Sunday, October 12, 2014

POSHO ZA BUNGE ZAIBUA MAPYA


Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta. PICHA|MAKTABA

Siku chache baada ya Bunge la Maalumu la Katiba kumaliza muda wake, matumizi ya fedha zilizobaki kwenye Bunge hilo yameibua mvutano baada ya kuwapo taarifa kuwa fedha hizo ziliisha, huku Wizara ya Fedha ikieleza kuwa bado zipo.
Idadi ya wajumbe wa Bunge hilo kisheria ni 629 na wajumbe ambao hawakuhudhuria vikao vya Bunge hilo tangu Aprili 16, mwaka huu, wanakadiriwa kufikia 140.
Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta, aliwahi kukaririwa akiwaeleza wajumbe wa Bunge hilo kuwa fedha zitakazookolewa zitatafutiwa utaratibu badala ya kurudishwa zilikotoka.
Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Katibu wa Bunge, Yahaya Khamis Hamad, alisema hakuna pesa zilizobaki na kwamba waliomba Serikali kuwaongezea fedha za siku nne zilizobakia kabla ya kukabidhi Katiba inayopendekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete Jumatano wiki hii. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 12, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MABINGWA WA DUNIA UJERUMANI ‘ YACHAPWA’ KWA MARA YA KWANZA NA POLAND

Poland imeifunga UJerumani kwa mara ya kwanza na kukwea juu ya kilele katika kundi la Nne kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za Ulaya, Euro, 2016 nchini Ufaransa. Mabingwa wa dunia , Ujerumani ilikuwa na rekodi ya kucheza mara 18 mfululizo bila kupoteza mchezo wowote dhidi ya majirani zao, Poland ambao walipata mabao yote mawili katika kipindi cha pili.
Mshambulizi kinda wa klabu ya Ajax Amsterdam, Arkadiusz Milik, 20 alifunga bao la kuongoza katika dakika ya 51, na dakika mbili kabla ya kumalizika kwa mchezo, Sebastian Mila aliwahakikishia wenyeji ushindi baada ya kufunga bao la pili katika mchezo huo uliopigwa jijini, Warsaw.
Mabingwa hao wa sasa wa dunia, walifungwa mara ya mwisho na Jamhuri ya Czech, Oktoba, 2007 katika michezo ya kufuzu. Ujerumani ilicheza michezo 33 ya kufuzu pasipo kupoteza. Kipa wa Ujerumani, Manuer Neur aliokoa mabao manne ya wazi katika mchezo ambao walishambuliwa sana. Poland iliyokuwa na mshambulizi wa Bayern Munich, Robert Lewandowski ilipiga jumla ya mashuti 19, huku mashuti 12 yakilenga bao.
Kocha wa Ujerumani, Joachim Loew alikwenda Poland huku baaddi ya wachezaji wake muhimu wakikosekana. Ujerumani ilibanwa hasa na walimudu kufanya mashambulizi machache . Walipiga mashuti saba tu ambayo yote yalilenga lango lakini nyota wa mchezo huo, golikipa, Wojciech Szczesny alikuwa imara, kipa huyo wa klabu ya Arsenal aliokoa mara 14. Tomas Mueller, Andre Schurrle na Mario Gotze walishindwa kufunga kwa muda wote waliokuwa uwanjani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

UFARANSA YAICHAPA URENO NA C.RONALDO AKIWEMO

Mshambulizi Karimu Benzema alifunga bao la mapema na akatengeneza lingine kwa kiungo Paul Pogba katika kipindi cha pili na kuisaidia Ufaransa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ureno. RicaRrdo Quaresma alitokea benchi katika kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Luis Nani katika dakika ya 68, alifunga kwa mkwaju wa penalti dakika tisa baada ya kuingia uwanjamni .
Ufaransa ambao ndiyo wenyeji wa fainali zijazo za Ulaya waliifunga Ureno ambayo ilikuwa na mshambulizi wake mahiri na mchezaji bora wa dunia, Cristiano Ronaldo katika mchezo uliofanyika jijini Paris. Ronaldo alipiga mashuti manne katika mchezo huo lakini ni shuti moja tu ambalo lilikuwa na uhai. Timu zote zilicheza mchezo wa kufanana, Ufaransa walipiga mashuti 12 sawa na waliyopiga Ureno, lakini wageni walifanikiwa kupiga mashuti mawili tu ambayo yalimsumbua golikipa, Steven Mandanda.
Eliaguim Mangala, RAfaer Varane, Patrice Evra na Bacary SAgna walianza katika safu ya ulinzi na wanne hao hawakuwekwa majaribuni na kikosi kilichopoteza makali cha Ureno. Ronaldo alitoka uwanjani dakika ya 76 akimpisha Jose Mario alianza sambamba Danny na Nani katika safu ya mbele lakini watatu hao hawakuwa tishio kwa Ufaransa ambao walicheza jumla ya faulo 15 katika mchezo huo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

SITI MTEMVU NDIYE REDD'S MISS TANZANIA 2014

Miss Tanzania 2014, Siti Abass Zuberi Mtemvu akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia leo katika shindano lililoshirikisha warembo 30 na kufanyika ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam. Siti Mtemvu ametwaa taji hilo lililokuwa likishikiliwa na Happyness Watimanywa.

Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2014,Sitti Abbas Mtemvu akiwa katika picha ya pamoja na Mshindi wa pili,Lillian Kamazima (kulia) na Mshindi wa Tatu,Jihhan Dimachk mara baada ya kutawazwa rasmi usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam.Sitti Mtemvu alianza kwa kunyakua Redds Miss Chang'ombe na baadaye Redds Miss Temeke. Sitti ni binti wa Mbunge wa Temeke, Mhe. Abbas Mtemvu.

Redd's Miss Tanzania aliemaliza muda wake, Happiness Watimanywa akimpisha crown, Redd's Miss Tanzania wa sasa, Sitti Mtemvu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz




Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

BOKO HARAM LAWAACHIA MATEKA 27

boko haram
Rais wa Cameroon amesema kuwa mateka 27 wakiwemo raia 10 wa Uchina wameachiliwa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram.
Raia hao wa China walitekwa nyara mwezi mei wakati kampuni moja ya China ilipovamiwa karibu na mpaka wa Nigeria.
Wengine walioachiliwa ni pamoja na mke wa naibu waziri mkuu nchini Cameroon aliyetekwa nyara mwezi Julai.
Haijulikani iwapo fidia ililipwa.
Boko haramu wameeneza mashambulizi kutoka nchini Nigeria kwenda kaskazini magharibi mwa Cameroon. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Saturday, October 11, 2014

UTAFITI: VIAGRA HUSABABISHA UPOFU

Kipofu
Watafiti nchini Australia wanadai kwamba dawa inayotumiwa kuongeza nguvu za kiume VIAGRA husababisha upofu baada ya mda mrefu.
Kulingana na Watafiti hao kutoka Australia, kiungo fulani katika dawa hiyo inayotumiwa kukabiliana na ukosefu wa nguvu za kiume,huathiri uwezo wa kuona miongoni mwa wanaume ambao wana ugonjwa wa macho.
Kulingana na gazeti la Nation nchini kenya,Madaktari nchini Australia wamebaini kwamba kiungo fulani katika dawa hiyo kinaweza kusababisha upofu miongoni mwa wanaume wenye tatizo la ugonjwa wa macho.
Vilevile inadaiwa kuwa dawa hiyo pia inaweza kuwaathiri watumiaji ambao wanaona vizuri.
Utafiti huo uliofanywa katika panya,ulibaini kwamba hata watu wasio na ugonjwa wa macho wanaweza kuathirika. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

WENJE ABADILI UPEPO MKUTANO WA RAIS KIKWETE

 

Rais Jakaya Kikwete (katikati) akipita kwenye daraja la waenda kwa miguu la Mabatini, Mwanza jana, baada ya kulizindua, daraja hilo limeghalimu kiasi cha sh8bilioni litasaidia kuondoa tatizo la ajali zilizokuwa zikitokea mara kwa mara eneo hilo. kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dk. John Magufuli.


Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje jana amebadilisha upepo kwenye mkutano wa Rais Jakaya Kikwete, kwa kueleza kuwa miradi yote ya Serikali ni fedha za wananchi.

Wenje alisema hayo alipopewa nafasi ya kuzungumza kwenye viwanja vya Mabatini mkoani hapa, akidai kuwa miradi yote inayotekelezwa na Serikali ni kodi za wananchi wala siyo fedha za CCM.

Wenje alitoa kauli hiyo mbele ya Rais Kikwete baada ya Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli kudai kuwa CCM ndiyo inayotekeleza miradi yote ya maendeleo kupitia ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2010.

Rais Kikwete alikuwa akizindua daraja ya Mabatini lililojengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh1 bilioni na Kampuni ya Adivance Life.

Kabla hajazungumza Wenje alipopanda jukwaani hapo, mamia ya watu waliohudhuria uzinduzi wa daraja hilo walianza kupiga kelele huku wakishangilia kwa kuonyesha ishara ya vidole viwili juu na kuimba ‘Peoples Power’. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAOFISA POLISI 120 WATIMULIWA CCP

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu  

Moshi. Maofisa wa Polisi wapatao 120 wa Jeshi la Polisi, waliokuwa wakihudhuria mafunzo ya kupandishwa vyeo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi (MPA), wametimuliwa chuoni hapo.
Habari za uhakika zilizopatikana jana kutoka ndani ya chuo hicho zamani kikijulikana kama CCP, zimedai uamuzi wa kuwaondoa chuoni ulitangazwa jana na mkuu wa chuo hicho, Matanga Mbushi.
Vyanzo mbalimbali vililidokeza gazeti hili kuwa, waliotimuliwa chuoni hapo ni maofisa ambao wana ulemavu wa aina mbalimbali walioupata wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kazi.
Habari hizo zilisema hadi jana saa 9:00 alasiri, maofisa hao walikuwa ofisi za mkuu wa chuo hicho wakisubiri kupatiwa maelekezo ya namna ya kurejea katika vituo vyao vya kazi mikoa mbalimbali. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI OKTOBA 11, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.

.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Friday, October 10, 2014

MAMBO HAYA: MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI AMTUNDIKA MIMBA MWALIMU WAKE....!!!


Hii ni moja ya picha mbalimbali za wajawazito kama inavyonekani siyo ya mwalimu muhusika kwa tukio hilo.

WAKATI ikiwa imezoeleka kuwa baadhi ya walimu wa kiume huwarubuni wanafunzi wao wa kike na hata kuwaharibia kabisa ndoto zao za kielimu kutokana na kuwapa ujauzito, hali imekuwa tofauti mkoani Rukwa ambako mwanafunzi wa Kidato cha Pili anadaiwa kumzalisha mwalimu wake.

Mwanafunzi huyo aliyemzalisha mwalimu wake ana umri wa miaka 17, wakati mwalimu huyo anayefundisha katika Shule ya Sekondari ya Umma ya Nkasi, iliyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, Rukwa, ana umri wa miaka 25.

Tukio hilo linalotajwa kuwa la kwanza kutokea wilayani hapa, limekuwa gumzo kubwa kwa wakazi wa Nkasi na wilaya jirani.

Hata hivyo, kwa wanafunzi, wamekuwa wakimpongeza mwenzao kwa kujaliwa kupata mtoto katika umri wake huo mdogo, huku mzazi mwenzake akiwa na uhakika wa maisha kutokana na kuwa ni mtumishi serikalini. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

NEC: HAKUNA KURA YA MAONI BILA DAFTARI JIPYA




Rais Jakaya Kikwete akipokea Katiba Inayopendekezwa kutoka kwa Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta wakati wa hafla iliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma juzi. Katikati ni Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein. 


Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema haitaendesha uchaguzi wa aina yoyote, wala kuitisha kura ya maoni hadi kazi ya kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura itakapokamilika.

Kauli ya NEC imekuja siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kukabidhiwa Katiba inayopendekezwa na Mwenyekiti wa lililokuwa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta na kulitaja suala la uboreshaji wa daftari la hilo kama mambo matatu yanayoiweka kura ya maoni kupitisha Katiba hiyo njiapanda.

Mambo mengine ni Sheria inayotaka kura hiyo ipigwe ndani ya siku 84 baada ya Katiba inayopendekezwa kuchapishwa na kufanyiwa marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema jana kwamba kuendesha uchaguzi bila kuboresha daftari hilo ni kuongeza malalamiko kwa wananchi na wadau, hususan vyama vya siasa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WASHUKIWA 7 WA UCHAWI WAUAWA KIGOMA



Moja ya nyumba zilizoteketezwa katika Kijiji cha Murufiti ambapo watu saba waliuawa kwa kuchomwa moto.

Kigoma. Watu saba wameuawa kwa kuchomwa moto ndani ya nyumba katika tukio ambalo nyumba 18 ziliteketezwa na mbili kubomolewa na wananchi waliodai wanawaua wachawi katika Kijiji cha Murufiti, Kasulu, mkoani Kigoma.
Polisi wameeleza kuwa tayari watu 17 wamekamatwa kwa kuhusika kwenye tukio hilo.
Miongoni mwa waliouawa katika tukio hilo lililotokea Jumatatu iliyopita ni John Mavumba (68) na mkewe Elizabeth Kaje 55 ambao pamoja na wenzao walikuwa wakituhumiwa kuwa ni washirikina. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA OKTOBA 10, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

RAIS MUSEVEN AKATAA WATU KUSALIMIANA....!!!

shaking hands 
October 9 2014 nchi ya Uganda iliazimisha uhuru wake huku rais wake Yower Museven akizungumza mambo muhimu matatu kwa wananchi wake ambapo ishu ya kwanza ni kuwataka wananchi wake kuwa makini kutokana na tishio la magonjwa ya Marburg pamoja na Ebola hivyo waache kusalimiana kwa kushikana mikono pamoja na kukumbatiana bila kuwepo ulazima wa kufanya hivyo.
Alisema magonjwa hayo kwa sasa yameonekana kuchukua nafasi kubwa duniani na amewataka kuwa makini zaidi ili yasizidi kusambaa lakini pia kumekuwa na utamaduni wa baadhi ya watu hasa wanaoishi maeneo yenye misitu kula nyama za nyani ambazo magonjwa hayo yanaaminika kuanzia huko, nao pia amewataka waache ili haya magonjwa ya ajabu yasije kwa binadamu.
Kitu kingine ambacho rais huyo alizungumza ni kitendo cha mabosi wa mahakama ya The Hague  ya Uholanzi kumtaka rais mwenzake wa Kenya, Uhuru Kenyatta kuhudhuria kikao cha kujibu tuhuma dhidi yake kuhusiana na ghasia zilizotokea nchini kwake na kusema kililenga kudharau na kusitisha mkutano uliofanyika juzi nchini kwake.
Alisema pamoja na Serikali ya nchi hiyo kuomba rais Kenyatta kuhudhuria mkutano huo muhimu lakini mahakama hiyo ilionekana kukataa na kulazimisha ahudhurie katika kesi hiyo.
Hata hivyo Kenyatta alikanusha tuhuma za yeye kuhusika na ghasia zilizosababisha kupoteza maisha ya zaidi ya watu 1200 huku wengine zaidi ya laki sita wakikosa mahali pa kukaa mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu na jambo la mwisho alilozungumzia ni kuhusu timu ya Taifa ilo ambalo inakabiliwa na mchezo dhidi ya Togo ambapo aliwatakia kila la Kheri. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...