Mkurugenzi
wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia
Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi akitoa hotuba yake wakati
wa uzinduzi wa mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo
vya nje ya nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam.
Kaimu
Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Magishi Nkwabi
Mgasa akiwapongeza kampuni ya Global Education Link kwa kushirikiana na
Benki ya Afrika (BOA) kwa kuweza kubuni njia itakayowawezesha wanafunzi
wengi waliokuwa wanapenda kwenye kusoma nje ya nchi ila wanakosa pesa.
Vile vile aliwaomba wanafunzi kuacha kukurupukia vyuo vya nje bila
kutambua kama vinatambulika Tanzania ama lah ili kuwaepushia usumbufu. Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Naibu
katibu mkuu Tamisemi, Zuberi Samataba akiongea machache katika uzinduzi
wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya nchi
uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa taasisi ya Global Education Link, AbdulMalki Molel akitoa maelezo jinsi mpango wa utoaji
wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ambapo jna ilikuwa ndiyo
uzinduzi katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania, Ammish OWUSU-AMOAH akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi
wa mpango wa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya nje ya
nchi uliofanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Mmoja
ya wazazi waliohudumiwa na taasisi ya Global Education Link wakitoa
ushuhuda wao jinsi watoto wao walivyowezeshwa kutafutiwa nafasi za
masomo kwa vyuo vya nje ya nchi bila usumbufu kwa vyuo vinavyotambuliwa
na Tume ya Vyuo
Vikuu Tanzania. Ambapo wazazi hao walitoa rai yao kwa wazazi wengine
kuendelea kuiunga mkono GEL ili isonge mbele zaidi kwa vile inafanya
kazi zake kiuhakika bila ya kudanganya.
Waliongeza kuwa kwa
sasa wanafunzi wengi wamekuwa na moyo wa kusoma nje ila kuna baadhi ya
makampuni ambayo yamekuwa yakiwadanganya na kujikuta wakidondokea kwenye
vyuo ambavyo havitambuliki mwisho wake kuishia kupoteza hela na muda.
Uzinduzi huo ulifanyika jana katika hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaama.
Mkurugenzi
wa Elimu ya juu, Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi, Profesa Sylvia
Temu ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyemwakilisha Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi (katikati) akizindua. Pembeni toka kulia ni Wafanyakazi wa GEL, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Afrika Tanzania, Ammish OWUSU-AMOA, Kaimu
Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Magishi Nkwabi
Mgasa pamoja na Naibu katibu mkuu Tamisemi, Zuberi Samataba.
Hiki ndicho kilichozinduliwa. Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
No comments:
Post a Comment