Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepata habari kupitia
mtandao wa Jamii Forum na Gumzo la Jiji na mingineyo kuwa likizo
zimesitishwa Jeshini na waliokuwa likizo wameitwa kurudi kazini.
Taarifa hizo pia zimeeleza kwamba Brigedi za Tembo na Kifaru zimepewa
maagizo ya kuwa katika hali ya utayari endapo watahitajika kusonga
mbele.
JWTZ linapenda kuwaeleza wananchi pamoja na watumiaji wa mitandao
hiyo kuwa taarifa hizo ni za upotoshaji mtupu na hazina ukweli wowote.
Aidha, taarifa hizo ni zenye nia ya kuzorotesha uhusiano mzuri uliopo
kati ya nchi yetu (Tanzania) na majirani zake.
Sambamba na taarifa hii, pia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania
linapenda kutoa taarifa za kutohusika na viunganishi vya JWTZ kwenye
mitandao ya ‘Facebook‘ – (Facebook/JWTZ) na ‘Twitter‘ (Twitter/
JWTZ).
Mitandao hiyo yenye viunganishi vya JWTZ imekuwa ikijihusisha na
kutoa taarifa ambazo zimekuwa zikichangiwa na watu mbalimbali, ambapo
baadhi yao wamekuwa wakitoa taarifa za upotoshaji na zisizo sahihi.
Tunapenda kutaarifu kwamba akaunti za facebook na twitter zilizotajwa
siyo za JWTZ.
Hatua zimechukuliwa za kuwatambua wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria.
Aidha inasisitizwa kwamba JWTZ lina taratibu za zake zinazotumika
kufanya mawasiliano na Vyombo vya Habari, Taasisi, au mtu binafsi kuhusu
utoaji wa taarifa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi
Dar es salaam, Tanzania
Kurugenzi ya habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi
Dar es salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment