Monday, December 16, 2013
ANGALIA MATUKIO YALIYOJILI JANA WAKATI WA MAZISHI YA MZEE MANDELA, QUNU AFRIKA KUSINI
Goodbye to an icon: Nelson Mandela's coffin is slowly lowered into the ground in the hills close to where he grew up at the small, private burial today in Qunu as military salute and mourners watch the poignant moment
Poignant: Nelson Mandela's coffin was carried to his grave and then the flag of the country he loved so ardently was removed and handed to his widow Graca Machel
United in grief: Mandela's widow Graca Michel and his ex-wife Winnie Mandela tearfully comforted one another as they sat next to president Jacob Zuma and Mandela's grandson Mandla as he was laid to rest
Special tribute: The South African air force fly over Mandela's grave in the hills of Qunu where he grew up, which was accompanied by a 21-gun salute
Saturday, December 14, 2013
Friday, December 13, 2013
AZIMIO LA KUWANG'OA MAWAZIRI LAPITISHWA RASMI NA BUNGE...!!!
********
Bunge limepitisha azimio la kuwataka mawaziri katika Ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), kujipima
iwapo wanatosha kuendelea kuongoza wizara hiyo nyeti.
Azimio hilo lilipitishwa jana na wabunge kwa kura
ya ndiyo bila kupingwa, baada ya kuhojiwa na Spika wa Bunge Anne Makinda
iwapo wanaipokea taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
(Laac) iliyowasilishwa na Mwenyekiti wake Rajabu Mbaruku.
Moja ya mapendekezo yake ni Waziri wa Tamisemi,
Hawa Ghasia na manaibu wake, Aggrey Mwanri na Kassim Majaliwa kujipima
kama wanatosha kuendelea kuongoza wizara hiyo kutokana na kugubikwa na
vitendo vya ufisadi.
Kwa mujibu wa taratibu za Bunge, taarifa ya kamati
inapowasilishwa na kupitishwa pamoja na mapendekezo yake, huwa ni
azimio kamili ambapo Serikali hutakiwa kutoa maelezo ya utekelezaji
wake.
Kabla ya azimio hilo kupitishwa, Mwenyekiti wa
Laac, Rajabu Mbaruku alijibu michango ya wabunge waliochangia katika
taarifa ya kamati yake iliyowasilishwa Ijumaa iliyopita, akiwemo Waziri
Ghasia.
KUMBE GRACA MACHEL NA WINNIE MANDELA NI MTU NA 'DADA YAKE'
Winnie Madikizela-Mandela, (77) aliinama kumbusu Graca Machel
(68), kabla ya kukaa katika kiti cha tatu kutoka kile alichokalia
mwanamke huyo. Graca Machel alimwambia maneno machache ‘dada yake’
Winnie wakati akimbusu.
Wanawake hao wote wakiwa wamevalia majaketi meusi
na vilemba, walikumbatiana kwa sekunde kadhaa huku Winnie akitabasamu na
Graca akitazama mbele.
Wote wawili wanaheshimika nchini Afrika Kusini
kutokana na sababu mbalimbali. Winnie anaheshimika kwa mchango wake
mkubwa wa kupigania ubaguzi wa rangi; Graca kwa moyo wake wa kujitolea
kumtunza kiongozi wao mpaka anafariki dunia.
Hata hivyo Winnie amekuwa akikosolewa kutokana na
sababu mbalimbali ikiwamo ile ya kuruhusu wapinzani wake wauawe kwa
kuchomwa moto wakitumia mafuta ya petroli na matairi ya magari.
ZITTO AWASHA MOTO MPYA CHADEMA...!!!
Siku moja baada ya kuwasilisha maelezo yake ya utetezi baada ya
kuvuliwa nyadhifa zake ndani ya Chadema, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa
chama hicho, Zitto Kabwe amekata rufaa Baraza Kuu kupinga hatua hiyo.
Zitto pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema
Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila
Mkumbo walivuliwa nyadhifa zao na Kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika
Novemba 20 na 21 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jana, Mwanasheria wa Zitto, Albert
Msando alitaja sababu mbili za kukata rufaa kuwa ni kukiukwa kwa
taratibu za kuchukua hatua za nidhamu na sababu zilizotolewa kutokuwa
sahihi.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa
Chadema, John Mnyika alisema mambo hayo yalishatolewa ufafanuzi na chama
na kwamba kukata rufaa ni haki ya kikatiba kwa mwanachama yeyote.
“Kukata rufaa ni haki ya kikatiba ya wanachama
yeyote. Rufaa ikatwe tu, itashughulikiwa kwa mujibu wa katiba, kanuni,
maadili na itifaki ya chama. Hata hivyo, ieleweke, rufani inahusu
kuvuliwa nafasi za uongozi, kusudio hilo haliwaondolei wajibu wa
kujieleza kwa maandishi mbele ya Kamati Kuu kwa nini wasifukuzwe
uanachama,” alisema Mnyika.
Thursday, December 12, 2013
DR. ASHA ROSE MIGIRO ALA KIAPO BUNGENI DODOMA LEO
Mbunge
wa Kuteuliwa , Dr. Asha Rose Migiro akiongozwa na Mpambe wa wa Bunge
na kusindindikizwa na badhi ya wabunge wa CCM kuingia Bungeni ili
kuapishwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mjini Dodoma Desemba 12,
2013.
Mbune
wa Kuteuliwa , Dr. Asha Rose Migiro akiongozwa na Mpambe wa wa Bunge
na kusindindikizwa na badhi ya wabunge wa CCM kuingia Bungeni ili
kuapishwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mjini Dodoma Desemba 12,
2013.
OPRAH WINFREY AELEZEA KWA NINI HANA WATOTO...!!!
Kwenye
taarifa za hivi karibuni za Waandishi wa Hollywood, Oprah amefunguka
juu ya kwa nini hana watoto na ukweli wa juu ya hali hiyo kutohusani na
wanachohisi wengi kwamba hana uwezo wa kushika ujauzito huku akielezea
kwa sababu kuu ni yeye kutaka kuwa mwanamke mwenye nguvu.
"Kama
ningekuwa na watoto, watoto wangu wangenichukia. "Wangeishia kwenye
hali ya kuniongelea kama ilivyo kwenye Oprah show; sababu kuna kitu
katika maisha yangu kingeishia kuteseka na inawezekana kabisa wangekuwa
wao.
Gayle [King, rafiki wa karibu Winfrey ambaye ni mama wa watoto
wawili] alikuwa ni aina ya mtoto ambaye, kwenye daraja la saba la
darasa, alikuwa anaandika jina lake chini na majina ya watoto wake.
Wakati alipokuwa na ndoto hizo za mchana, nilikuwa na ndoto za mchana
juu vipi naweza kuwa Martin Luther King.
BASI LA BURUDANI LAPATA AJALI LEO HII MKOANI TANGA, WATU 12 WAPOTEZA MAISHA NA WENGINE KUJERUHIWA
Basi la Burudani baada ya ajali leo Wilaya ya Handeni, Tanga.
Basi la Burudani leo limepata ajali kijiji cha Kwaluguru Kata ya Kwedizinga wilayani Handeni,
Imeripotiwa mpaka sasa watu zaidi ya 12 wamefariki na majeruhi zaidi ya
55. Watu 4 wamepelekwa MOI na KCMC. Tuwaombee majeruhi.
Hospitali ya wilaya ya Korogwe.
Wednesday, December 11, 2013
Tuesday, December 10, 2013
'BABU SEYA, PAPII LAZIMA WATAACHIWA HURU TU'
NGUZA Mbangu,
mtoto mkubwa wa mwanamuziki mahiri wa muziki wa dansi anayetumikia
kifungo cha maisha jela, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya, amesema
mzazi wake pamoja na mdogo wake, Papii, ni lazima wataachiwa huru hivi
karibuni.
Mbangu,
ambaye pia hufahamika kisanii kama Mashine, ambaye hivi sasa ni
mwinjilisti, alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipozungumza na gazeti la Uwazi, akisema kuwa kutolewa jela kwa ndugu zake hao, kutawafanya
Watanzania kumsujudia Mungu kupitia tukio hilo.
“Amini
nakuambia, Mungu amenipa maono, Babu Seya na Papii wako huru, watatoka
tu, kinachosubiriwa ni muda tu ambao hauko mbali, ni lazima watatoka kwa
sababu hawana hatia,” alisema Mbangu, ambaye pia alihukumiwa kifungo
cha maisha jela kama mzazi wake, lakini akaachiwa wakati walipokata
rufaa kwa mara ya kwanza mahakamani.
JIONEE PICHA ZAIDI YA 200 ZA IBADA YA KUMUOMBEA MANDELA INAVYOENDELEA IKIWAMO NA MARAIS NA VIONGOZI WALIOWASILI
Sombre occasion: Members of Nelson Mandela's
family take their seats amid heavy rain ahead of his memorial service
at the FNB Stadium in Soweto, near Johannesburg
Respect: Nelson Mandela is shown on a giant
screen inside the stadium as thousands of South Africans and global
dignitaries file into the ground
NORA AFUNGUKA KUHUSU RAY ADAI ALIMTONGOZA. MSIKILIZE HAPA..!!!
Muigizaji wa kike aliyefanya vizuri kupitia kundi la Kaole Sanaa
Group, Nuru Nassoro aka Nora amedai kuwa amekuwa akifanyiwa fitina na
muigizaji mwenzake Vicent Kigosi aka Ray kwa kuwa aliwahi kumtaka
kimapenzi akamkataa.
Nora amefunguka kupitia kipindi cha Filamonata cha 100.5 Times Fm na
kudai kuwa Ray amekuwa akimbania hata kwenye baadhi ya makampuni ambayo
anapeleka kazi zake.
“Mpaka kwenye kampuni ambayo nimepeleka kazi nimeshawahi kusikia
wanasema, wakaniahidi sana mpaka nikawakubalia walichokuwa wanataka wao.
Lakini yeye (Ray) alitanguliza movies zake, akasema ana movie zake
sijui kitu gani..” amelalamika Nora.
Ameeleza kuwa Ray amewahi kumbania kufanya kazi na marehemu Kanumba, na hata Mtitu sababu ikiwa ile ile kumkataa kimapenzi.
Subscribe to:
Posts (Atom)