiki hii na kwa kuanzia orodha hiyo itahusu vyama vilivyosajiliwa mkoa
wa Dar es Salaam”Alisema
Alisema kufuatana na orodha iliyopo vyama
10,000 vya kijamii na Taasisi za Dini vimesajiliwa na wizara hiyo na
vitakavyofutwa ni vile tu ambavyo haviwasilishi taarifa za kila mwaka za
ukaguzi wa hesabu zao na pia kama havilipi ada ya kila mwaka kama
sheria inavyotaka.
Juzi, gazeti moja la kila siku liliandika kuwa Waziri wa Mambo ya
Ndani Mathias Chikawe anaanza kuhakiki NGOs jambo ambalo siyo la kweli
kinachofanyika ni kwa taasisi za kijamii. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment