Shirika
la kimataifa la msalaba mwekundu limesema kuwa hali inazidi kuwa mbaya
nchini Yemen, huku Mji mkuu Sanaa ukikosa umeme na maji kwa kipindi cha
siku tisa zilizopita.
Afisa wa ngazi ya juu wa Shirika hilo nchini
humo Robert Mardini amesema ameshuhudia miili kadhaa kwenye mitaa
alipotembelea mji wa Aden, na kueleza kuwa changamoto iliyopo ni
upelekaji wa huduma za kitabibu.
Awali Saudi Arabia ilisema
itaendelea kutumia jeshi kuzuia waasi wa kihudhi kudhibiti Yemen, waasi
nao wametaka kumalizwa kwa mashambulizi ya anga dhidi yao na kuanza
mazungumzo.
Mpiganaji anayemuunga mkono Rais Abdrabbuh Mansour
Hadi amesema ni mapema mno kuanza kuzungumzia makubaliano kati ya pande
mbili. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment