Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
imesema haitaendesha uchaguzi wa aina yoyote, wala kuitisha kura ya
maoni hadi kazi ya kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura
itakapokamilika.
Kauli ya NEC imekuja siku moja baada ya Rais
Jakaya Kikwete kukabidhiwa Katiba inayopendekezwa na Mwenyekiti wa
lililokuwa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta na kulitaja suala la
uboreshaji wa daftari la hilo kama mambo matatu yanayoiweka kura ya
maoni kupitisha Katiba hiyo njiapanda.
Mambo mengine ni Sheria inayotaka kura hiyo ipigwe
ndani ya siku 84 baada ya Katiba inayopendekezwa kuchapishwa na
kufanyiwa marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema jana
kwamba kuendesha uchaguzi bila kuboresha daftari hilo ni kuongeza
malalamiko kwa wananchi na wadau, hususan vyama vya siasa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Msimamo wetu (NEC) ni kuwa bila daftari
kuboreshwa hatuko tayari kuendesha uchaguzi wowote na hata huo wa kura
ya maoni,” alisema na kuongeza:
“Sasa tuna takriban vijana milioni 2.3 ambao
wamefikisha umri wa kupiga kura ... lakini kuna watu waliokufa, vyote
hivi vinatakiwa kuboreshwa kwanza na sisi Tume hatuko tayari, naomba
muwaambie wananchi.”
Kuhusu hoja kwamba NEC itumie daftari lililopo
kama ambavyo wamekuwa wakifanya katika uchaguzi mdogo mara kwa mara pale
mbunge anapofariki dunia, Jaji Lubuva alisema tume yake haitaki
yajirudie malalamiko ambayo imeyapata kupitia uchaguzi wa aina hiyo.
“Katika Uchaguzi wa Kalenga, Arumeru Mashariki na
Chalinze, tulilalamikiwa sana kuhusu matumizi ya daftari hili, hivyo
kutokana na malalamiko hayo yaliyotoka kwa vyama vya siasa, hatutaki
tena kupata mengine kama hayo, ndiyo maana nasema muwaambie wananchi
kwamba hatutaendesha chaguzi zozote hadi pale tutakapoboresha daftari,”
alisema Jaji Lubuva.
Kuhusu lini kazi ya kuboresha daftari hilo
itaanza, Jaji Lubuva alisema: “Tunasubiri vifaa vifike na vitakapofika
tu tutaanza mara moja.”
Kauli ya Rais Kikwete
Akizungumza juzi katika sherehe ya makabidhiano ya
Katiba inayopendekezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Rais
Kikwete alielezea maeneo matatu yenye utata ambayo yanatakiwa kupatiwa
ufumbuzi ili kufanikisha hatua hiyo.
Alisema suala la kwanza ni ratiba iliyotolewa na
Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao ambayo inaonyesha
mchakato wa kuandika upya Daftari la Wapiga Kura utakamilika Mei 2015. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi
Alisema suala hilo litaingiliana na mchakato wa Kura ya Maoni
ambayo inatakiwa ifanyike ndani ya siku 84 tangu siku ambayo Katiba
inayopendekezwa ilikabidhiwa kwa Rais.
Alisema ili suala hilo lifanikiwe, ni lazima
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ifanyiwe marekebisho, jambo ambalo
linaweza kushughulikiwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye
atatakiwa kupeleka muswada bungeni.
“Ikifika Mei inabaki miezi miwili au mitatu kabla ya Bunge kuvunjwa na hapo ndipo watu huanza kampeni za uchaguzi mkuu.
“Lakini wapo pia wanaopingana na NEC. Wao wanasema
mbona akifariki mbunge uchaguzi hufanyika. Jambo hili ninawaachieni na
pale ambapo litapatiwa ufumbuzi mtaelezwa.”
Alisema kutokana na kuwapo kwa utata huo, ni jambo
gumu kwa Katiba Mpya kupatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015
kwa sababu ya utata wa masuala hayo matatu, huku akisisitiza jambo hilo
kutazamwa ili kuona kama linaweza kupatiwa ufumbuzi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment