MSICHANA
mmoja mkazi wa eneo la Minga katika Manispaa ya Singida (muuza duka),
amenusurika kifo baada ya kumwagiwa uji wa moto na mke wa tajiri yake na
kumsababishia maumivu makali kutokana na kile kinachosadikiwa kuwa ni
wivu wa kimapenzi.
Muuguzi
wa zamu katika Hospitali ya mkoa wa Singida, wodi namba mbili ya
wanawake, Anna Sprian amefahamisha kuwa binti huyo amejeruhiwa sehemu za
sikio la upande wa kulia na mgongoni, ambapo amesema hali ya mgonjwa
huyo inaendelea vizuri kutokana na matibabu anayoyapata hospitalini
hapo.
Akizungumza
Agosti 10, 2014 kwa tabu, binti huyo Jackline Lasway (23), maarufu kwa
jina la Pendo, amesema majeraha ya moto yapo katika sehemu ya sikio la
upande wa kulia na mgongoni.
Pendo
amesema kuwa tukio hilo limetokea Jumamosi Agosti 9, 2014 saa nane
mchana wakati akiwa dukani kwa bosi wake aliyemtaja kwa jina la, Charles
Kamnde.
Amesema
akiwa anaendelea na kazi zake za kuuza bidhaa mbalimbali dukani hapo,
ghafla alitokea mke wa bosi wake akiwa na chupa yenye uji wa moto na
kuwa alimmwagia usoni ambapo baada ya kumwagiwa uji huo alitaka kujiokoa
ili usimmwagikie usoni na ndipo ulimuunguza kwenye sikio la kulia na
mgongoni na kuwa baada ya mke wa bosi wake kumkosa uso alitoa kisu
kutaka kumchoma kifuani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
“Mimi
sikuwa na ugomvi naye wala sijui chanzo cha yeye kufika dukani na
kunifanyia vile jana, maana kama ni kazi mimi ninafanya kulingana na
maelekezo kutoka kwa bosi wangu Chale lakini sijui kilichomfanya
afikirie kunifanyia huu unyama” alisema.
Aidha,
amesema katika purukushani za kujiokoa asichomwe kisu hicho,
alifanikiwa kumkamata mkono mwanamke huyo na kupiga kelele za kuomba
msaada ambapo watu walifika na kumwokoa baada ya muda mchache ambapo
alichukuliwa na bosi wake hadi Kituo cha Polisi mjini Singida na kupewa
PF3 kwa ajili ya matibabu na kupelekwa katika hospitali hiyo ambako
amelazwa huku akiwa ma majeraha mwilini.
Kwa
upande wake, mmiliki wa duka hilo Chale Kamnde alikiri kutokea kwa
tukio hilo na kusema kuwa hayuko tayari kulizungumzia kwani maelezo
aliyotoa binti huyo yanajitosheleza.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti baadhi ya majirani wa familia hiyo, wameonyesha
masikitiko yao juu ya tukio hilo na hatua ya mwananmke huyo kummwagia
uji msichana huyo huku wakihusisha tukio hilo na wivu wa kimapenzi baina
ya mfanyakazi huyo na mume wa mtuhumiwa.
“Kama
aliona kama kuna sehemu kamkosea angemuonya au kama ameshindwa
kueleweka basi angemshitaki hata polisi kwani kitu alichokifanya
hakiendani na haki za binadamu kwakuwa ni kumdhalilisha huyu msichana
ambaye alikuwa akifanya kazi kwa ajili ya kujipatia kipato chake na
familia yake." alisema shuhuda mmoja
Kamanda
wa Polisi Mkoani hapa, Geofrey Kamwela, amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kuwa wanamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano na mara baada ya
upelelezi kukamilika atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma hizo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment