Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Askofu Mkuu Pietro Parolin |
Mjadala wa sasa umeibuliwa na Waziri wa
Mambo ya Nje wa Vatican, Askofu Mkuu Pietro Parolin ambaye aliteuliwa
hivi karibuni kushika wadhifa huo aliposema useja, yaani maisha ya
utumishi ndani ya kanisa bila ndoa siyo imani, bali utamaduni na mazoea.
Akizungumzia kauli hiyo, Msemaji wa
Vatican, Federico Lombardi alisema kauli ya Askofu Parolin haipingani na
mafundisho ya kanisa. Askofu Mkuu Parolin ambaye aliteuliwa karibuni na
Papa Francis kushika wadhifa huo kutoka kwa Kardinali Tarcisio Bertone
amenukuliwa na Gazeti la El Universal la Venezuela, Amerika ya Kati
akieleza kuwa suala hilo linaweza kujadiliwa.
Hata hivyo, msimamo huo unaweza kupingwa
na waumini wengi wenye misimamo mikali ndani ya kanisa hilo ambao bado
wanaamini kuwa kuishi useja ndiyo mfumo na utamaduni unaofaa ndani ya
kanisa hilo.
Kwa upande wake, Papa Francis mwaka jana
hata kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo, alizungumzia suala hilo
kwa maneno mafupi kuwa angependa kuona mfumo huo ukibaki kama ulivyo. Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
Msimamo huo wa Askofu Mkuu Parolin
unamaanisha kuwa kuna haja ya kanisa hilo kufanya mabadiliko makubwa
kwenye kanuni ngumu ya useja kwa mapadri wake.
“Useja si suala la kitaasisi, lakini
linaonekana kuwa kweli, linaaminika. Ni suala gumu ambalo linaweza
kujadiliwa kwani si imani ya kanisa (dogma), halihusu imani ya kanisa,”
alisema Askofu Mkuu Parolin.
Askofu huyo alisema kwa kuwa siyo suala la kiimani, useja katika kanisa hilo limezama zaidi kwenye utamaduni. Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
“Juhudi za kanisa kuendelea na mfumo
huo, hazina budi kufanyika, pia zisizuie mjadala,” alisema na kuongeza:
“Hakuna anayeweza kuzuia mjadala huu kwa maelezo kuwa ni suala ambalo
limepitwa na wakati.”
Akiwa Waziri Vatican, Askofu Mkuu
Parolin anaonekana kwa wengi kama mtu mwenye nguvu na ushawishi mkubwa
baada ya Papa Francis tofauti na watangulizi wengi wa kiongozi huyo wa
Kanisa Katoliki duniani ambao kwa miaka mingi wamekuwa na msimamo kwamba
jambo hilo halifai kujadiliwa. Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
“Kumekuwa na upinzani mkubwa kwenye
mjadala huu wa useja,” anasema Mhariri Mtandao na Mhariri wa zamani wa
Gazeti la Kikatoliki la Uingereza, The Tablet, Abigal Frymann na
kuongeza: “Mawazo haya ya Parolin yatazusha mjadala mkubwa.”
No comments:
Post a Comment