Wednesday, March 20, 2013

HATIMAYE SERIKALI NA TFF ZAFIKIA MUAFAKA KUHUSU UCHAGUZI MKUU

Serikali imekubali mchakato wa uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uendelee kwa sharti la kuhakikisha haki inatendeka kwa wagombea waliofika mbele ya Kamati ya Rufani ya Uchaguzi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana, Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao kati ya uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo chini ya Waziri Dk. Fenella Mukangara, TFF na Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Amesema baada ya maafikiano hayo, TFF italiandikia barua Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo ndilo lililosimamisha mchakato huo ili litume ujumbe wake kwa ajili ya kusikiliza malalamiko ya wagombea walioenguliwa.

Rais Tenga ambaye ameishukuru Serikali kwa kuruhusu mchakato huo uendelee, pia ameahidi kuwa uchaguzi wa TFF utafanyika kabla ya Mei 25 mwaka huu kama walivyokubaliana na Serikali, na kuwa haki si tu itatendeka bali ionekane imetendeka.
“Serikali imetuelekeza uchaguzi ufanyike kabla ya Mei 25. Tumewaambia kwetu huko ni mbali. FIFA wakija hata kesho wakituambia endeleeni sisi tuko tayari. Hesabu zetu ziko tayari, makabrasha yote yako tayari yanasubiri mkutano tu. Labda itakuwa kutoa muda tu kwa wajumbe walioko mbali waweze kujiandaa, maana wajumbe huwezi kuwaita ghafla,” amesema.

Amesisitiza kuwa TFF ilishapanga tarehe ya uchaguzi, lakini ukasimamishwa na FIFA baada ya baadhi ya walioenguliwa kulalamika huko. Hivyo maneno kuwa TFF hawataki uchaguzi kwa sababu wanataka kuendelea kubaki madarakani haya maana hata kidogo.

Hivyo amewataka wagombea wote waliofika kwenye Kamati ya Rufani ya Uchaguzi na wakaendelea kujiandaa vizuri, kwani FIFA watakapofika watawasikiliza wao na vyombo vilivyowaengua.

Pia amesema TFF ina heshimu Serikali na itaendelea kufanya hivyo, lakini vilevile lazima iheshimu FIFA sababu iko kwenye mpira wa miguu, na FIFA ndiyo wasimamizi wa mchezo huo duniani.  

Amewakumbusha wanachama wa TFF, hasa wajumbe wa Mkutano Mkuu kufahamu kuwa TFF ina katiba, lakini ni lazima pia wafahamu kwanini kuna FIFA.

Rais Tenga amewahadharisha watu wanaopitapita mikoani kuomba saini za wajumbe ili kuita Mkutano Mkuu wa dharura wakati wanajua mkutano ulishaitishwa, lakini ukasimamishwa na FIFA. Jambo hilo kikatiba ni kosa.

MSANII MATUMAINI ANAOMBA ASAIDIWE....KWA SIKU ANAMEZA VIDONGE 39

Mchekeshaji na muigizaji wa Tanzania Tumaini Martin ‘Matumaini’ amevunja ukimya kuelezea maendeleo ya afya yake akidai kusumbuliwa na maumivu makali ya miguu kwasasa.

Akiongea na BK Cop leo Matumaini amesema kuwa anaendelea kutumia dozi ingawa hali ya afya yake bado si shwari kutokana na kugulia maumivu makali ya
miguu hali inayomfanya ashindwe kutembea.

Msanii huyo ameeleza kuwa kwa siku moja huwa anameza vidonge zaidi ya 39 lakini hapati lishe nzuri kwababu ya kutokuwa na pesa na kujinunulia chakula. 

Aidha amedai kuwa wakati alipokuwa msumbiji alipata misaada ya kifedha kutoka kwa wasanii mbalimbali lakini hasaidiwi tena tangu alipofika Tanzania.

‘Niliomba msaada kwenye magazeti ambapo niliacha namba zangu za tigo pesa lakini meseji nyingi nazopokea ni za pole; hata hivyo kuna watu wanadai wametuma kwa namba ya Michael Sangu (Mkt Chama cha waigizaji) ambayo alitoa gazetini lakini mimi sikuwahi kuonana tena na Michael tangu aliponililipia matibabu wakati natoka hospitali’. Alisema Matumaini

Mnamo Februari 9 mwaka huu Matumaini aliruhusiwa kutoka hospitali ya Amana jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa kwa siku tatu tatizo kubwa likiwa ni miguu na alitakiwa kurudi tena hospitali baada ya kumaliza dozi aliyoandikiwa na daktari.

Awali Matumaini alikwenda kuishi nchini msumbiji na kuripotiwa kusumbuliwa na maradhi, lakini alishindwa kutibiwa akiwa huko ambako Naibu Waziri wa Habari vijana na utamaduni na michezo Bw Amos Makalla akishirikiana na baadhi ya wasanii alichukua jukumu la kutoa nauli ya kumrudisha nchini. 

SOURCE::MPEKUZI::

WASANII WAMELAZIMIKA KUTOA PENZI KWA WATOTO WADOGO KWA SABABU WANAUME WAMEADIMIKA..." BABY MADAHA


MSANII wa nyimbo za muziki wa bongo fleva  anayefahamika kwa jina la  Baby Madaha amewashukia baadhi ya wasanii wa kike nchini wanaojihusisha na maswala ya ngono na wanaume wenye umri mdogo maarufu kwa jina la 'Kijibwa' kuwa ni hali ya kukata tamaa na ushamba ndio unaochangia kufanya kitendo hiko

Akizungumza jijini Dar es Salaam Msanii huyo alisema kuwa anashangazwa na baadhi ya wasanii hususani wa kike kujihusisha na maswala ya ngono na wavulana wenye umri mdogo huku wakitumia jina la 'kijibwa' kwa ajili ya kukidhi matakwa yao ya kingono


Alieleza kuwa hali ya kukata tamaa ndio chanzo kinachopelekea baadhi ya wasanii hao kujihusisha na maswala ya ngono na vijana wadogo huku wakijipa moyo kuwa wanatafuta faraja wakiwa na vijana hao

"Unajua hao wasichana wanaonekana kukata tamaa kwa kukosa mwanaume wanaolingana kiumri ndio maana ajimchukua mtoto mdogo na kumuhudumia kila kitu na ndipo hapo jina la 'kijibwa' linapotumika kwa kumfananisha mvulana huyo na mbwa unayemuudumia kila kitu huku kazi yake kubwa inakuwa ni kumlinda tu " aliongezea kuwa

"Kwa sababu mvulana huyo anapewa kila kitu ikiwemo kununuliwa hadi nguo yeye anakuwa na kazi moja tu hivyo hapo hamna mapenzi zaidi ya utumwa na kumsababisha mvulana huyo kukosa uhuru wa kuwa na maamuzi ya mambo yake binafsi" alisema Madaha

Kutokana na hicho kitendo Madaha alikiita ni ushamba kwa kuwa na mahusiano ambayo hayana msingi wowote ule na si kwa ajili ya mtazamo wa maisha hivyo mahusiano hayo hayaendana na mazingira ya nchi na kusababisha kudharaulika kwenye jamii inayomzunguka

Alitoa wito kwa wasichana hao wanaojihusisha na maswala hayo kuwa wanachotakiwa ni kujiamini na kujipanga upya kwa ajili ya kupambana na maisha na kutoyaogopa maisha hivyo wanachotakiwa ni kujipanga upya.

MSANII WA BONGO MOVIE MATATANI KWA UJAMBAZI

                                                                  Lungi Mwaulanga.
 STAA wa filamu za Kibongo, Lungi Mwaulanga hivi karibuni aliswekwa lupango katika Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar baada ya kuzushiwa kesi ya ujambazi na mpangaji mwenzake (jina tunalo).
Akizungumza na waandishi wetu, Lungi aliyesota mahabusu kwa siku mbili alisema hivi karibuni usiku wa manane aligongewa mlango nyumbani kwake na watu asiowafahamu, alipotoka alikutana na askari waliomchukua na kumwambia kwamba anatuhumiwa kwa ujambazi.

Hata hivyo, Lungi alisema kuwa baada ya kuwauliza askari ni wapi dada huyo amevunjiwa  au kitu gani alichoibiwa, askari walimbadilishia kesi na kumwambia kuwa amemtukana. Mpaka sasa, Lungi yuko nje kwa dhamana
CHANZO"GUMZOLA JIJI BLOG

WASANII WA MOVIE NA MUZIKI WAUNGANA NA MASHABIKI KUMTETEA DIAMOND


Msanii Diamond plutnum
Msanii mkali na ambaye anaongoza kwa kuandikwa sana katika vyombo vya habari Diamond platnum ameanza kupata furaha mara baada ya mashabiki kuanza kumtetea na kuonyesha kukerwa na habari zinazoendelea kuvuma kila kukicha katika magazeti,redio na hata katika tv na blog mbali mbali kuwa yeye ni fremason na nyingine zikisema anategemea waganga.



Moja Show zake Uwanja wa Taifa

Kwa wiki kadhaa sasa tumefanya utafiti na kugundua jinsi msanii huyo anavyokubalika katika jamii na hata kwa wasanii wenzake.Nadhani utakumbuka msanii Prof jay aliwahi kuandika akimtetea msanii huyu na kusema tuache majungu na kama dogo kakosea inafaa aitwe na arekebishwe na si kumponda na kumshusha kisanii kwa skendo,


Hapa akipiga Kinanda Huku Anaimba
Hivi karibuni pia baadhi ya wasanii katika page na twita zao wameonekana kuponda jinsi watu wanavyoibuka kwa kusema wao ndio waganga wanaomfanya msanii huyu kukua kisanii,wengine wakimsema mganga huyo kuwa kama anataka kumshusha Diamond basi ajipandishe yeye aimbe au awasaidie ndugu zake waimbe ili wapate pesa kama diamond na wasaidie.Wadau hao wamefika mbali na kulaani maneno ya watu kumzushia msanii huyo kuwa yeye ni fremason ...Kiukweli kwa sasa hapa nchin tanzania kumeibuka tabia ambayo hata haileweki imetokea nchi gani hadi kufika hapa kwani msanii akifanikiwa kidogo tu basi ujue atahusishwa na fremanson,nadhan mtakubaliana na mm kuwa hata kwa marehem kanumba walisema ni fremason wakaja kwa ray,jackline wolper na sasa kwa Diamond sasa swali la kujiuliza ni kwamba kuna mtu hata mmoja ambaye alikutana naye huko kwa hao jamaa akathibitisha juu ya uhalali wawasanii wetu kuwa huko?ukiwauliza utasiki sijakutana nae lakini huoni amepata mafanikio ya haraka lazima atakuwa fremason yule jaman hebu tubadilike tuswe watu wakumuabudu shetan kila saa alisema mama brayan

Kiukweli inakatisha tamaa na tutabaki hivi hivi hatutakuwa na wasanii wazuri wala wachezaji wazuri kwa sababu hatujui kuthamini vya kwetu alisema bwana mikidadi wa masaki huku bwana Ally Jo akisema anashangazwa sana na staili ya hapa bongo Nadhani hii inatokana na watu kuijua fremason juzi juzi ndio maana kila mtu akipata pesa kidogo tu za kununua nyanya basi ni fremason hebu tuelimike jaman tuache ubabaishaji tupende na kuthamini wasanii wetu


Baada ya yote hayo mwandishi wetu aimvutia wayaJack Wolper na kumuliza anajisikiaje kuhusishwa na imani ya fremason.Binafsi sipendi kuhusishwa na jambo ambalo sijalifanya wala sina ndoto nalo na siwezi kulifanya hebu jiulize super star mimi na fremason wapi na wapi kwa pesa gani nilizo nazo hadi niwe fremason hebu watu wasitake kujulikana kwa kutunga habari za uwongo,Utasikia eti diamond naye ni fremason jaman kwa hiyo prado au?basi hao fremason wana kazi.Alisema jack huku akionyesha dhahiri kukerwa na watu hao wanaotunga habari za uwongo

Msanii vicent Kigosi (Ray)


Kwa upande wa Ray alisema yeye hana la kusema kwani kama ni maneno kashayazoea hivyo hawezi kumzuia mtu kusema maana ni binadamu na wamezaliwa wanasema kwa hiyo hawampi tabu.Unajua kaka hawa ni binadamu huwezi kuwazuia cha msingi ni kufanya kazi sana ili uendeleze maisha yako ila ukiwasikiliza utaharibikiwa ndugu yangu,mimi nimezoea ila na mshauri mdogo wangu Diamond akomae afunge masikio kwa yale anayoona hayana faida na afungue masikio kwa yale yenye faida na yeye Alisema Ray Kwa upande wa Diamond alisema kuwa bado anaimani kubwa sana na mashabiki wake kuwa hawatamuangusha kwa kuwa amekula kiapo kuwatumikia na kamwe hatafanya kinyume na hilo....Kaka sina mengi ila nachoweza kusema mashabiki wangu wasivunjike moyo haya ni mapito tu na yataisha so cha msingi wajue Diamond wao ni yule yule wa kamumbie mbagala ni yule yule wa kesho so nawapenda sana hizo ni stori tu kama movie na mungu atawanyoosha kwani yeye ndiye anayenijua zaidi yao kikubwa sintatetereka kwa maneno yao nimeandaa nyimbo za kutosha kwa ajili ya watu wangu u know sasa hayo maneno hayatani felisha kwakuwa namtegemea mungu.Alisema Diamond



Moja ya Show zake

Kwasasa Diamond ni msanii anayeongoza kwakufanya shoo nyingi sana ndani na nnje ya nchi huku wengine wakimtaja kama msanii mwenye mafanikio zaidi,kwa upande wake dimond amesema anashukuru mungu kwa kupiga hatua na anategemea kuingiza gari mpya na lenye thamani kubwa sana ukiachilia mbali Prado analomiliki hivi sasa,Pia msanii huyo ameweka wazi kuwa anamalizia mjengo wake ambao umebakia hatua ndogo sana kukamilika na soon atahamia huko na familia yake kwa sasa msanii huyo ana miliki Toyota prado na Alteza aliyomnunulia mama yake.

Mashabiki wa diamond

Mashabiki wa Diamond Waliofurika kupata show
The super stars tz inapongeza sana Diamond na kumtaka kukaza buti na asife moyo kwani bado anasafari ndefu sana ya muziki wakehivyo asilewe sifa wala asiumizwe na yanayotokea kwani hata fid Q alisema usuperstar mzigo wa mwiba ukiubeba utaumia.

Read more

Kikosi cha Morocco kutua nchini Ijumaa tayari kuikabili ‘Taifa Stars’ jijini Dar kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia

Timu ya Taifa ya Morocco (Lions of the Atlas) inatarajiwa kuwasili nchini kesho kutwa Ijumaa kwa ndege ya Emirates tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania (Taifa Stars) itakayochezwa Jumapil9 na waandishi wa habari 12 utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 8.55 mchana na utafikia hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency.
Siku hiyo Morocco inatarajia kufanya mazoezi jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karumei katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Msafara wa timu hiyo yenye watu 58 wakiwemo maofisa
na Jumamosi itafanya mazoezi yake ya mwisho kwenye Uwanja wa Taifa kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa saa 9 kamili alasiri.
Wachezaji walioko kwenye kikosi hicho chini ya Kocha Rachid Taoussi ni Nadir Lamyaghri, Anas Zniti, Yassine Bounou, Younnes Bellakhadar, Abdellatif Noussair, Abderrahim Achchakir, Zoheir Feddal, Younnes Hammal, Zakarya Bergdich na Abdeljalil Jbira.
Issam El Adou, Kamel Chafni, Salaheddine Saidi, Mohamed Ali Bamaamar, Abdelaziz Barrada, Salaheddine Aqqal, Abdessamad El Moubarky, Nordin Amrabat, Chahir Belghazouani, Abdelilah Hafidi, Youssef Kaddioui, Brahim El Bahri, Hamza Abourazzouk na Youssef El Arabi.
Wakati huo huo, tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa keshokutwa katika vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Uwanja wa Taifa na Dar Live Mbagala.
Milango siku ya mechi kwa ajili ya watazamaji itafunguliwa saa 6 kamili mchana

Kwa mujibu wa matokea ya kura nchini Zimbabwe Wananchi waunga mkono Katiba mpya.

Wapiga kura nchini Zimbabwe wameunga mkono mabadiliko ya katiba.
Katika kura ya maoni iliyopigwa mwishoni mwa wiki ililopita, asilimia 95 ya wapiga kura hao wamepiga kura ya ndio.
Kura hiyo imetayarisha mchakato wa uchaguzi mwishoni mwa mwaka huu, ambao utamaliza kipindi cha utawala wa mpito wenye mivutano, unaoshirikisha rais Robert Mugabe na mpinzani wake Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai.
Mabadiliko hayo ya katiba yanaweka kikomo cha mihula miwili ya miaka mitano kwa rais, na yanalipa bunge madaraka makubwa.
Mabadiliko hayo hali kadhalika yanaondoa wadhifa wa Waziri Mkuu.-DW.

2015: URAIS WA DAMU.

GENGE HATARI LAIBUKA, CCM, CHADEMA VYAHUSISHWA.
Dk Steven Ulimboka akiwa chumba cha wagonjwa mahututi MOI.
Mhariri Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda, akiwa ndani ya Ndege ya Flightlink.
Daudi Mwangosi aliyekuwa mwandishi wa chanel ten akisulubiwa na askari polisi na kumfyatulia bomu la machozi mwilini na kupoteza maisha mkoani Iringa. Mkurugenzi Mtendaji wa Hali halisi publishers Ltd, Saed Kubenea akiwa katika wodi ya Hospitali ya Apollo, New Delhinchi INDIA mara baada ya kufanyiwa Upasuaji macho, Kubenea amekuwa akitibiwa katika Hospitali hiyo tokea mwaka 2008 alipomwagiwa tindikali katika ofisi yake jijini Dar es Salaam na hii ni operesheni yake ya tano.

Balozi Seif Ali Idd azindua rasmi safari za ndege za kitalii moja kwa moja kutoka Afrika Kusini hadi Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisoma hotuba ya uzinduzi rasmi wa safari za watalii kutoka moja kwa moja Afrtika kusini hadi Zanzibar kwa usafiri wa shirika la Mango Airlines katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar Kisauni Nje kidogo ya mji wa Zanzibar. (Picha na Hassan Issa wa – OMPR-ZNZ).
Rubani wa Ndege ya Shirika la Mango Airlines Kepteni Kevin Viljoen akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Zanzibar kuanza safari za kuleta abiria kati ya Afrika Kusini na Zanzibar. Nyuma ya Kepteni Kevin ni Kaimu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Juma Dunia Haji.
Baadhi ya Watalii 175 waliotua uwanja wa ndege wa Zanzibar kwa kutumia ndege ya shirika la Mango Airlines wakifurahia ukarimu wa kinywaji cha dafu mara tu baada ya kutua uwanjani hapo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akimaliza kuzindua safari za ndege za shirika la Mango Airlines kati ya Afrika Kusini na Zanzibar katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar uliopo Kisauni. Kulia yake ni Kaimu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Juma Duni Haji na Kushoto yake ni Mwakilishi wa Shirika la Mango Airlines hapa Zanzibar Bw. Javed Jaffery.

Lowassa afufua kashfa ya kigogo Ikulu

Dar es Salaam. Sakata la Mkuu wa Itifaki wa Ikulu, Anthony Itatiro, ambaye anahusishwa na njama za kutaka kuchota kiasi cha Sh3 bilioni kwa ajili ya safari hewa ya Rais, limechukua sura mpya baada ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje kutaka kujua hatima ya kigogo huyo jana.
Itatiro na maofisa wanne wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walituhumiwa mwaka jana kuidhinisha kuchota kiasi hicho cha fedha bila ya kuwapo kwa ziara ya Rais kwenda nchi yoyote ya kigeni.
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Juma Mahadhi alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa swali na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Bunge, Edward Lowassa.
Lowassa, ambaye pia ni Mbunge wa Monduli aliuliza swali hilo ghafla kwa Mahadhi wakati akitoka nje, baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati yake kilichofanyika kwenye ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam.
Mahadhi, ambaye alilazimika kutoa ufafanuzi wa swali hilo baada ya kubanwa zaidi na waandishi wa habari, alisema Rais Kikwete ndiyo mwenye mamlaka ya kuchukua hatua dhidi ya Itatiro kutokana na ripoti ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi wa Ndani wa Wizara hiyo.
Alisema pia kuwa walishauriwa kuwa maofisa walioshirikiana na Itatiro nao wachukuliwe hatua za kinidhamu kufuatia njama hizo.
Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu Ombeni Sefue hakupokea simu. Pia hakujibu pindi alipotumiwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu. Naye Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utumishi, George Yambesi alisema hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kwani alikuwa likizo.
Mahadhi alisema wakati tukio hilo linatokea viongozi wakuu wa wizara hiyo walikuwa kwenye majukumu mengine ya Serikali, jambo ambalo lilisababisha nafasi zao kukaimiwa na watendaji hao.
“Wale maofisa walitumia mwanya wao wa kukaimu nafasi ile ndiyo wakasuka mpango huo,” aliongeza Mahadhi.
Alisema kutokana na hali hiyo baadhi ya maofisa hao wamechukuliwa hatua za kinidhamu ikiwamo ya kuwashusha vyeo na kuwabadilisha vitengo.
Mahadhi alisema kwamba huwa ni utaratibu wa kawaida kwa Rais anaposafiri maofisa wa Itifaki na wale wa Wizara ya Mambo ya Nje kupewa fedha na hazina kwa ajili ya kufanikisha ziara zake.

KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU YATEMBELEA DARAJA LA KIGAMBONI LEO

Mkurgenzi Mkuu wa Shirika la taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhani Dau akifafanua jambo mbele ya wajumbwe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu walipofanya ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi wa daraja la Kingamboni jijini Dar es Salaam leo. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ramadhan Dau (wa pili kushoto) akiangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni wakati Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea mradi huo leo. Kushoto ni Mhandisi wa NSSF, John Msemwa.
 Mhandisi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), John Msemwa akitoa mada wakati Kamati ya Bunge ya miundombinu ilipotembelea mradi wa ujenzi wa daraja la Kigamboni..
 Naibu Waziri wa
Ujenzi, 
Gerson Lwenge akizungumza wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi wa Ujenzi
wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam leo. 
 Kamati ya Bunge ya Miundombinu ikiangalia maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo.
 Mafundi wakiwa kazini.
 Mafundi kazini.
 Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Peter Selukamba (kushoto) akiwa na Naibu Waziri
wa Ujenzi, 
Gerson Lwenge wakati kamati hiyo
ilipotembelea mradi wa Ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Hapa moja ya za daraja la Kigamboni itawekwa hapa.
 Mhandisi wa Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Karim Mattaka akifafanua jambo kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mradi
wa daraja la Kigamboni. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Peter Selukamba. 
 Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu akiwa na Ofisa wa Trafic, Peter.
 Mhandisi wa NSSF, John Msemwa akitoa ufafanuzi wa maendeleo ya ujenzi wa daraja la Kigamboni kwa Mkufugenzi Mkuu wa NSSF, Ramadhan Dau (kulia)
 Zege ikimiminwa katika moja ya nguzo za daraja hilo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Peter
Selukamba (kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Ujenzi, 
Gerson Lwenge wakati kamati
hiyo ilipotembelea mradi wa Ujenzi wa daraja la Kigamboni jijini Dar es Salaam leo.

KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS YAZINDULIWA RASMI LEO

kili1Meneja wa bia ya Kilimanjaro Bw. George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBL Masaki wakati alipozungumzia uzinduzi wa Tuzo za Kilimanjaro Music Award na kuasiniwa kawa mkataba wa udhamini wa Tuzo hizo kati ya kampuni ya TBL na BASATA.kili2Kushilla Thomas Mkurugenzi wa Masoko wa TBL akibadilishana hati na Godfrey Mngereza Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, huku viongozi wengi9ne wa TBL na BASATA wakipiga makofi.kili3
Katikati ni Kushilla Thomas Mkurugenzi wa Masoko wa TBL kulia na Godfrey Mngereza Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA kushoto pamoja na Maofisa wa TBL na BASATA wakifurahia jambo mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa nembo  ya Kilimanjaro Music Award.
Tuzo za muziki maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam zikiwa na dhumuni kubwa la kutambua wasaniii waliopata mafanikio katika sekta ya muziki kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
George Kavishe, Meneja wa  kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager amesema wakati wa uzinduzi huo kuwa, “Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kuendelea kudhamini  tuzo hizi kwa mara ya 12 sasa lengo likiwa kukuza muziki nchini Tanzania. Mchakato wa kuwapata wanamuziki bora wa mwaka unaanza leo na utamalizika tarehe 8 Juni ambapo tutakuwa na hafla ya usiku maalum wa kwa ajili ya kutangaza washindi.”
Alisema Kilimanjaro Premium  Lager imejizatiti kuendeleza tasnia ya muziki Tanzania kwa kutambua na kuwapa tuzo wasanii wenye vipaji. ‘Tunataka  wanamuziki  wetu wajisikie wanathaminiwa na kutambuliwa kwa kazi nzuri wanayoifanya  vile vile tunataka Watanzania  waweze kuthamini muziki wa nyumbani na kutambua mchango wa wanamuziki katika kuleta maendeleo ya uchumi katika nchi.
‘’Kilimanjaro Premium Lager inajivunia  kuwa sehemu ya tuzo hizi na ni matumaini yetu kua mwaka huu tukio hili litakua kubwa na zuri zaidi’’
‘’Pia tuna furaha kutangaza  kwamba BASATA imetupatia leseni ya kuendelea kudhamini tuzo hizi kwa kipindi cha miaka mingine mitano. Kusainiwa kwa mkataba mpya na BASATA ni uthibitisho wa azma kubwa tuliyonayo katika kuendeleza muziki wa Tanzania. Mkataba huu utaifanya Kilimanjaro Premium Lager kuwa mdhamini wa tuzo hizi mpaka mwaka 2018.

Tuesday, March 19, 2013

MWANAMKE MWENYE WAUME WATANO, AMBAO WOTE NI MAKAKA WA FAMILIA MOJA NA ANALALA NA KILA MMOJA KWA SIKU TOFAUTI

 Huyu ni dada Rajo Verma, mwenye umri wa miaka 21 kaolewa na wanaume watano na cha ajabu zaidi ni kua wanaume hao wote ni ndugu. Rajo anasema kua kutokana na kua na uhusiano na wanaume hao watano imekua ngumu kwake kujua nani ni baba wa mtoto huyo, kwani hulala na wanaume hao wote kwa zamu. Yani leo ni zamu ya huyu na kesho ni zamu ya mwingine.

Wa kwanza kumuoa ni Guddu mwenye umri wa miaka 21, yeye anasema haoni wivu mke wake kulala na kaka zake kwani  ni ndugu zake na wanaishi kwa amani na upendo kama familia moja. Ndugu wengine wa Guddu ni  Bajjumwenye miaka 32, Sant Ram mwenye miaka 28, Gopal mwenye miaka 26, naDinesh ambaye amefikisha miaka 18 mwaka huu.

Rajo anasema kua kipindi anaolewa na mme wake wa kwanza alijua kwamba ni lazima awakubali wanaume hao,kwani hata mama yake Rajo alikua kaolewa na wanaume watatu ndugu wa familia moja

Mwandishi mwingine anusurika kutekwa

Andrew Chale Mwandihi wa Gazeti la Tanzania Daima anayedai kufanyiwa jaribu la kutekwa
Dar es Salaam
MWANDISHI wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima Andrew Chale ameanza kuishi maisha ya wasiwasi baada ya watu wasiojulikana kufanya jaribio la kumteka.
Akizungumza naHabarimpya.comChale alisema kwamba siku ya Jumamosi usiku watu wasiojulikana walikuwa wakifuatilia nyedo zake.
Alisema watu walikuwa kwenye magari mawili yenye rangi na namba za Jeshi la Polisi walikuwa wakimfuta nyuma kila alipokuwa akipita kuelekea nyumbani kwake maeneo ya Sinza jijini Dar es Salaam.
"Siku ya Jumamosi usiku nikiwa njiai kutoka Kazini, niliona magari mawili ya Polisi yakinifuata kwa karibu na baada ya kuingia uchochoro flani wakuingia nyumbani magari hayo yakapaki"alisema Chale na kuongeza"
"Watu waliokuwa eneo hilo walisema kwamba baada ya magari hayo kupaki wakakaa hapo kwa saa mbili na baadaye walishuka askari watu huku wawili wakivaa nguo za kiraia huku mmoja akiwa na Gazeti la Tanzania Daima mkononi".
Alisema kwamba baada ya watu hao kushuka na kuuliza mtu waliemwita kwa jina la ANDRESON,, ndipo wakaambiwa kwamba hakuna mtu mwenye jina hilo katika mtaa huo lakini , walipoelezea mwonekano wake, wakajibiwa kuwa kijana anayefahamika eneo hilo hupita tu lakini mahali anapoishi hapajulikani.
"Tunayemfahamu ni kijana mmoja ila huwa anapita hapa akiwa na hilo Gazeti majira ya usiku, na wakati mwingine huwa anapita hapa akiwa na mambo yake mengine, baaada ya hapo magari hayo yaliondoka"aliwanukuu mashuhuda wa tukio hilo.
"Watu hao walirudi tena hadi nyuma ya nyumba yangu na nikawasikia wakijitambulisha kuwa wao ni Polisi jamiii na kwamba walikuwa wakimtafuta kijana mmoja ambaye wamesahau anapoishi"alifafanua Chale. SOURCE JAMII FORAM

TAARIFA ZA KIMICHEZO KUTOKA SHIRIKISHO LA LEOMPIRA WA MIGUU TFF


tff_LOGO1

KIINGILIO MECHI YA STARS, MOROCCO 5,000/-
Kiingilio cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco (Lions of the Atlas) itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani.
 Viti vya kijani katika uwanja huo wenye uwezo wa kumeza watazamaji 60,000 viko 19,648. Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu ambavyo viko 17,045 ni sh. 7,000. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 ni sh. 10,000.
 Viingilio vya daraja la juu ni kama ifuatavyo; VIP C yenye watazamaji 4,060 ni sh. 15,000 wakati sh. 20,000 ni kwa VIP B yenye watazamaji 4,160. VIP A yenye watazamaji 748 kiingilio chake ni sh. 30,000.
 Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo itakayoanza saa 9 kamili alasiri zitaanza kuuzwa siku mbili ya mchezo (Ijumaa na Jumamosi) katika vituo vifuatavyo; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni na Dar Live Mbagala.
 Katika vituo hivyo tiketi zitauzwa katika magari maalumu. Magari hayo pia yatafanya mauzo ya tiketi uwanjani siku ya mechi. Vilevile tunapenda kuwakumbusha watazamaji kutonunua tiketi mikononi mwa watu au katika maeneo yasiyohusika ili kuepuka kununua tiketi bandia, hivyo kukosa fursa ya kushuhudia mechi hiyo.
 SAMATA, ULIMWENGU WARIPOTI STARS
Washambuliaji wa Taifa Stars, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wamewasili nchini jana usiku na kwenda moja kwa moja kambini.
 Ujio wa washambuliaji hao unafanya idadi ya wachezaji walioripoti kambini kufikia 20 kati ya 23 walioitwaa baada ya mshambuliaji Khamis Mcha aliyekuwa na kikosi cha timu yake ya Azam nchini Liberia naye kuripoti kambini leo asubuhi.
 Wachezaji John Bocco na makipa Mwadini Ally na Aishi Manula ambao pia nao walikuwa Liberia na timu yao ya Azam wataripoti kambini leo alasiri. Wachezaji hao ni sehemu ya msafara wa timu ya Azam ambao utakuja na ndege ya mchana kutokea Nairobi kwa vile ile ya asubuhi waliyotangulia nayo wenzao kuwa imejaa.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...