Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje jana
amebadilisha upepo kwenye mkutano wa Rais Jakaya Kikwete, kwa kueleza
kuwa miradi yote ya Serikali ni fedha za wananchi.
Wenje alisema hayo alipopewa nafasi ya kuzungumza
kwenye viwanja vya Mabatini mkoani hapa, akidai kuwa miradi yote
inayotekelezwa na Serikali ni kodi za wananchi wala siyo fedha za CCM.
Wenje alitoa kauli hiyo mbele ya Rais Kikwete
baada ya Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli kudai kuwa CCM ndiyo
inayotekeleza miradi yote ya maendeleo kupitia ilani yake ya uchaguzi ya
mwaka 2010.
Rais Kikwete alikuwa akizindua daraja ya Mabatini lililojengwa kwa gharama ya zaidi ya Sh1 bilioni na Kampuni ya Adivance Life.
Kabla hajazungumza Wenje alipopanda jukwaani hapo,
mamia ya watu waliohudhuria uzinduzi wa daraja hilo walianza kupiga
kelele huku wakishangilia kwa kuonyesha ishara ya vidole viwili juu na
kuimba ‘Peoples Power’. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Baada ya mbunge huyo kuanza kuhutubia alisema:
“Naomba nimjibu Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli kwamba miradi hii siyo
ya CCM, bali ni kodi za Watanzania wakiwamo, wakulima, polisi,
wafanyabiashara, hivyo asitambe hapa kuwa hii ni nguvu ya CCM siyo kweli
hata kidogo.”
Wenje akihutubia kwa jazba alisema kuwa yeye siyo
mtu wa kawaida na hana chembe ya CCM wala wasitegemee kuwa yeye ni
muumini wa chama hicho.
Alitoa mfano kuwa yeye siyo kama tikiti maji
kwamba nje lina rangi ya kijani, lakini ndani lina rangi nyekundu, na
kwamba ataendelea kupiga kelele ili CCM waendelee kufanya mambo ya
maendeleo, kwani bila hivyo hawawezi kufanya lolote.
Kabla Wenje hajamaliza kuhutubia mkutano huo aliwataka wananchi hao kukunja ngumi ili waagane kwa salamu yao.
“Mheshimiwa Rais hapa Mwanza tuna salamu zetu
naomba niage kwa salamu hiyo, haya ndugu zangu naomba tukunje ngumi,
koroga koroga, peoples,” alitamka na mamia ya wananchi waliohudhuria
mkutano huo wakaitikia ‘Power’ huku wakinyoosha vidole viwili juu.
Hali hiyo ilisababisha wafuasi wa CCM kuibuka na
kuanza kusema CCM oyee, jambo lililosababisha wafuasi hao kuanza
kutupiana maneno na kupiga kelele na kusababisha watu kutosikilizana.
Hatua hiyo ilisababisha askari polisi waliokuwa wamevalia sare kuongezwa kwenye uzinduzi huo ili kuimarisha ulinzi.
Awali akihutubia kwenye viwanja vya Kisesa Dk Magufuli alisema
kuwa anampongeza Mbunge wa Nyamagana Wenje kwa kuwa na moyo mzuri, huku
akisema kuwa wote ndani ya chama chake wangekuwa kama yeye mambo
yangekuwa safi.
Dk Magufuli alisema, “Naomba nimpongeze Wenje kwa
kuwa na moyo mzuri, kwani ameweza kushiriki na sisi, viongozi wa chama
chake wangekuwa kama yeye mambo yangekuwa safi, lakini haya yote ya
maendeleo yanafanywa na CCM.”
Akiwa kwenye viwanja vya polisi Mabatini, Dk
Magufuli alijibu kauli ya Wenje baada ya kutoa mfano wa tikiti maji kuwa
nje lina rangi ya kijani, lakini ndani lina rangi nyekundu.
Dk Magufuli alisema, “Ndugu zangu naomba niwaambie
kuwa hata kama ukubali usikubali maendeleo haya ikiwamo ujenzi wa
daraja hili ni nguvu za CCM na Wenje anakubaliana na hilo na mmesikia
wenyewe kuwa yeye siyo kama tikiti maji, lakini ndiyo hivyo kwani nje
rangi yake kijani na ndani nyekundu ndiyo Wenje huyo.”
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia
Nishati, Charles Kitwanga akihutubia baada ya uzinduzi huo alisema
kwenye msafara wa kenge na mamba wapo, hivyo hatashangaa kuona wapinzani
wanahudhuria sherehe za miradi hiyo kwani wanatambua kazi inayofanywa
na CCM. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
JK ahutubia
Akizungumzia na wakazi wa Mabatini na Kisesa, Rais
Kikwete alisema kuwa kazi ya kuandika Katiba imemalizika hivyo kazi
iliyopo ni wananchi kumalizia kazi yao.
Alisema kwenye Katiba iliyopendekezwa hakuna jambo
lililoachwa na kwamba upande wa wanawake asilimia 50 kwa 50 imewekwa na
kwamba watalitazama kwa kina kama ikiwezekana uchaguzi ujao suala hilo
litumike.
“Ndugu zangu naomba niwaambie kuwa kazi ya Katiba
imemalizika, hivyo kilichobaki ni kazi yenu kumalizia. Suala la 50 kwa
50 limewekwa na kwamba tutalitazama kwa kina ili uchaguzi ujao liwepo
suala hilo,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Lakini haya yote majibu yatatoka baadaye baada ya
kulitazama jambo hilo kwanza, lakini kama Katiba haitapita, iliyopo
itaendelea kutumika, hivyo msiwe na hofu.”
Azishukia Halmashauri za Jiji la Mwanza
Rais Jakaya Kikwete aliagiza kuwa fedha za mfuko
wa barabara ambazo zimekuwa zikitolewa zinapaswa kutumika vyema, ili
kukamilisha kazi zilizopangwa.
Na Mwananchi
“Nafahamu kuwa kuna mchwa ambao wanakula fedha
za maendeleo, Mwanza kuna kama bilioni saba zimetolewa kwenye mfuko huo,
hivyo naagiza zitumike kwenye kazi zilizokusudiwa na zisiishie kulipana
posho kwenye vikao vya mabaraza ya madiwani.”
Awali akitoa taarifa ya miradi hiyo, Kaimu Meneja
wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroad), Crispianus Ako alisema Barabara
ya Usagara Kisesa yenye urefu wa kilometa 16 imejengwa kwa gharama ya
zaidi ya Sh17 bilioni na Kampuni ya Nyanza Road na kwamba imekamilika
kwa asilimia 45.
Alisema Daraja la Mabatini limejengwa kwa zaidi ya Sh1 bilioni na kwamba limeakamilika na kuanza kutoa huduma. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment