Marekani sasa imesema inafikiria
kutumia njia mbadala za kuwaokoa maelfu ya Wayazidi, wananchi wa Iraq
waliokwama katika mlima kaskazini mwa Iraq wakikimbia kushambuliwa na
wapiganaji wa dola ya
Kiislamu.Ikulu ya Marekani imerudia kauli yake kuwa haitatumia majeshi ya ardhini kupambana na wapiganaji hao wa dola ya kiislam lakini ikasema inaweza kuwatumia katika kutoa msaada wa kibinadamu.
Msemaji wa Ikulu ya marekani Ben Rhodes amesema Serikali yake ilikuwa ikijadili wazo la Ufaransa, Australia na Canada nao kutoa msaada wa kibinadamu.
Kwa upande wa Uingereza Waziri Mkuu David Cameron amesema mipango thabiti ilikuwa ikiwekwa sawa kwa ajili jumuia ya kimataifa kuwaokoa Yazidi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz