Afya za Watanzania ziko shakani
kutokana na kuwapo kwa biashara ya kuingiza samaki kutoka nje ya nchi,
wanaodaiwa kuharibika na kuuzwa katika la Soko la Feri jijini Dar es
Salaam.
Samaki hao kutoka Yemen, Dubai, China na Japan, wanaoingizwa nchini wakiwa wameganda kwenye barafu, wengi huharibika muda mfupi baada ya barafu kuyeyuka au baada ya kununuliwa.
Samaki hao kutoka Yemen, Dubai, China na Japan, wanaoingizwa nchini wakiwa wameganda kwenye barafu, wengi huharibika muda mfupi baada ya barafu kuyeyuka au baada ya kununuliwa.
Uchunguzi wa gazeti hili umegundua
kuwa samaki hao huletwa nchini kutafutiwa soko baada ya kukaa kwenye
majokofu kwa muda mrefu huko wanakotoka, kiasi cha kuelekea kuharibika.
Ili wasiharibike, samaki hao aina ya
Marckerel hukaangwa hadi wakauke. Uchunguzi zaidi umebaini kuwa wanunuzi
wake wakuu ni wafanyabiashara wa chakula wakiwamo wamiliki wa migahawa
na Mama Lishe wanaofanya shughuli zao katika miji ya Dar es Salaam,
Pwani, Morogoro na Dodoma.
Samaki hao wanauzwa kwa bei ya chini
ambayo ni Sh38,000 kwa boksi lenye uzito wa kilo 15, ikilinganishwa na
wanaovuliwa hapa nchini ambao bei yake ni Sh60,000, kwa uzito huohuo.
Inaelezwa kuwa samaki hao baadhi yake
ni waleambao wamekwisha muda wake wa kutumika katika nchi hizo, hivyo
kuingizwa nchini kutafutiwa soko.
Gazeti hili lilifika katika soko hilo
kwa siku mbili na kushuhudia samaki hao wakiuzwa kwa wingi, huku wauzaji
wakihimizwa wateja wao kuwahi kuwakaanga au kuwaweka kwenye jokofu.
Gazeti hili pia lilinunua boksi moja
la samaki hao lenye uzito wa kilo 15 kwa Sh38,000, lakini lilipodai
kupewa stakabadhi wauzaji walisema: "Hatuna stakabadhi ya kukupa ndugu
yangu," alisema muuzaji.
Baada ya kuwasafirisha kutoka Soko la
Feri hadi ofisi za gazeti hili zilizopo Tabata Reli, Barabara ya Mandela
kwa muda wa saa moja, tayari walikuwa wameharibika.
Baadhi ya samaki hao walianza kuoza
huku wengine wakiwa wamelegea tofauti na samaki wa kawaida. Baada ya saa
nne kupita, samaki hao waliharibika na kuanza kutoa harufu mbaya.
Dk Raymond Mwenekano wa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili, anayataja madhara ya ulaji wa samaki wa aina hiyo
kuwa ni kupata magonjwa kama vile kansa ya utumbo, mwili kuwasha,
kubabuka na vidonda mwilini.
"Madhara yake ni makubwa, ndiyo maana
siku zote tunasisitiza kula vyakula visivyokaa sana kwani vingine
vimehifadhiwa kwa dawa na wanaofanya hivi ni wafanyabiashara kwa faida
yao," alisema Dk Mwenekano.
Daktari huyo alisema pia yapo madhara
ya muda mfupi ambayo ni mtu aliyekula samaki wa aina hiyo kuharisha na
kutapika muda mfupi baada ya kula.
Mamlaka husika
Ofisa Afya katika Soko la Feri,
Barnabas Hanje alithibitisha kuwepo katika soko hilo, samaki wabovu
wanaotoka nje ya nchi na kwamba ofisi yake imekuwa ikipokea malalamiko
mengi kuhusu suala hilo.
Hanje ambaye pia alitajwa kuwa ni
Mwakilishi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) katika soko
hilo, alisema kesi zinawahusu wanunuzi wanaodai warejeshewe fedha au
kubadilishiwa samaki, baada ya wale waliowanunua kuharibika haraka hata
kabla hawajatoka sokoni hapo.
Alifafanua kuwa baadhi ya kesi hupata
ufumbuzi baada ya waliouza samaki wabovu kukubali kurejesha fedha kwa
wahusika na kwamba kwa pale mwagizaji wa jumla anapokataa kurejesha
fedha kesi hizo hupelekwa mahakamani. Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
"Sina idadi kamili ya kesi, lakini
kesi kama hizo ni nyingi na baadhi yake tuliposhindwa kuwapatanisha watu
wawili mnunuzi na muuzaji tuliwaambia waende mahakamani, lakini nakiri
ni kweli jambo kama hilo lipo," alisema Hanje.
Ofisa Uvuvi wa Manispaa ya Ilala,
Msongo Songoro alisema wamekuwa wakipata changamoto nyingi kuhusiana na
suala hilo ndiyo maana wameanza mchakato wa kutambua kampuni zote
zinazoingiza katika Soko la Feri samaki kutoka nje ya nchi.
Alisema hadi sasa wamebaini kuwapo kwa
kampuni 20 na kati ya hizo ni sita pekee ambazo zimewasilisha
uthibitisho wa kufuata sheria pale wanapoingiza shehena ya samaki
nchini. Songoro aliongeza kuwa kaributani moja na nusu ya samaki hao
kutoka nje wanauzwa kila siku katika Soko la Feri. Tembelea jambotz8.blogspot.com kila siku.
"Niliwahi kupata kesi kama hizo ambapo
nilichukulia kama changamoto na kuanza kufanya hiki ninachokifanya sasa
na hadi sasa ni kampuni sita pekee ambazo wameniletea vibali vyao
vinavyoonyesha uhalali wa kuagiza shehena ya samaki kutoka nje kati ya
kampuni 20 ambazo zinaagiza,"alisema Songoro.
Songoro alivitaja vitu ambavyo kila
kampuni inatakiwa kuviwasilisha kwao kuwa ni pamoja na Cheti cha Shirika
la Viwango Tanzania (TBS), Cheti cha Usajili wa kampuni, Cheti cha
TFDA, leseni ya biashara na vibali vyote vinavyoruhusu kuingiza samaki
nchini.
Ofisa Maliasili wa Manispaa ya Ilala,
Charles Seche, alisema hatua walizochukua ni mwanzo lakini lengo ni
kuondosha bidhaa zote zisizo na ubora katika soko hilo.
Ofisa Uhusiano wa TFDA, Gaudencia
Simwanza alipoulizwa alisema hafahamu kuhusu uwepo wa samaki wabovu na
kuahidi kwamba angekwenda kulijadili na wahusika.
Alimtaka mwandishi wa habari amwambie
samaki hao wameanza kuingia lini nchini, wanatoka nchini gani na
wanaitwaje, ili aweze kuwasiliana na wahusika wa idara ya chakula.
"Wewe ndiyo unaniambia nitaiwasilisha
kwenye idara ya wahusika wa chakula moja kwa moja waifanyie kazi na
baada ya kukamilisha uchunguzi nitakupa taarifa," alisema Simwanza.
Alipohojiwa baada siku moja, Simwanza
alisema jukumu la TFDA ni kuangalia mzigo ambao unaingizwa kwa wingi na
hii ni baada ya kupokea sampuli na kuridhishwa nao, kisha hutoa kibali
kwa ajili ya kuruhusu uingizwe.
"Kazi yetu sisi ni hiyo kwa mzigo
uliopo sokoni hasa wa vyakula muhusika mkuu ambaye tunafanya naye kazi
kwa karibu ni ofisa afya wa soko ambaye ndiye ana wajibu wa kukagua
mzigo na kuangalia una tatizo gani,"alisema Simwanza.
Simwanza alifafanua kuwa hata
wanapotoa kibali cha kuingiza mzigo siyo mwisho, kwani unapowasili huwa
unafanyiwa ukaguzi mwingine uwapo bandarini na ukigundulika una matatizo
unazuiliwa.
No comments:
Post a Comment