Spika
wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) akimkaribisha Balozi wa
Rwanda hapa nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Ben Rugangazi, wakati Balozi huyo
alipomtembelea Spika ofisini kwake Dar es Salaam. Katika mazungumzo
yao, Balozi Rugangazi alimuomba Spika kupitia Bunge nchi mbili hizi
zizidi kuimarisha mahusiano mzuri yaliyopo.
Spika
Makinda alimhakikishia Balozi Rugangazi kulisimamia jambo hilo huku
akimweleza kwa muhtasari nia ya mabadiliko ya Bunge ya kuanza mkutano
wake wa Bajeti mwezi Aprili badala ya mwezi Juni kama ilivyozoeleka.
Mkuu huyo wa mhimili wa Bunge amesema hatua hii itaisaidia serikali
kuanza kutumia fedha za mapato na matumizi mara tu mwaka wa fedha wa
serikali (Julai Mosi) unapoanza. “Siku ya kusomwa bajeti kwa nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki itabakia kuwa ni ile ile ila sisi tutaanza
kujadili wizara zote za kisekta isipokuwa wizara ya Fedha hadi mwezi
Juni,” alisema Spika na kuongeza.
Balozi
Rugangazi aliifurahia hatua hiyo huku akisisitiza kuwa Rwanda inayo
mengi ya kujifunza kutoka Tanzania. Aidha Balozi huyo alitoa mwaliko na
taarifa ya maadhisho ya siku ya ‘Utu wa Binadamu’ ambayo taifa la Rwanda
huadhimisha kila tarehe 7 Aprili kwa ajili kuwakumbuka wale wote
waliouawa katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo watu takriban
milioni moja waliuawa kikatili kufuatia mchafuko baina ya kabila la
Wahutu na Watutsi.
No comments:
Post a Comment