Sunday, August 04, 2013
AUA MKE WAKIBISHANA KIPI KITANGULIE KUPIKWA KATI YA MAINI NA NYAMA ....!!!
Mkazi wa kijiji cha Minyughe, wilayani Ikungi, Bonphace Misanga (70) anashikiliwa na polisi mkoani Singida, kwa tuhuma za kumpiga mkewe Amina Kunyonga (67) hadi kufariki dunia baada ya kuzuka mabishano ya nini kianze kupikwa kati ya nyama na maini.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, aliwaeleza waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea Jumanne wiki hii.
Alisema siku hiyo wanandoa hao walikwenda kwenye mnada kijijini hapo na baada ya kunywa kiasi kingi cha pombe ya kienyeji walikubaliana wanunue nusu kilo ya maini na nusu ingine ya nyama mchanganyiko ya ng'ombe, huku wakiwa tayari wamekwisha lewa.
TANESCO WAANZA KUTUMIA TRANSFORMA ZISIZOTUMIA MAFUTA KUDHIBITI WIZI
Dar es Salaam. Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limelazimika kufunga transfoma zisizotumia mafuta kutokana na tatizo kubwa la wizi wa mafuta ya transfoma kwa maeneo mengi nchini.
Meneja mawasiliano wa Tanesco, Badra Masoud amesema, shirika hilo limelazimika kufunga transfoma zijulikanazo kama ‘Dry type Transfoma’ambazo hazitumii mafuta ili kupambana na changamoto za wizi wa mafuta unasababisha baadhi ya maeneo kukosa umeme.
“Tatizo la wizi wa mafuta ya Transfoma ni kubwa, limesababisha shirika kununua transfoma zisizotumia mafuta ambazo zinapatikana kwa gharama kubwa ukilinganisha na transfoma zitumiazo mafuta ili kuepusha kutokukatika kwa umeme kwa maeneo husika,” alisema Badra
Aliyataja baadhi ya maeneo ambayo yamefungwa transfoma zisizotumia mafuta kutokana na kukithiri kwa tatizo la wizi huo kuwa ni pamoja na Mbezi Beach na maeneo mengi katika Wilaya ya Temeke.
Saturday, August 03, 2013
MAKAMU WA RAIS JANA AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA SHINDANO LA TATU LA KUHIFADHI QUR'AN TUKUFU JIJINI DAR
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza za waumini wa dini ya Kiislamu, wakati wa hafla ya
kukabidhi zawadi kwa washindi wa shindano la tatu la kuhifadhi Qur'an
Tukufu, iliyofanyika jana usiku Agosti 2, 2013 katika Msikiti wa
Istiqaama, jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi zawadi ya Sh. milioni 2, mshindi wa kwanza wa kuhifadhi
Juzuu 30, Abdulkarim Khamis, wakati wa hafla ya kuwakirimu na kukabidhi
zawadi kwa washindi hao iliyofanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama, Ilala
jijini Dar es Salaam, jana usiku.
NAPE NNAUYE AWACHEFUA WAZEE WA CCM ...!!!
Wazee kwenye mkutano wa CCM, Uwanjwa wa Community Cetre Mwanga hivi karibuni mkoani Kigoma.Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (katikati) akibadilishana jambo na mmoja wa
wanachama wakongwe wa kata ya Elerai hivi karibuni.
SIMBA YAMSAINI RASMI BEKI WA KATI NAHODHA WA TIMU YA TAIFA YA BURUNDI GILBERT KAZE
Chanzo: Shaffih Dauda Blog
KESI YA JENGO LA GHOROFA JIRANI NA IKULU LAZIDI KUWANASA WATU WENGI
UPANDE
wa Jamhuri katika kesi ya jengo refu la ghorofa 18 lililojengwa jirani
na Ikulu bila kufuata utaratibu unatarajia kuita mashahidi 13 na
vielelezo 20 kuthibitisha mashtaka dhidi ya vigogo walioruhusu ujenzi
huo.
Hayo yalielezwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Leonard Swai.
Hayo yalielezwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Leonard Swai.
Alikuwa akisoma maelezo ya awali ya kesi hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Sundi fimbo.
Swai alisema kesi hiyo itaanza kusikilizwa Agosti 7 mwaka kwa ajili ya mashahidi wa upande wa mashtaka kutoa ushahidi wao.
Washitakiwa katika kesi hiyo ni Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na Msanifu Mkuu wake Richard Maliyaga.
RAIS KIKWETE AMVAA KAGAME, MSHANGAA KWA LUGHA ZA MATUSI NA KEJELI.
RAIS KIKWETE.RAIS KAGAME.
DAR ES SALAAM. KWA mara ya kwanza Rais Jakaya Kikwete amemtolea uvivu Rais wa Rwanda, Paul Kagame kutokana na kitendo chake cha kumtolea lugha za matusi baada ya kumshauri kukaa meza moja na vikundi vya waasi wa nchi yake (FDLR), huku akimtaka kuacha kukuza mgogoro usiokuwepo.
Rais Kikwete alitoa ushauri huo kwa Rwanda
takribani miezi miwili iliyopita wakati akizungumza katika kikao cha
Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika mapema mwaka huu, mjini
Addis Ababa, Ethiopia, ambao ulikuwa ukij
adili suala la amani ya Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) pamoja na Ukanda wa Maziwa Makuu.
Ushauri huo pia uliwagusa Rais Yoweri Museveni wa
Uganda na Joseph Kabila (DRC), ambao aliwataka kufanya mazungumzo na
waasi wanaopingana na Serikali zao.
MZEE MAJUTO AFUNGA NDOA YA SIRI NA MSICHANA "MBICHI"....!!!
Mzee Majuto aliambatana na wasanii wenzake Suleiman Barafu aliyekuwa mpambe wake na mwingine aliyefahamika kwa jina la utani kama mama Sharon.
Baada ya waandishi wetu kupata taarifa kuhusu tukio hilo, waliwahi kutia timu Mbagala, nyumbani kwa binti huyo.
Baada ya kufika, waandishi wetu walibaini kuwa ni kweli kulikuwa na shamrashamra za ndoa ambayo ilikuwa ikifanyika kwa siri huku watu wakizuiliwa kupiga picha.
Muda mfupi baadaye, gari aina ya Toyota Noah (namba za usajili tunazo) lililowabeba mzee Majuto na wapambe wake liliwasili.
hakuna makato yoyote kwenye huduma ya Airtel money – “Hakatwi Mtu Hapa”
Meneja
Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando(katikati) akiongea wakati wa
uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure ijulikanayo kama Hakatwi mtu
hapa, itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure
popote pale nchini. Kushoto Meneja uendeshaji Airtel money Asupya
Naligwingwa (kulia) Meneja masoko Airtel money Rwebu Mutahaba.
Meneja
uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa akiongea na wahandishi wa
habari wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure itakayo
wawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure, pichani Meneja
Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando.
Meneja
Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando na Meneja masoko Airtel money
Rwebu Mutahaba kwa pamoja wakionyesha Bango la hakatwi mtu wakati wa
uzinduzi wa promosheni ya Airtel money Bure ijulikanayo kama Hakatwi
mtu hapa, itakayowawezesha wateja wa Airtel kutuma na kutoa pesa bure
popote pale nchini.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa huduma za mawasilino leo
imezindua ofa kabambe kwa watumiaji wa huduma ya kifedha ijulikanayo
kama ‘Hakatwi mtu hapa’ inayowawezesha wateja wake nchi nzima kutuma na
kutoa pesa kupitia huduma ya Airtel money bila makato yoyote.
Promosheni ya Airtel money Bure itatoa unafuu wa kiuchumi kwa wateja wengi wanaotumia huduma ya Airtel money.
akiongea
wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Bw
Jackson Mmbando alisema “Airtel inaongoza kwa huduma bora zenye gharama
nafuu nchini, na tunaendelea kutoa huduma zenye ubunifu kwa kuzindua
promosheni mbalimbali kwa mwaka mzima.’Hakatwi mtu hapa’ promosheni
tunayozindua leo ni mfano na mwendelezo wa dhamira yetu ya kufanya
huduma ya Airtel money kuwa suluhisho na huduma bora ya kifedha nchi
nzima”.
Kwa
upande wake Meneja uendeshaji Airtel money Asupya Naligwingwa aliongeza
kwa kusema “ promosheni hii itawawezesha wateja wa Airtel nchi nzima
kutuma na kutoa pesa kwenye mtandao wowote bila makato.
“Tunayofuraha
kuweza kutoa unafuu kwa wateja kufanya miamala ya pesa bila makato
yoyote na kuwaondolea gharama za kutuma na kutoa fedha zillizokuwepo
hapo awali. Tumeamua kufanya hivyo ili kuwawezesha wateja wetu kupata
kiasi chote cha pesa zao bila makato yoyote” aliongeza Singano.
Airtel
kwa sasa inaendesha promosheni maalumu kwa wateja wake ya Airtel
yatosha. promosheni ya ‘Hakatwi mtu hapa’ ni msisitizo unaoonyesha
Airtel yatosha ambapo huduma zote ikiwa ni pamoja na kupiga simu,
kutuma ujumbe mfupi, huduma za internet na sasa kwenye huduma ya Airtel
money ambayo inakuwa promosheni kabambe , nafuu kuliko zote nchini.
Huduma ya Airtel money sasa bila shaka Yatosha
MKOJO NA MAAJABU KWA BINADAMU DUNIANI...!!!
Mkojo kama huo ambao mwanaume huyu anajisaidia kwa kificho, kinyume cha sheria hadharani ni bidhaa ambayo inaweza kusaidia jamii kwa sasa. Na mpigapicha wetu
JOHANNESBURG, AFRIKA YA KUSINI.
JIULIZE , je, umeenda haja ndogo leo asubuhi au la?
Kama jibu ni ndiyo, basi ujue umemwaga kiasi
kikubwa cha nishati ambacho pengine kingeweza kuok
oa kiasi cha fedha za
kulipia bili ya umeme nyumbani kwako. Pia, mkojo una manufaa zaidi
kwako ambayo huenda hukuyajua.
Wanayansi na watafiti nchini Uingereza wamevumbua
nguvu za mkojo katika kuzalisha nishati ambayo inaweza kuchaji simu kwa
muda wa dakika 25 na pia kumwezesha mteja kutuma ujumbe na kuperuzi
intaneti.
Friday, August 02, 2013
MKE WA DR. SLAA ATOA KALI MAHAKAMANI....!!!
JOSEPHINE Mushumbusi, mke wa Katibu Mkuu wa CHADEMA,
Dk. Wilbroad Slaa, jana alisababisha vicheko
mahakamani baada ya kushindwa kumtambua mshtakiwa anayedaiwa kumpora maeneo ya
SUMA JKT.
Josephine alimuacha mshtakiwa katika kesi yake na kumtambulisha mshitakiwa wa kesi nyingine kuwa ni miongoni wa watuhumiwa waliomvamia.
Hayo yalitokea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa alipokuwa akitoa ushahidi kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali Leonard Chalo.
Washitakiwa katika kesi hiyo ambao wanakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha ni Getisi Mturi, Gake Mwita, Salum Mpanda na Charles Chasens.
Mturi na wenzake wanadaiwa Julai 13, 2011, eneo la Suma JKT makutano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi, walimvamia Josephine na kumpora vitu mbalimbali na kabla ya kufanya uhalifu huo walimtishia kwa silaha.
Josephine alidai Julai 13 mwaka 2011, aliingia ofisini kwake katika jengo la Mawasiliano Tower saa 2.00 asubuhi na kutoka saa 11.00 jioni kwenda nyumbani kwake eneo la Boko akiendesha gari aina ya Toyota Harrier.
Josephine alimuacha mshtakiwa katika kesi yake na kumtambulisha mshitakiwa wa kesi nyingine kuwa ni miongoni wa watuhumiwa waliomvamia.
Hayo yalitokea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa alipokuwa akitoa ushahidi kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali Leonard Chalo.
Washitakiwa katika kesi hiyo ambao wanakabiliwa na shtaka la unyang'anyi wa kutumia silaha ni Getisi Mturi, Gake Mwita, Salum Mpanda na Charles Chasens.
Mturi na wenzake wanadaiwa Julai 13, 2011, eneo la Suma JKT makutano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi, walimvamia Josephine na kumpora vitu mbalimbali na kabla ya kufanya uhalifu huo walimtishia kwa silaha.
Josephine alidai Julai 13 mwaka 2011, aliingia ofisini kwake katika jengo la Mawasiliano Tower saa 2.00 asubuhi na kutoka saa 11.00 jioni kwenda nyumbani kwake eneo la Boko akiendesha gari aina ya Toyota Harrier.
Subscribe to:
Posts (Atom)