NGUZA Mbangu,
mtoto mkubwa wa mwanamuziki mahiri wa muziki wa dansi anayetumikia
kifungo cha maisha jela, Nguza Viking maarufu kama Babu Seya, amesema
mzazi wake pamoja na mdogo wake, Papii, ni lazima wataachiwa huru hivi
karibuni.
Mbangu,
ambaye pia hufahamika kisanii kama Mashine, ambaye hivi sasa ni
mwinjilisti, alitoa kauli hiyo hivi karibuni alipozungumza na gazeti la Uwazi, akisema kuwa kutolewa jela kwa ndugu zake hao, kutawafanya
Watanzania kumsujudia Mungu kupitia tukio hilo.
“Amini
nakuambia, Mungu amenipa maono, Babu Seya na Papii wako huru, watatoka
tu, kinachosubiriwa ni muda tu ambao hauko mbali, ni lazima watatoka kwa
sababu hawana hatia,” alisema Mbangu, ambaye pia alihukumiwa kifungo
cha maisha jela kama mzazi wake, lakini akaachiwa wakati walipokata
rufaa kwa mara ya kwanza mahakamani.
Alisema
tukio hilo litakapotokea, litawafanya Watanzania wote kumsujudia
mwenyezi Mungu, kwa sababu litakuwa ni ishara ya uwezo wake katika
kutenda maajabu.
Babu
Seya na Papii walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004 baada ya
kupatikana na hatia ya kuwanajisi watoto wa Shule ya Msingi Mashujaa iliyopo Sinza.
Hata hivyo, jitihada zao za kujinasua kwa mara ya mwisho ziligonga mwamba hivi karibuni baada ya jopo la majaji watatu kutupilia mbali maombi ya kuachiliwa huru baada ya kufanya mapitio ya kesi hiyo iliyovuta hisia za watu wengi nchini.
Na GPL.
Tafadhari Like page yetu HAPA
Hata hivyo, jitihada zao za kujinasua kwa mara ya mwisho ziligonga mwamba hivi karibuni baada ya jopo la majaji watatu kutupilia mbali maombi ya kuachiliwa huru baada ya kufanya mapitio ya kesi hiyo iliyovuta hisia za watu wengi nchini.
Na GPL.
Tafadhari Like page yetu HAPA
No comments:
Post a Comment