Mwanamke mmoja mfanyabiashara mjini
Nairobi, Kenya, ambaye alikiri kosa la kupanga njama ya kumuua mumewe,
ameachiliwa na mahakama
Bi Faith Wairimu Maina, aliachiliwa huru baada ya mumewe kuitaka mahakama kufuta kesi yake kwani amemsamehe.
Bi Faith alikiri kuwa aliwakodi
mamluki kumuangamiza mumewe. "Nataka kumsamehe kwa sababu ya watoto na
familia yetu," mumewe Faith aliambia mahakama.
Mwanamke huyo alikiri makosa ya
kupanga njama ya kutaka kumuua mumewe baada ya kukamatwa ingawa baadaye
alibadili msimamo wake na kukanusha madai hayo na alitarajiwa
kushtakiwa.
Polisi walitibua njama ya mwanamke
huyo baada ya majasusi waliokuwa wanajidai kuwa mamluki kupokea malipo
ya shilingi 40,000 kuitekeleza njama hiyo.
Mwendesha mkuu wa mashtaka alisema
kuwa alifahamishwa wanandoa hao walikubali kusameheana na kuwa bwana
Muthee ambaye ni mumewe mwanamke huyo akataka kesi hiyo kufungwa. Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
Wakili wa mwanamke huyo alisema kuwa
hakuwa na pingamizi zozote kutupilia mbali kesi hiyo. Bwana Muthee
alisema kuwa mwanamke huyo ni mkewe na alimsamehe kwa sababu ya familia,
jambo linaloruhusiwa na mahakama.
Mwanamke huyo tayari alikuwa amewalipa
mamluki kumuua mumewe na kisha kuwataka wamletee nguo zake zenye damu
ili aweze kuwalipa pesazitakazokuwa zimesalia ambazo ni shilingi 160,000
na pia aweze kuthibitisha kuwa mumewe ameuawa.
Majajusi walisema kuwa ilikuwa mara ya
pili kwa mwanamke huyo kujaribu kumuua mumewe baada ya njama ya kwanza
kukosa kufaulu licha ya kuwalipa mamluki waliomwambia kuwa walishikwa na
uoga. Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
Mwanamke huyo alipanga njama ya kumuua mumewe kutokana na madai kuwa alikuwa na uhusiano na mwanamke mwingine.
No comments:
Post a Comment