Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta
Na:
Beatrice Moses
Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amewajibu wabunge wa
Afrika Mashariki akisema wengi hawahudhurii vikao vya kupewa mwongozo
kuhusu bunge hilo kwa kuwa “wanataka kulipwa posho”. Kauli hiyo ya Sitta
ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, imekuja siku moja tangu
wabunge hao waichongee wizara hiyo kwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje,
kwamba imeshindwa kuwapa mwongozo pale wanapokwenda kwenye vikao vya
Bunge la Afrika Mashariki. Akizungumza katika kikao cha kamati hiyo
jana, Sitta alisema wabunge hao wamekuwa vinara wa kuomba posho kila
wanapotakiwa
kuhudhuria kwenye mikutano ya wizara yake.
Katika
maelezo yake Sitta alimeshutumu Katibu wa Wabunge hao, Shyrose Bhanji
kuwa ndiye anayeongoza kwa kutoa udhuru mara kadhaa, hivyo kutoudhuria
vikao vinavyoitishwa na wizara hiyo.
“ Wizara
imejiwekea utaratibu mzuri wa kukutana na wabunge hao, lakini nafikiri
katibu wao ndiye anayeongoza kwa kutohudhuria,” alisema Sitta na
kuongeza:
No comments:
Post a Comment