Kiongozi huyo wa dini, aliyejeruhiwa
maeneo ya usoni, mikononi na kifuani baada ya kumwagiwa tindikali hiyo
alisafirishwa jana na ndege ya kukodi ya Shirika la Coastal kutoka
visiwani humo hadi Dar es Salaam na baadaye kupelekwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.
Sunday, September 15, 2013
PADRI ALITISHIWA KIFO MIEZI MITATU KABLA
Padri Joseph Magamba wa Kanisa Katoliki Parokia ya Machui Zanzibar aliyemwagiwa tindikali akisaidiwa kushuka kwenye ndege na Padri Thomas Assenga(kushoto) wa Kanisa la Mtakatifu Joseph Zanzibar baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana kuelekea katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.Picha na Fidelis Felix
Siku moja baada ya Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, Mkoa wa Kusini Unguja, Joseph Mwang'amba kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana, imebainika kuwa alitishiwa kuuawa miezi mitatu kabla ya kukutwa na tukio hilo.
Wakati Padri huyo akieleza hayo, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, ameijia juu polisi kwa kushindwa kudhibiti matukio ya viongozi wa dini na serikali visiwani humo, kushambuliwa kwa kumwagiwa tindikali huku akilitaka kuwakamata waliohusika na tukio hilo.
WAFANYAKAZI HARAMU WAMEAJIRIWA KWENYE NAFASI NYETI JNIA
Baadhi ya wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam wamedai kuwepo kwa wafanyakazi ambao ni wahamiaji haramu katika uwanja huo, ambao wamekuwa wakipewa nafasi nyeti katika mamlaka hiyo.
Aidha, wameeleza kuwa wahamiaji hao haramu pia wamekuwa wakipatiwa vitambulisho nyeti kama watanzania halisi.
Wafanyakazi walimueleza Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe jana alipofanya ziara uwanjani hapo na kuzungumza na wafanyakazi wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) katika uwanja huo.
Mfanyakazi Dominic Bomani alisema
licha ya juhudi za serikali kuwaondoa nchini wahamiaji haramu, kiwanja
hicho cha ndege kimekuwa chimbuko la wahamiaji hao ambao wamekuwa
wakipewa nafasi nyeti.
Aliomba serikali kusaidia katika
kuwabaini na kuwaondoa wahamiaji hao ikiwa ni pamoja na kutoa nafasi
hizo ziweze kushikiliwa na watanzania ambao wako wenye sifa stahili.
Saturday, September 14, 2013
IRENE UWOYA ATIWA MBARONI KWA WIZI WA SIMU ( AINA YA iPhone 5)
MSANII aliyewahi kutamba
kisha kuporomoka kwa kasi katika tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa
sababu ya tabia zake chafu, Irene Uwoya, amefikishwa Kituo cha Polisi
Msimbazi kwa wizi wa simu aina ya iPhone 5.
Kwa mujibu wa habari za kipolisi, mmiliki wa simu hiyo ni mwanamme aliyejulikana kwa jina la Mohammed Marjey, mkazi wa Dar.
Uwoya ambaye siku hizi anajitutumua kwa kuanzisha kipindi kwenye runinga moja ya Bongo baada ya kushindwa kwenye filamu, alidakwa na askari wa Kituo cha Polisi Msimbazi, Dar baada ya kusakwa usiku na mchana kwa kutumia kumbukumbu ya jalada la kesi namba MS/RB/8522/13 WIZI KUTOKA MAUNGONI.
Kwa mujibu wa habari za kipolisi, mmiliki wa simu hiyo ni mwanamme aliyejulikana kwa jina la Mohammed Marjey, mkazi wa Dar.
Uwoya ambaye siku hizi anajitutumua kwa kuanzisha kipindi kwenye runinga moja ya Bongo baada ya kushindwa kwenye filamu, alidakwa na askari wa Kituo cha Polisi Msimbazi, Dar baada ya kusakwa usiku na mchana kwa kutumia kumbukumbu ya jalada la kesi namba MS/RB/8522/13 WIZI KUTOKA MAUNGONI.
Simu aina ya iPhone 5 kama inayodaiwa kuibiwa na Uwoya.
MULUGO AMEAHIDI KITITA CHA SH. MILIONI MBILI IWAPO TIMU YA MBEYA CITY ITAISHINDA TIMU YA YANGA LEO JIJINI MBEYA
Waziri Mulugo akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya amesema atahakikisha kuwa kila timu itakayotia mguu mbeya inaondoka na kipigo cha magoli |
WAMAREKANI WADAI KUGUNDUA CHANJO INAYOANGAMIZA UGONGWA WA UKIMWI
Washington. Wanasayansi nchini Marekani
wamegundua chanjo ambayo wanaamini itaweza kuangamiza Virusi Vya Ukimwi
(VVU) kwa binadamu.
Katika majaribio ya chanjo hiyo, wanasayansi hao wameelezea kuwa imeonyesha mafanikio kwa kuangamiza kabisa virusi wanaofanana na VVU kwa nyani.
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limechapisha kwenye tovuti yake kuwa baada ya kubaini hilo sasa wamekusudia kufanya majaribio ya chanjo hiyo kwa binadamu.
Likinukuu taarifa iliyochapishwa kwenye jarida la kisayansi linaloitwa; Nature, lilimnukuu Mwanasayansi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Oregon, nchini Marekani akisema walijiridhisha kuwa chanjo hiyo iliangamiza virusi vyote kwenye mwili wa nyani.
Katika majaribio ya chanjo hiyo, wanasayansi hao wameelezea kuwa imeonyesha mafanikio kwa kuangamiza kabisa virusi wanaofanana na VVU kwa nyani.
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limechapisha kwenye tovuti yake kuwa baada ya kubaini hilo sasa wamekusudia kufanya majaribio ya chanjo hiyo kwa binadamu.
Likinukuu taarifa iliyochapishwa kwenye jarida la kisayansi linaloitwa; Nature, lilimnukuu Mwanasayansi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Oregon, nchini Marekani akisema walijiridhisha kuwa chanjo hiyo iliangamiza virusi vyote kwenye mwili wa nyani.
SAMAKI HATARI WAINGIZWA NCHINI....!!!
Afya za Watanzania ziko shakani
kutokana na kuwapo kwa biashara ya kuingiza samaki kutoka nje ya nchi,
wanaodaiwa kuharibika na kuuzwa katika la Soko la Feri jijini Dar es
Salaam.
Samaki hao kutoka Yemen, Dubai, China na Japan, wanaoingizwa nchini wakiwa wameganda kwenye barafu, wengi huharibika muda mfupi baada ya barafu kuyeyuka au baada ya kununuliwa.
Samaki hao kutoka Yemen, Dubai, China na Japan, wanaoingizwa nchini wakiwa wameganda kwenye barafu, wengi huharibika muda mfupi baada ya barafu kuyeyuka au baada ya kununuliwa.
Uchunguzi wa gazeti hili umegundua
kuwa samaki hao huletwa nchini kutafutiwa soko baada ya kukaa kwenye
majokofu kwa muda mrefu huko wanakotoka, kiasi cha kuelekea kuharibika.
Ili wasiharibike, samaki hao aina ya
Marckerel hukaangwa hadi wakauke. Uchunguzi zaidi umebaini kuwa wanunuzi
wake wakuu ni wafanyabiashara wa chakula wakiwamo wamiliki wa migahawa
na Mama Lishe wanaofanya shughuli zao katika miji ya Dar es Salaam,
Pwani, Morogoro na Dodoma.
Samaki hao wanauzwa kwa bei ya chini
ambayo ni Sh38,000 kwa boksi lenye uzito wa kilo 15, ikilinganishwa na
wanaovuliwa hapa nchini ambao bei yake ni Sh60,000, kwa uzito huohuo.
Inaelezwa kuwa samaki hao baadhi yake
ni waleambao wamekwisha muda wake wa kutumika katika nchi hizo, hivyo
kuingizwa nchini kutafutiwa soko.
Gazeti hili lilifika katika soko hilo
kwa siku mbili na kushuhudia samaki hao wakiuzwa kwa wingi, huku wauzaji
wakihimizwa wateja wao kuwahi kuwakaanga au kuwaweka kwenye jokofu.
YANGA WAPEWA SIKU 14 KUWALIPA NSAJIGWA NA MWASIKA 15.5m
Yanga imepewa siku 14 kuanzia (Septemba 13 mwaka huu) kuwalipa waliokuwa wachezaji wake msimu uliopita, nahodha Shadrack Nsajigwa na Stephen Mwasika wanaoidai klabu hiyo jumla ya sh. milioni 15.5.
Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya
Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) iliyokutana jana (Septemba 12 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo
mengine ilisikiliza madai ya wachezaji hao.
Fedha hizo ni ada ya usajili ambayo
klabu hiyo ilikubaliana na wachezaji hao wakati ikiwasainisha mikataba.
Yanga imeshawalipa sehemu ya fedha walizokubaliana na kiasi hicho ndicho
bado hakijalipwa. Nsajigwa anadai sh. milioni 9 wakati Mwasika ni sh.
milioni 6.5. Chanzo: shaffihdauda
MUME AMSAMEHE MKEWE ALIYEPANGA KUMUUA....!!!
Mwanamke mmoja mfanyabiashara mjini
Nairobi, Kenya, ambaye alikiri kosa la kupanga njama ya kumuua mumewe,
ameachiliwa na mahakama
Bi Faith Wairimu Maina, aliachiliwa huru baada ya mumewe kuitaka mahakama kufuta kesi yake kwani amemsamehe.
Bi Faith alikiri kuwa aliwakodi
mamluki kumuangamiza mumewe. "Nataka kumsamehe kwa sababu ya watoto na
familia yetu," mumewe Faith aliambia mahakama.
Mwanamke huyo alikiri makosa ya
kupanga njama ya kutaka kumuua mumewe baada ya kukamatwa ingawa baadaye
alibadili msimamo wake na kukanusha madai hayo na alitarajiwa
kushtakiwa.
Polisi walitibua njama ya mwanamke
huyo baada ya majasusi waliokuwa wanajidai kuwa mamluki kupokea malipo
ya shilingi 40,000 kuitekeleza njama hiyo.
PADRI AMWAGIWA TINDIKALI ZANZABAR
Polisi huko visiwani Zanzibar wanachunguza tukio la kasisi wa kanisa katoliki kushambuliwa kwa tindikali.
Imeelezwa kuwa Kasisi huyo Anselmo
Mwang'amba, alimwagiwa tindikali akitoka mgahawa mmoja wa kutumia
mtandao mjini Zanzibar. Tukio hilo linatokea ndani ya mwezi mmoja tangu
wasichana wawili wa kiingereza kushambuliwa.
Hili ni janga jingine kwa Zanzibar ambayo imekuwa ikizongwa na matukio ya aina hii kwa muda sasa.
Mkurugenzi wa upelelezi wa Zanzibar,
Yusufu Ilembo ameieleza BBC kuwa bado hawajakamata mtu yoyote kuhusika
na tukio hilo ingawa amethibitisha kuwa uchunguzi tayari umeanza.
Ameeleza kuwa Kasisi Mwang'amba aliungua usoni na mabegani na kwamba anaendelea kutibiwa. Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
Katika miaka ya karibuni Zanzibar imekabiliwa na mikasa ya watu kushambuliwa hivi na kuzua hisia kuwa chuki za kidini.
Mapema mwaka huu kasisi mwingine wa kanisa katoliki alishambuliwa kwa risasi na kuuawa.
Mwezi uliopita Zanzibar ilitikisika kutokana na wasichana wawili wangereza kushambuliwa kwa tindikali na watu wasiojulikana.
Kiongozi mmoja wa dini ya kiislamu pia alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana.
MAMA MANGWEA AJITOSA KUMTETEA MWANA FA.
Mama wa MwanaHip Hop aliyewahi kuaminika kuwa bingwa wa mitindo
huru, Albert Mangwea aliyefariki mwezi Mei mwaka huu, Denisia Costantine
Mangwea ameibuka na kumtetea mwanamuziki wa kizazi kipya Hamis
Mwin’juma ambaye anatuhumiwa kuahidi pesa kwa mama huyo na kuingia
mitini.
Sakata hilo ambalo limekuwa likiripotiwa tangu
mwishoni mwa wiki iliyopita, linatokana na kitendo cha mwanamuziki huyo
(MwanaFA) ambaye aliwahi kuahirisha onesho lake, baada ya kifo cha
msanii mwenzake (Albert Mangwea), kutokuweka hadharani hitimisho la
ahadi aliyoitoa kwa familia ya marehemu.
Tarehe 31 ya mwaka huu ilikuwa ni tarehe ya onesho
la The Finest ambalo MwanaFA alikuwa akitimiza miaka 13 ya muziki wake,
akawa na lengo pia na kuugeuza muziki wa Hip Hop uwe na sura ya
kistaarabu na kibiashara pia ili kuuongezea aina ya mashabiki.
Siku moja kabla ya onesho, msiba wa Albert Mangwea
ukatokea, na hapo ikamlazimu mwanamuziki huyo kuahirisha onesho lake,
na kulisogeza wiki mbili mbele huku akiahidi asilimia 15 ya faida
atakayopata, angeipeleka kwa familia ya Albert Mangwea.
Friday, September 13, 2013
VATICAN SASA KUJADILI KUHUSU UWEZEKANO WA MAPADRI WAKATOLIKI KUOA....!!!
Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Askofu Mkuu Pietro Parolin |
Mjadala wa sasa umeibuliwa na Waziri wa
Mambo ya Nje wa Vatican, Askofu Mkuu Pietro Parolin ambaye aliteuliwa
hivi karibuni kushika wadhifa huo aliposema useja, yaani maisha ya
utumishi ndani ya kanisa bila ndoa siyo imani, bali utamaduni na mazoea.
Akizungumzia kauli hiyo, Msemaji wa
Vatican, Federico Lombardi alisema kauli ya Askofu Parolin haipingani na
mafundisho ya kanisa. Askofu Mkuu Parolin ambaye aliteuliwa karibuni na
Papa Francis kushika wadhifa huo kutoka kwa Kardinali Tarcisio Bertone
amenukuliwa na Gazeti la El Universal la Venezuela, Amerika ya Kati
akieleza kuwa suala hilo linaweza kujadiliwa.
ETO'O: 'NISHAWAHI KUAPA KUTOCHEZA KWENYE TIMU INAYOFUNDISHWA NA MOURINHO
Samuel Eto'o amefunguka na kusema kwamba aliwahi kuapa kutokuja kucheza chini ya kocha Jose Mourinho.
Nyota huyo wa zamani wa Barcelona
alisema alikuwa na mahusiano yasiyoridhisha na na kocha wa kireno kabla
ya hawajafanya kazi pamoja wakiwa Inter Milan, mahala ambapo walishinda
vikombe vitatu kwa msimu mmoja.
Eto'o ameungana tena na Mourinho
wakati alipojiunga na Chelsea hivi karibuni akitokea klabu ya Anzhi
Makhachkala kwa mkataba wa mwaka mmpja utaoisha wakati ujao wa kiangazi. Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
Huu ulikuwa uhamisho ambao Eto'o mwanzoni asingeweza kukubaliana nao.
"Kabla hatujakutana kule Inter, Jose
na mimi hatukujuana vizuri kwa ukaribu, hivyo mahusiano yetu hayakuwa
yakieleweka," alikaririwa Eto'o alipohojiwa na gazeti la The Sun.
"Nadhani nilisema huko nyuma kwamba nisingekuja kuichezea klabu inayofundishwa na Jose.
"Lakini mungu anajua zaidi. Alitaka kunionyesha sikuwa sahihi na leo hii Jose ni rafiki yangu mkubwa, pia ni kocha wangu kwa mara nyingine tena." Chanzo: Shaffihdauda
"Lakini mungu anajua zaidi. Alitaka kunionyesha sikuwa sahihi na leo hii Jose ni rafiki yangu mkubwa, pia ni kocha wangu kwa mara nyingine tena." Chanzo: Shaffihdauda
Subscribe to:
Posts (Atom)