Mkuu wa polisi katika mji mkuu wa Libya Tripoli, ameuawa na watu wasiojulikana.
Kanali Muhammad Suwaysi alipigwa risasi,
alipokuwa anaondoka kwenye mkutano katika eneo la Tajoura , mtaa ulio
mashariki mwa mji mkuu Tripoli.Libya imekumbwa na vurugu zinazosemekana kusababishwa na wapiganaji wa kiisilamu, ambao walisababisha harakati za kumuondoa mamlakani Muammar Gaddafi mwaka 2011.
Maelfu ya watu wamelazimika kutoroka Tripoli. Zaidi ya miaka mitatu baada ya kuondolewa mamlakani kwa Gadaffi, jeshi la polisi nchini Libya linasemekana kuwa dhaifu,
ikilinganishwa na wapiganaji wanaodhibiti sehemu kubwa za nchi hiyo.
Mamia ya watu wamefariki katika miezi ya Julai na Agosti katika kile kinachoonekana kuwa kukithiri kwa vurugu. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment