Na Mwandishi Wetu
MABERE
Nyaucho Marando, wakili wa mwanamuziki maarufu nchini, Nguza Viking
‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ amesema amemaliza
kazi ya kuwatetea wafungwa hao waliohukumiwa kifungo cha maisha jela
baada ya kukutwa na hatia ya kuwanajisi watoto 12 waliokuwa wakisoma
Shule ya Msingi Mashujaa, Sinza jijini Dar es Salaam..........
Babu Seya (wa pili kulia) na Papii Kocha (wa pili kushoto) wakiwa mahakamani kusikiliza rufaa yao.
Akizungumza
na gazeti hili juzi, Marando alisema kazi aliyokusudia kuifanya
ameimaliza, sasa anasubiri majaji waliosikiliza alichokisema ili watoe
uamuzi wa mwisho lakini pia anamtegemea Mungu.
“Mimi
kazi nimemaliza sasa nawasubiri hao wakubwa (majaji) ili wapime
nilichowaambia kwa mujibu wa sheria na kisha watoe uamuzi, lakini pia
namtegemea Mungu,” alisema Marando.
Alisema ameiomba Mahakama ya Rufaa Tanzania ifanye marejeo
kuhusu hukumu iliyoitoa na ifute ushahidi uliowatia hatiani wateja wake
hao na adhabu ya kifungo cha maisha jela wanayoitumikia kwa sasa.
Wakili wa mwanamuziki maarufu nchini, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’, Mabere Marando.
Alipoulizwa
alitumia muda gani kuwasilisha hoja zake hizo, Marando alisema takriban
dakika 120 mbele ya jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo, wakiongozwa
na Jaji Nathalia Kimaro akisaidiana na Jaji Mbarouk Mbarouk na Jaji
Salum Massati.
Akiwa
mahakamani hapo, Marando alidai kuwa mahakama iliteleza katika kutoa
uamuzi uliowatia hatiani na kuwafunga maisha wateja wake na kwamba
kuteleza huko kunaonekana waziwazi.
Alifafanua kuwa wakati wakifanya majumuisho ya kesi hiyo,
mahakama ilijiridhisha kwamba kulikuwa na makosa katika kupokea ushahidi
wa watoto wanaodaiwa kufanyiwa vitendo hivyo.
Alidai kuwa ushahidi wa watoto hao ulichukuliwa bila ya kufuata taratibu za uchukuaji wa ushahidi wa watoto.
Alieleza kuwa mtoto anayesoma shule kuanzia ya msingi anapotoa
ushahidi licha ya tahadhari, ana uwezo wa kutambua zuri na baya na
kwamba lazima ushahidi wake uwekwe kwenye kumbukumbu ya maandishi na
kwamba usipoonekana ushahidi wote ni batili na unaondolewa.
Babu Seya na Papii Kocha wakiwa na furaha wakati wakitoka katika Mahakama ya Rufaa Tanzania.
Katika
shauri hilo upande wa Mkurugenzi wa Mashtaka uliwakilishwa na Mawakili
Jackson Mlaki, Angaza Mwaipopo, Emakulata Banzi, Joseph Pande na Apimack
Mbarouk ambao waliyapinga maombi hayo kuhusu marejeo kwa madai kuwa
yamepelekwa mahakamani bila usahihi.
Mahakama hiyo imesema itatoa uamuzi wake siku itakayotangaza.
Babu Seya na Papii Kocha wako jela kwa makosa 10 ya kubaka watoto wa
kike wenye umri kati ya miaka sita na minane na mengine 11 ya kulawiti
watoto wa kike wenye umri kama huo.
Walidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Aprili na Oktoba 2003
eneo la Sinza Kwaremy jijini Dar es Salaam.
Katika kesi hiyo, Mwalimu wa
Shule ya Msingi Mashujaa, Sigirinda Ligomboka ambaye alishitakiwa kwa
makosa mawili ya kumsaidia Babu Seya kutenda makosa hayo kwa kuwaruhusu
baadhi ya wanafunzi hao kutoka madarasani, aliachiwa huru na Mahakama ya
Kisutu.Chanzo Global Publishers Blog
No comments:
Post a Comment