Waathirika wa kesi inayomkabili rais
wa Kenya, Uhuru Kenyatta wameutaka Umoja wa Mataifa kukataa wito wa
kutaka kucheleweshwa kwa kesi dhidi ya Rais Kenyatta katika mahakama ya
kimataifa ya ICC mjini The Hague, Uholanzi.
Baadhi ya viongozi wa Afrika wameandaa
rasimu ya azimio la kuomba kesi inayomkabili Rais Kenyatta iahirishwe
kwa mwaka mmoja kwa masilahi ya usalama wa taifa, kufuatia shambulio la
kigaidi katika kituo cha kibiashara cha Westgate mjini Nairobi.
Lakini mwanasheria wa waathirika,
Fergal Gaynor, amesema kucheleweshwa kwa kesi kutapunguza nafasi ya
kupatikana haki kwa waathirika.
Bwana Kenyatta anakanusha mashitaka
yanayomkabili dhidi ya uhalifu wa kibinadamu, kufuatia ghasia za baada
ya uchaguzi mkuu wa 2007
No comments:
Post a Comment