Kadhalika, Mkurugenzi wa Mawasiliano
Ikulu, Salva Rweyemamu alithibitisha kuwa Rais Kikwete atalihutubia
Bunge, Alhamisi... "Nathibitisha ni kweli, ila kwa taarifa nyingine
watafuteni watendaji wa Bunge, kama Katibu wa Bunge nadhani wana taarifa
zaidi."
Wednesday, November 06, 2013
MAELEZO BINAFSI YA MH. ESTER BULAYA KUHUSU WAHARIFU WA DAWA ZA KULEVYA.....!!!
Haya
ni maelezo binafsi ya Mheshimiwa Ester Amos Bulaya bungeni Dodoma
November 4 2013 kuitaka serikali kufanya mabadiliko ya sheria ya dawa za
kulevya na kuanzisha mahakama maalum ya kushughulikia wahalifu wa dawa
za kulevya.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 28(8) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la
mwaka 2013, napenda kutoa maelezo binafsi ya juu ya tatizo sugu la
uagizaji, uuzaji na usafirishaji wa dawa za kulevya linaloongezeka kwa
kasi kubwa nchini, lengo likiwa ni kuitaka serikali ifanye
mabadiliko/marekebisho ya sheria ya Dawa za kulevya na kuanzisha
Mahakama Maalum kushughulikia wahalifu wanaojihusisha na usafirishaji na
biashara ya dawa za kulevya.
Mheshimiwa Spika,
Nimeona ni wakati muafaka kutoa maelezo haya, ili Bunge lako tukufu na Serikali ipate fursa ya kuona uzito wa tatizo hili kutokana na ukweli kwamba katika miaka ya karibuni tatizo la dawa za kulevya katika nchi yetu limeongezeka kwa kasi ya ajabu hali inayopelekea athari kubwa za kiuchumi, kijamii na kiafya. Na mbaya zaidi kundi kubwa linaloathirika ni kundi la vijana, ambao ndio nguvu kazi ya Taifa letu.
Nimeona ni wakati muafaka kutoa maelezo haya, ili Bunge lako tukufu na Serikali ipate fursa ya kuona uzito wa tatizo hili kutokana na ukweli kwamba katika miaka ya karibuni tatizo la dawa za kulevya katika nchi yetu limeongezeka kwa kasi ya ajabu hali inayopelekea athari kubwa za kiuchumi, kijamii na kiafya. Na mbaya zaidi kundi kubwa linaloathirika ni kundi la vijana, ambao ndio nguvu kazi ya Taifa letu.
HILI NDILO JUMBA LA KIFAHARI LENYE UWANJA WA NDEGE HAPO HAPO NYUMBANI
Nyumba
hii ipo huko Las Vegas Marekani na ina heka 40 na indoor car parking
kubwa sana kuingiza magari zaidi ya kumi kwa wakati mmoja na upande wa
mwingine ina zoo humohumo ndani, jet inayopark kwenye airport yako
binafsi hapo mjengoni haina haja ya kwenda kwenye public airport na
ukitaka kumiliki hii nyumba inabidi zikutoke $ 48 millioni.
Vyumba vya kulala vipo vingi kiasi kwamba wakati mwingine inabidi
kuwasiliana kwa simu chumba hadi chumba kwasababu ya umbali wa kufikia
vyumba vingine pia kuna ofisi binafsi kiasi kwamba unaweza usiende
sehemu yoyote kazi zako zote zikafanyika ndani ya hizi heka 40.
Upande wa michezo kuna uwanja wa kucheza golf, basketball, swimming
pool kubwa likiunganishwa na water falls na pia kuna eneo kubwa sana la
wazi na humo ndani kumewekwa nakshi na material ya gharama kuanzia
dinning, jikoni hadi vyumbani.
RAIS KIKWETE KULIHUTUBIA BUNGE KESHO....!!!
Habari zilizopatikana Mjini Dodoma jana na kuthibitishwa na uongozi wa Bunge pamoja na Ikulu, Dar es Salaam zinasema atahutubia mchana.
Kutokana na ujio huo, Serikali imewaelekeza Mawaziri na Manaibu Waziri kutotoka nje ya Dodoma hadi hapo Rais atakapokuwa amehutubia Bunge.
Kadhalika safari zote za Kamati za Bunge ambazo zilikuwa katika mchakato wa kutekelezwa zimeahirishwa hadi baada ya kesho, ili kutoa fursa kwa wabunge wote kuwapo wakati wa hotuba hiyo.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema jana kuwa hata yeye amesikia taarifa kuwa Rais atazungumza bungeni lakini hajui atazungumza kitu gani... "Hata mimi nimesikia kuwa atazungumza lakini sijui atazungumza jambo gani kwa kuwa siyo miongoni mwa watu wanaomwandalia hotuba," alisema Balozi Sefue.
M23 'WAMALIZA UASI' BAADA YA KIPIGO
Waasi wa M23 katika Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo wametangaza kumaliza uasi wao ndani ya nchi hiyo
muda mfupi baada ya kupigwa katika ngome yao ya mwisho na majeshi ya
serikali ya Congo yakishirikiana na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa
kilichopewa uwezo wa kupigana na waasi hao.
Katika taarifa walioitoa waasi hao wamesema badala ya kufanya uasi sasa wataendesha harakati zao kutumia njia ya kisiasa.
Muda mfupi uliopita Kiongozi wa waasi
hao Bertrand Bisimwa ametangaza kuwaamuru mkuu wa wapiganaji wa M23 na
makamanda wa vikosi vyote muhimu wa kundi hilo kuwaandaa wapiganaji wao
kusalimisha silaha, kutawanyika kuondoka katika eneo la mapigano na
kukubaliana na matakwa yatakayowekwa na serikali ya Congo
Awali Msemaji wa Serikali ya Jamuhuri
ya Kidemokrasia ya Congo Lambert Mende aliambia BBC kuwa majeshi ya nchi
yameishambulia ngome ya mwisho ya waasi na wamekimbia na wengine huenda
wakawa wamejisalimisha.
Majeshi ya serikali ya Kongo
yakishirikana na kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa kilichopewa uwezo wa
kupambana na waasi hao walianza mapambano dhidi ya M23 Octoba mwaka huu
na kufanikiwa kuwaondoa katika eneo la Bunagana kwenye mpaka wa Uganda
ambayo ni ngome yao muhimu.
Tuesday, November 05, 2013
NEY WA MITEGO AMPA KICHAPO BABA 'AKE...!KISA KUMUONEA MAMA' AKE...!
Kisa cha kumpa kichapo mzee wa watu.. ni kwa sababu alikuwa anampiga sana mama yake Nay wa Mitego kitu ambacho kilikua kinamuumiza sana yeye, na mwisho wa siku akachukua uamuzi wa kumpiga akimtetea mama yake.
Tukio hilo lilimsukuma Nay wa Mitego kuandika mashairi ya wimbo unaohusu wanawake akiwaambia wanaume wenye tabia kama za baba yake wa kufikia kwamba ‘Mwanamke hapigwi, anatulizwa na mapenzi.’
“Ule wimbo ulikuwa ni dedication kwa mama yangu mzazi, mama yangu mzazi alikuwa anaishi na baba yangu wa kufikia, yule baba yangu alikuwa mkorofi sana, alikuwa anampiga sana mama bila sababu, kiasi kwamba alisababisha mimi na mama tusielewane kwa sababu mimi nilikua sipendi vile alivyokuwa anamfanyia mama, mi nakumbuka kwa bahati mbaya nilishawahi kumpiga yule mzee and then mama yangu akachukua hatua ambayo mimi sikuitegemea kwa sababu mimi nilikuwa namtetea mama.
“Mi nikajifunza kwamba mwanamke hatakiwi kupigwa hata siku moja, na ndo maana nikaimba, so ilikuwa dedication kwa mama yangu na wanawake wote Afrika.” Alisema Nay wa Mitego.
SULEIMAN ANAHITAJI MSAADA WETU AENDE INDIA KUTIBIWA
Wapendwa, Siku ya Leo haikuwa nyepesi kwangu na hata kwa
mtoto Suleiman na familia yake, baada ya kupokea ujumbe rasmi kutoka kwa
madakatri bingwa wa upasuaji wa Hospitali ya CCBRT kuwa Upasuaji huo
HAUTAWEZEKANA kufanyika CCBRT kama tulivyojipa moyo mara ya kwanza.
LAKINI, wamekubali kutusaidia kupata hospitali nzuri nchini
India kwa ajili ya kumsafirisha kijana Suleiman. Nguvu zenu zinahitajika sana
kipindi hiki kigumu kwa familia hii. Tayari msamaria mwema ametoa tiketi moja
ya kumsindikiza Suleiman India. Wapendwa, tushikamane, tunaweza. Hatua
zinazofuata:
Kwanza kupata hospitali India.
Kufanya malipo
Kupata barua ya referral na kutafuta passport na visa ya Suleiman na msindikizaji Safari
CCBRT wataturudishia milioni 3 tulizolipa kama gharama za matibabu na tukijumlisha na pesa alizo nazo Imelda tuitakuwa tumebakiwa na shilingi milioni 6.2. Safari ni ndefu lakini msichoke.
Kwanza kupata hospitali India.
Kufanya malipo
Kupata barua ya referral na kutafuta passport na visa ya Suleiman na msindikizaji Safari
CCBRT wataturudishia milioni 3 tulizolipa kama gharama za matibabu na tukijumlisha na pesa alizo nazo Imelda tuitakuwa tumebakiwa na shilingi milioni 6.2. Safari ni ndefu lakini msichoke.
Asanteni sana. Mola atuongoze. Amen
PAPII KOCHA, BABU SEYA KAZI IMEKWISHA.
Na Mwandishi Wetu
MABERE
Nyaucho Marando, wakili wa mwanamuziki maarufu nchini, Nguza Viking
‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ amesema amemaliza
kazi ya kuwatetea wafungwa hao waliohukumiwa kifungo cha maisha jela
baada ya kukutwa na hatia ya kuwanajisi watoto 12 waliokuwa wakisoma
Shule ya Msingi Mashujaa, Sinza jijini Dar es Salaam..........
Babu Seya (wa pili kulia) na Papii Kocha (wa pili kushoto) wakiwa mahakamani kusikiliza rufaa yao.
Akizungumza
na gazeti hili juzi, Marando alisema kazi aliyokusudia kuifanya
ameimaliza, sasa anasubiri majaji waliosikiliza alichokisema ili watoe
uamuzi wa mwisho lakini pia anamtegemea Mungu.
“Mimi
kazi nimemaliza sasa nawasubiri hao wakubwa (majaji) ili wapime
nilichowaambia kwa mujibu wa sheria na kisha watoe uamuzi, lakini pia
namtegemea Mungu,” alisema Marando.
SERIKALI YAIRUDISHA DARAJA SIFURI
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imebatilisha uamuzi wake wa
kubadili mfumo wa upangaji wa madaraja ya ufaulu kwa mitihani ya kidato
cha nne kama ilivyotolewa awali kwa kurudisha daraja sifuri.
Kutokana na uamuzi huo, sasa daraja la tano lililotangazwa wiki iliyopita kuchukua nafasi ya daraja sifuri sasa limefutwa.
Uamuzi huo umetolewa siku nne baada ya wizara hiyo kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Profesa Sifuni Mchome, kutangaza kuwa serikali imeamua kubadilisha mfumo wa kupanga alama na madaraja ya ufaulu.
Uamuzi wa kushusha alama za ufaulu ulipokewa kwa hisia tofauti na wadau wa elimu nchini ambao walikosoa mfumo huo kwa kueleza kuwa unaipeleka kaburini sekta ya elimu ya Tanzania.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu kutoka Dodoma, alisema baada ya kutafakari serikali imeamua kuondoa daraja la tano kama ilivyokuwa imetangaza awali na kurejesha daraja sifuri.
“Kwanza niwaombe radhi Watanzania kwa mkanganyiko huo uliojitokeza ambao ni jambo moja tu limewachanganya, lakini walio wengi wanapongeza mfumo huu wa madaraja, tulichokuja kuharibu ni ‘statement’ ya neno division five,” alisema.
Monday, November 04, 2013
GLOBAL EDUCATION LINK YAZINDUA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU NJE YA NCHI
Mkurugenzi
wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia
Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi akitoa hotuba yake wakati
wa uzinduzi wa mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo
vya nje ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.
Kaimu
Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Magishi Nkwabi
Mgasa akiwapongeza kampuni ya Global Education Link kwa kushirikiana na
Benki ya Afrika (BOA) kwa kuweza kubuni njia itakayowawezesha wanafunzi
wengi waliokuwa wanapenda kwenye kusoma nje ya nchi ila wanakosa pesa.
Vile vile aliwaomba wanafunzi kuacha kukurupukia vyuo vya nje bila
kutambua kama vinatambulika Tanzania ama lah ili kuwaepushia usumbufu. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
RAIS KIKWETE NAYE ANAFUATILIWA NA MAREKANI?
NA MWANDISHI WETU
HATUA ya Marekani kudaiwa kufuatilia
mawasiliano ya viongozi wa nchi washirika wake wa karibu, sasa ni wazi
imeiacha Tanzania katika wingu la shaka, kama viongozi wake nao
wanafuatiliwa kwa namna ile ile inayoelezwa na viongozi wa Ulaya. Shaka
hiyo inatokana na urafiki wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na
Marekani, ambapo kwa nyakati tofauti, marais watatu wa taifa hilo kubwa
duniani wamepata kuzuru nchini.
Kauli tofauti zilizotolewa ndani ya
wiki hii na majasusi wa mataifa makubwa duniani, ikiwemo Marekani na
Uingereza, wakati wakizungumzia madai ya Marekani kufuatilia mawasiliano
ya Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, kwamba nchi zote duniani
zinachunguzana, ndiyo ambayo baadhi ya wafuatiliaji wa mambo wanadai
kuwa Tanzania bila shaka haiwezi kukwepa kufuatiliwa.
Mbali na hiyo, kauli ambayo imepata
kutolewa na mfanyakazi wa zamani wa shirika la NSA, Edward Snowden,
kwamba ujasusi huo wa Marekani haufanywi dhidi ya watuhumiwa wa ujasusi
na wakazi wa nchi zenye ugomvi na Marekani tu, bali hata marafiki na
waitifaki wa karibu kabisa na nchi hiyo, ndiyo ambayo inajenga mazingira
ya Tanzania nayo kuwemo kwenye orodha hiyo ya kufuatiliwa.
Marais watatu wa Marekani, kwa nyakati
tofauti wamepata kuzuru nchini. Maraisi hao ni pamoja na Bill Clinton,
George W. Bush na Barack Obama, ambaye alitembelea nchini mwezi Julai,
mwaka huu.
BOBBY WILLIAMSON KOCHA MPYA SIMBA SC
Maofisa wa ngazi ya juu wa Simba
wameanza mazungumzo na kocha Bobby Williamson wa Gor Mahia ya Kenya ili
achukue mikoba ya Abdalla Kibadeni.
SIMBA itaanza mzunguko wa pili wa Ligi
Kuu Bara, Januari 26 mwakani dhidi ya Rhino Rangers kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam ikiwa na kocha mpya, Mwanaspoti linaweza
kuthibitisha.
Maofisa wa ngazi ya juu wa Simba
wameanza mazungumzo na kocha Bobby Williamson wa Gor Mahia ya Kenya ili
achukue mikoba ya Abdalla Kibadeni.
Williamson (52), ni straika wa zamani wa West Bromwich Albion na katika mechi 53 aliyoichezea timu hiyo alifunga mabao 11.
Williamson, ambaye ni raia wa Scotland
alijiunga na Gor Mahia msimu huu na tayari ameipa ubingwa wa Ligi Kuu
Kenya ikiwa ni miaka 18 tangu timu hiyo itwae ubingwa wa Kenya mwaka
1995.
WAPINGA KUAHIRISHWA KESI YA KENYATTA
Waathirika wa kesi inayomkabili rais
wa Kenya, Uhuru Kenyatta wameutaka Umoja wa Mataifa kukataa wito wa
kutaka kucheleweshwa kwa kesi dhidi ya Rais Kenyatta katika mahakama ya
kimataifa ya ICC mjini The Hague, Uholanzi.
Baadhi ya viongozi wa Afrika wameandaa
rasimu ya azimio la kuomba kesi inayomkabili Rais Kenyatta iahirishwe
kwa mwaka mmoja kwa masilahi ya usalama wa taifa, kufuatia shambulio la
kigaidi katika kituo cha kibiashara cha Westgate mjini Nairobi.
Lakini mwanasheria wa waathirika,
Fergal Gaynor, amesema kucheleweshwa kwa kesi kutapunguza nafasi ya
kupatikana haki kwa waathirika.
Bwana Kenyatta anakanusha mashitaka
yanayomkabili dhidi ya uhalifu wa kibinadamu, kufuatia ghasia za baada
ya uchaguzi mkuu wa 2007
Subscribe to:
Posts (Atom)