Ni usiku wa saa 4 nipo katika eneo maarufu la
Buguruni lililopo jijini Dar es Salaam nikiwa nimekaa napata kinywaji
kwenye baa moja.
Katika eneo hilo ambalo lipo
pembezoni mwa Barabara ya Mandela si tulivu sana kutokana na pilika
pilika za magari na watu wanaopita karibu kwa shughuli mbalimbali.
Huku nikiendelea kupata kinywaji
mara naona wasichana wadogo wenye umri wa miaka 14 hadi 16 wakizunguka
zunguka katika eneo hili la baa.
Awali nilifikiri walikuwa
wakitafuta msaada au wakipita kuelekea nyumbani kwao, kwani umri wao
haukunipa picha kwamba walikuwa kazini wakati huo wa usiku wa kiza
kinene.
Kilichonifanya niwaangalie kwa
udadisi zaidi ni kuona jinsi walivyovaa nguo ambazo zilionyesha nusu ya
sehemu zao za mapaja, huku kifuani wakiwa wamevaa blauzi zilizobana
zikionyesha matiti yao madogo ambayo yanaanza kuchipua.
Hawa ni sehemu ndogo tu ya wasichana wadogo ambao hukesha usiku kucha katika baadhi ya mitaa ya jiji la Dar es Salaam wakitafuta wateja ili wapate fedha za kujikimu.
Mwandishi analazimika kuwadadisi
wasichana hawa ili kujua nini kilichosababisha waingie katika biashara
hii.
Inavyokuwa
Mwandishi ana mwita mmoja wa
wasichana hawa Neema Mashiri (16) (sio jina lake halisi) na kuongea naye
katika sehemu tulivu katika baa hiyo huku wakitumia vinywaji kunogesha
mazungumzo.
Neema akiwa mwenye kujiamini na
kazi yake bila ya kutetereka anasema kazi hiyo aliianza zaidi ya miezi
sita nyuma huku akiwa tayari amekutana na idadi ya wanaume ambayo
haikumbuki kutokana na wingi wake.
“Kwa siku moja nakutana na wanaume
katiya watano hadi saba na hii hutegemea siku na siku, kwani kuna siku
huwa na biashara ya kutosha na tunapata fedha za kutosha,”anasema Neema.
Neema akieleza ujira ambao hulipwa
anasema ni Sh3,000 hadi Sh5,000 kwa muda usiozidi dakika 30 kwa
mwanamume mmoja huku wakati kwa yule anayetaka kulala naye hadi asubuhi
hutakiwa kulipa Sh10,000 hadi Sh15,000.
“Baadhi ya wanaume wamekuwa
wakitufanyia vitendo vya kikatili kwa kutuingilia kinyume cha maumbile,
lakini kutokana na hali ngumu ya maisha hukubali kwani dau huwa kubwa
Sh10,000 hadi Sh12,000, lakini wengine hutumia ubabe tu na kututumia
bila kutulipa,” anasema
Neema na kuongeza;